Wednesday, 10 September 2014

WATANGANYIKA KUPIGANiA NCHI YAO NJE YA BUNGE LA CCM !

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Said Arfi. Suala la Serikali tatu limeibuka upya katika Bunge Maalum la Katiba, baada ya mjumbe wa Bunge hilo, Said Arfi (pichani), kusema kuwa Serikali ya Tanganyika haiwezi kuepukika licha ya wajumbe wa Bunge hilo kuikandamiza. Alitoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa.
NA WAANDISHI WETU
9th September 2014
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Said Arfi.
Suala la Serikali tatu limeibuka upya katika Bunge Maalum la Katiba, baada ya mjumbe wa Bunge hilo, Said Arfi (pichani), kusema kuwa Serikali ya Tanganyika haiwezi kuepukika licha ya wajumbe wa Bunge hilo kuikandamiza.
Alitoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akisoma taarifa ya wachache ya Kamati namba 10 na kusema kama serikali tatu haitopatikana ndani ya Bunge hilo walio nje wataipigania.
Kauli hiyo ilizusha mvutano mkubwa ndani ya Bunge na kusababisha uongozi wa Bunge hilo kumkatisha na kumtaka kutozungumzia suala la muundo wa serikali kwa sababu halipo kwenye majadiliano.
Licha ya kukatazwa, Arfi alisema wajumbe wachache waliomo ndani ya Bunge hilo wanaheshimu maoni ya wananchi na ndiyo maana wanapigania uwepo wa serikali tatu.
Akifafanua maoni ya wachache, Arfi alisema muundo wa serikali tatu utazuiwa na walio wengi ndani ya Bunge, lakini wale walio nje ya Bunge hilo wataendelea kuidai serikali hiyo.
Alisema maudhui katika Sura ya 11 na 15 yanagusa serikali tatu na Tanganyika hivyo anashangaa kwa nini kila wanapogusia suala hilo wao wanaona kero.

“Sisi tunazungumzia maudhui yaliomo katika Sura ya 11 na 15 na kama wanaona hawayataki…basi haya ndiyo maoni yetu,” alisema.Aidha, Arfi aliutaka uongozi wa Bunge kuwatendea haki wajumbe walio wachache waliomo ndani ya Bunge hilo kwani hawakukubalina na maoni ya walio wengi ya kufuta neno Tanganyika au nchi washirika.
“Tumetafakari sana jambo hili la kudai uwapo wa Tanganyika halikuanza katika Tume ya kukusanya maoni lilisikika huko nyuma katika kundi la watu 55, wakatishwa wakatishika, wakanyamaza… likaibuka tena wakati wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Abood Jumbe, akawajibishwa na sasa limejirudia tena,” alisema.
“Walio wengi humu ndani wasijifanye vipofu kutokuliona tatizo…tatizo lipo na ufumbuzi wa tatizo ni kuwapo kwa serikali ya Tanganyika ili kuondoa kero na kudumisha Muungano imara wenye ridhaa ya pande zote…sisi tulio wachache tunasema muda wa viongozi kuwaamria wananchi umekwisha na sasa ni muda wa viongozi kuwasikiliza wananchi wanataka nini,” aliongeza Arfi.
Hata hivyo, wakati Arfi akiendelea kuzungumza, mjumbe Amon Mpanju alisimama na kuomba muongozo kutokana na kutoridhishwa na kauli iliyotolewa na Arfi.
Mpanju alisema: “Mheshimiwa mwenyekiti na waheshimiwa wajumbe, sijasimama kwa ajili ya kupinga maoni yanayotolewa na mjumbe anayewasilisha (Arfi) ila lugha anayoitumia, ukisema usitufanye vipofu inamaana vipofu hawana thamani.”
Hata hivyo, Arfi aliwataka radhi wale wote ambao amewakwaza kutokana na kauli yake na kudai kuwa neno hilo limo ndani ya Kamusi na hadhani kama amelitumia
CHANZO: NIPASHESerikali ya Tanganyika yaibuka tena Bungeni

No comments: