Tuesday, 1 April 2014

SERIKALI TATU NDIO SULUHISHIO

fedha
Fact 1: makusanyo ya kodi bara ni trilioni 33.2 tsh, zanzibar ni trilioni 1.2 tsh. Quote ya Mhe. D. Haji (28.3.2014 star tv).
Anaendelea katika uchambuzi kwamba kwa mantiki ya hesabu za haraka, uchumi wa tanganyika ni mkubwa mno ukilinganisha na wazanzibar. Na hii inatambulika tokea ya kabla ya mapinduzi, uchumi wa bara ni mkubwa mno kulinganisha na bara. Lakini ukitaka kufanya utafiti yakinifu, tuangalie factor nyengine zinazodefine uchumi wa nchi including population zetu.Anaendelea kwamba uchumi unakwenda na wingi wa population, mfano tanganyika ikiwa na watu milioni 43 katika uchumi huu wa ukusanyaji wa trilioni 33.2 za mapato utakuta mwananchi wa upande tanganyika anakuwa na shilingi 800 za kitanzania wakati ukitazama kwa uchambuzi zaidi kwa upande wa visiwani, trilioni 1.2 za kitanzania zitagawiwa kwa kila mzanzibari kwa thamani ya shilingi 900 na kitu.
Hapo ndipo anaposema wingi wa hesabu zinazotajwa hazitazamwi kwa ukweli wa hali halisi. Moja ya propaganda kubwa ya kuviza mabadiliko ya mfumo wa muungano ni hoja za mapato na uchumi mkubwa bara kulinganisha na zanzibar. Nafikiri kwa njia hii ya ukusanyaji wa mapato ni ishara nzuri ya kupima nyenzo za kudelegate madaraka kwa nchi husika katika mfumo mpya wa serikali tatu ili kuupa ufanisi mzuri ulio na haki na usawa baina yetu kwa yale tutayokubali kubakia ndani ya muungano. Kwa misingi wa hizi statistics hakutakuwa na kauli ya kwamba zanzibar itashindwa kuchangia katika muungano, kwa maana ya kwamba michango hio itaendana na approach ya uwiano wa mapato in relation to population zetu, ardhi na matumizi ya nchi husika.
Hoja kubwa ni bajeti ya ulinzi, zikitajwa trilioni nyingi ili kuleta khofu katika uchambuzi wa uchangiaji. Visiwani hivi sasa bajeti inayotengwa jeshini ni ndogo mara mia ukilinganisha na ya bara. Hii inatokana na udogo wa ardhi yenyewe, na kuwa hakuna border ya zanzibar iliona challenges za kiusalama mkubwa au kuwa remote isiofikika kwa urahisi. Hata population ya wanajeshi wetu visiwani ni ndogo hivyo matumizi kwa zanzibar yako zaidi katika masuala ya ceremonial, itifaki na strategies za emergencies, wakati kwa upande wa bara, ni kubwa kutokana na ukubwa wa ardhi, population, sababu za kiusalama hasa tukiwa mpakani na nchi zenye matatizo ya security na changamoto nyingi tu. Hivyo hakuna hoja ya kutotazama population, ardhi na mahitaji ili kujuwa mchango wa defence utakuwa wa uwiano gani ukilinganisha na upande wa zanzibar. Linakuzwa tu kutunyima haki ya kufanya informed decision based kwa ukweli wa uhakisia wa mambo yalivyo.
Gumu la kulimezea ni namna gani decisions za matumizi zitaangaliwa. Kwa mfano mdogo manunuzi ya radar ya jeshi yalioitia doa tanzania kwa kuwa thamani ya radar ilikuwa kubwa mno na kwa evidence kutoka kwa experts hakukuwa na sababu yetu kununua kwa gharama hizo kitu kikubwa kisichohitajika. Report ya house of commons iliitia mashakani kampuni ya uingereza ya defence system BAA kwa kuwa ilifanya transaction hii ya uuzaji wa radar kwa misingi ya kutoa rushwa. Hili tungelibeba sote watanzania na ndio moja ya sababu tunayoitazama kama ni ongezeko la bajeti ya defence kubwa isiobebeka.
Nani anafaidika na haya manunuzi na matumizi makubwa ya defence? Ukitazama report hio ya house of commons utakuta kuna nyufa za corruption zinazofanyika katika misingi ya sasa ya mfumo wa serikali mbili. Katika mfumo wa serikali tatu, hakuna nchi mshirika atakaekukubali kuchangia bajeti yenye ishara ya corruption na incompetence, na ndio tukasema mfumo wa tatu utaleta ufanisi kwa serikali kuu na kuwa fit for purpose. Tutaendelea..

No comments: