Wednesday, 2 April 2014

KWA NINI PRESIDENT KIKWETE ALISHINDWA KUELEWA KUWA WANADIASPORA TULINYIMWA HAKI YETU.YA KUTOA MAONI

Sina nia Kumjibu Rais Kikwete lakini imenilazimu baada ya kusikiliza hotuba yake ya London Juzi kuwa Watanzania walioko nje hawaoneshi kuwa wanataka uraia Pacha .Lakini hofu kubwa iliotanda Kwa chama cha Mapinduzi kuwa Watanzania  walioko nje hawaiungi Mkono CCM ndio ikaamuliwa kuwa tume ya kuchukua maoni ya Watanzania walioko nje isije kuchukau maoni ya Watanzania hawa ingawa Ubalozi wetu hapa Washington DC ulitoa Tamko Kuwa tujitayarishe kutao maoni yetu.

Watanzania wengi waliko nje walikua na madai mawili makubwa kama waliyokua nayo Jirani zetu Kule Kenya na Msumbiji na Rwanda  .Haki ya Kuwa na Uraia zaidi ya Mmoja kwa Mtanzania ndani ya ktiba mpya  na Haki ya kupiga kura , Lakini bado Rais Kikwete ameeendelea na Kauli yake kuwa munataka kula huku na huku alishindwa kueleza na kuwaomba samahani Watanzania miloni tatu wlioko nje kwa kushindwa kuwashirikishwa kutoa maoni yao na kuwemo na wao kuwa walishiriki kuunda Katiba Mpya .

Jee Huu Ustadh Kikwete ni Uungwana kuwanyima Watanzania miloni tatu waliko nje haki ya  kushiriki Mchakato huu wa Katiba ?.Baada ya ubalozi kuwaambia watu kuwa  Tume haina nafasi tena kuja huku nje  tunajua ilikua ni moja ya ajenda ya CCM kuwanyima Watanzania waliko nje haki ya kushiriki kuunda katiba Mpya.
Jee Mtanzania alieko nje hana thamani bali thamani yake ni zile senti anazotuma nyumbani tu ?
Mheshimiwa Rais uanposema hatuoneshi juhudi kupiganai uaraia pacha ilikua tuanze kwa kutoa maoni mengi ya watanzania miloni tatu wa vyama vyote na wasiokuwa na Vyama lakini fursa hiii tulivyimwa hapa ndio ilikua sehemu ya kuazia kupiganai haki za Mtanzania alieko nje Jee huku ndio unakotupeleka Mheshimwia Rais Kikwete Watanzanai tuliko nje ?

No comments: