Wednesday, 1 October 2014

SHAKING OF THE UNION WILL ZANZIBAR REPEAT IT MISTAKES ! MPASUKO WA MUUNGANO WA TANZANIA


Utawala Wa Karume ulimuweka jela Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakati huo Wolfgong Dourado pichani chini kwa kuuhoji Mungano na sasa Mwanasheria wa Zanzibar  kulia pichani asimama na Zanzibar anasema hatoiuza Zanzibar kwa kilo ya sukari.
Katika hali ya kawaida, Muungano linatakiwa lionekane ni jambo la kheri maana linamaanisha kuunganisha nguvu na kupata mafanikio ya pamoja. Kama hivyo ndivyo, Muungano haupaswi kufanywa kwa vitisho, ubabe, ghilba, hadaa na udanganyifu.
Ajabu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kwamba tokea kuasisiwa kwake, misingi yake imejengwa juu ya kuiburuza Zanzibar na kutumia ghilba, hadaa na udanganyifu na sasa inapoonekana hivyo pia havisaidii vimekuja vitisho na ubabe.
Kwa nini ilikuwa hivyo 1964 na inakuwa hivyo hata sasa 2014 ikiwa ni miaka 50 tokea kuasisiwa kwake? Jibu ninalolipata mimi ni moja tu - nalo ni kwamba wakati Zanzibar inaamini imeingia kwenye Muungano, Tanganyika inadhani imejiongezea eneo linaloitwa Zanzibar ambalo inaliona kama ni koloni lake.
Mwaka 1964, Zanzibar iliingizwa kwenye Muungano huku ikikosa au pengine ikikoseshwa ushauri wa kisheria wa Mwanasheria Mkuu wake, Wolfango Dourado. Na sasa 2014, wakati tunaambiwa Katiba Mpya ya Muungano inaandikwa, tumeshuhudia wale wanaopaswa kuwa washauri wakuu wa kisheria wa Zanzibar ambao ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Abubakar Khamis na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, wakijiweka mbali na uandishi huu wa rasimu ya Katiba inayopendekezwa isiyozingatia maslahi ya Zanzibar.
Wanachopaswa wakijue watawala wa CCM  Tanganyika ni kwamba 1964 siyo 2014. Chambilecho mwanamapinduzi Hassan Nassor Moyo; alipomwambia Samuel Sitta pale ukumbi wa Bwawani kwamba "Hawa unaowaona hawa... hawa vijana wa Zanzibar.... hawa wamesoma hawa... hawakubali tena sasa kuburuzwa." kUTOKA wall ya Mwakilishi wa Mji Mkongwe Islamil Jussa.
Ushauri wangu watawala wetu waangalie Jiji la HONG KONG Jinsi dola ya Uchina inavyosawijika na vijana wa kileo wa kutaka mabadiliko, ushauri wangu bora kuziba ufa kuliko kujenga ukuta.

No comments: