Saturday 13 December 2014

kampeni zanoga serikali za Mitaa na upigaji kura unaendelea ukiwa na Kasoro nyingi CCM yacheza rafu kuogopa tsunami ya Ukawa



UCHAGUZI WA SERIKALI YA MTAA WA MIGOMBANI WAINGIA KWIKWI MARA BAADA YA AFISA MTENDAJI WA KATA YA SEGEREA KUJA KUTANGAZA KUSITISHA UCHAGUZI

Wakazi wa Mtaa wa Migombani, Uliopo Katika kata ya Segerea Manispaa ya Ilala Jijini Dar Es Salaam wakiwa wamelizunguka gari la Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea aliyefika majira ya saa tisa kamili mchana huu na kutangaza kusitisha uchaguzi wa serikali ya mitaa kimya kimya.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea (katikati mwenye shati la draft) akiwa kawekwa mtu-kati mara baada ya kuja na kutaka kusitisha uchaguzi bila sababu ya msingi. Waliomzunguka ni wakazi wa mtaa wa segerea wakimuhoji afisa mtendaji huyo sababu ya kutaka kusitisha uchaguzi huo wakati hakukuwa na vurugu wala kero ya aina yoyote iliyojitokeza katika kituo cha kupigia kura cha Migombani.Wakazi wa Mtaa wa migombani wakumzuia afisa mtendaji kuondoka hadi pale atakapotangaza tena kuwa uchaguzi unaendelea

Msimamizi wa Uchaguzi wa serikali ya Mtaa wa Migombani katika Kituo cha uchaguzi wa Migomabni akielezea sababu za kusimamisha uchaguzi huo kwa muda kutokana na kusubiria barua ya kumtaka kuendelea na uchaguzi kutoka kwa afisa mtendaji wa Kata ya Segerea aliyetaka kujaribu kusitisha Uchaguzi huo kwa kisingizio cha Kutumwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea, Akiandika barua ya kutamka kuwa uchaguzi unaendelea mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kutaka afisa huyo kueleza sababu za msingi za kutaka kujaribu kusitisha uchaguzi huo.Pembeni ni wakazi wa Mtaa wa Migombani wakishuhudia kuwa afisa mtendaji huyo anaandika ipasavyo hiyo barua.

Hii ndio barua aliyokuwa akiandika afisa mtendaji wa kata ya segerea inavyosomeka ambapo baadae alienda nayo ofisi kwa kuongozana na wakazi wa migombani kwaajili ya kugonga muhuri wa kata kuthibitisha kuwa uchaguzi unaendelea

Afisa mtendaji wa Kata ya Segerea (Mwenye shati la drafti) akiongea na wakazi wa mtaa wa migombani mara baada ya vurugu kutaka kutokea mara baada ya afisa mtendaji wa kata ya segerea kujaribu kusitisha uchaguzi bila sababu za msingi

Wakazi wa Mtaa wa migombani, Kata ya Segerea wakimzuia Afisa mtendaji huyo kuondoka mpaka atangaze tena kuwa uchaguzi unaendelea.



Hali ya Kushtusha imetokea katika uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Migombani Mara baada ya Afisa Mtendaji huyo kuja na kutangaza kimyakimya Kuwa UChaguzi huo umesitishwa, Mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kusikia ndipo walipoanza sasa kutafuta mchawi na kumtia nguvuni afisa mtendaji huyo wa mtaa kwa kutaka kujua sababu za msingi zinazopelekea yeye kuja kutangaza kusitisha uchaguzi huo.
Afisa mtendaji huyo baada ya kuulizwa sababu za msingi alijitetea kuwa ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya ilala. Mara baada ya Kutoa sababu hiyo ndipo wakazi wa mtaa wa migombani walipoona kuna dalili za kuchakachuliwa kwa kura zao ndipo walipomuweka mtu kati na kumtaka Afisa mtendaji huyo kutangaza kwa maandishi kuwa uchaguzi unaendelea ndipo wakazi hao walipomuweka mtu kati na kuhakikisha anaandika barua hiyo ya kutaka kuendelea na uchaguzi.
Mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kwenda nae katika ofisi ya kata kwaajili ya kugonga muhuri kuthibitisha Uchaguzi huo kuendelea ndipo uchaguzi ukaendelea na muda huu zoezi la kuhesabu kura linaendelea


Msimamizi wa Upigaji Kura Faudhia Mbawala akihakiki majina ya washiriki wa wapiga kura katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Hekima Buguruni, wanaongalia kutoka kushoto ni Abasi Mzee wakala wa Chama cha Mapinduzi, Omary Issa Wakala wa CUF na Abubakari Said Wakala wa ADC, leo jijini Dar es Salaam.

Msimamizi wa Upigaji Kura Faudhia Mbawala akihakiki majina ya washiriki wa wapiga kura katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Hekima Buguruni, wanaongalia kutoka kushoto ni Abasi Mzee wakala wa Chama cha Mapinduzi, Omary Issa Wakala wa CUF na Abubakari Said Wakala wa ADC,leo jijini Dar es Salaam.

Mkaazi wa Buguruni, Wilaya ya Ilala akipiga kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Hekima, leo jijini Dar es Salaam


Wakazi wa Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala wakiwa katika foleni ya kuhakiki majina yao kwa ajili ya lupiga kura na kuweza kuwachaguwa viongozi wao wa Serikali za Mitaa katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Kimanga, leo jijini Dar es Salaam (Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)

Wakazi wa Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala wakiwa katika foleni ya kuhakiki majina yao kwa ajili ya lupiga kura na kuweza kuwachaguwa viongozi wao wa Serikali za Mitaa katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Kimanga, leo jijini Dar es Salaam

Wakazi wa Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala wakiwa katika foleni ya kuhakiki majina yao kwa ajili ya lupiga kura na kuweza kuwachaguwa viongozi wao wa Serikali za Mitaa katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Kimanga, leo jijini Dar es Salaam

Wakazi Buguruni, Wilaya ya Ilala wakiwa katika foleni kwa ajili ya kupiga kura na kuweza kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Hekima, leo jijini Dar es Salaam

Mkaazi wa Kariakoo Mashariki, Kata ya Kariakoo akishiriki katika upigaji kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Lumumba katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam

Mkazi wa Buguruni Wilaya ya Ilala akishiriki zoezi la kupiga kura katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Hekima, kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam

Wakazi wa Kariakoo Mashariki, Kata ya Kariakoo wakiwa katika foleni kwenye kituo cha Shule ya Msingi Lumumba kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam

Mkazi wa karikoo Mashariki Kata ya Kariakoo Bw. Fumbuka Ditopile akipiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Lumumba ,kwa ajili ya kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa Mitaa akiwemo Mwenyekiti na Wajumbe leo jijini Dar es Salaam.

Mkazi wa karikoo Mashariki Kata ya Kariakoo akipiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Lumumba

Msimamizi wa upigaji kura, Mwalimu Lucy Buzuka akitoa maelekezo kwa wapiga kura wa Kariakoo Mashariki, Kata ya Kariakoo jinsi ya kupiga kura katika zoezi la kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa ambapo siku ya leo jijini Dar es Salaam.

Msimamizi wa upigaji kura, Mwalimu Lucy Buzuka akitoa maelekezo kwa wapiga kura wa Kariakoo Mashariki, Kata ya Kariakoo jinsi ya kupiga kura katika zoezi la kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa ambapo siku ya leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo

No comments: