Friday, 7 March 2014

VIFO VYA UTATA NDANI YA CCM !

UKWELI WA KIFO CHA MGIMWA, KIGHOMA MALIMA, HORACE KOLIMBA, STEVEN KIBONA NA GILMAN RUTIHINDA, WALIVYOMALIZWA NA   WENGINE  WATOTO WAO WALIVYONYAMAZISHWA KWA KUPEWA VYEO !The late Dr. Omar Ali Juma The Vice President of the United Republic of TANZANIA was born on 26 June 1941 in Chake Chake, Pemba- Zanzibar.He served as Vice President of Tanzania from 1995 to 2001.
Attended primary school education between 1949 and 1957 at Chake Chake Boys' School. From 1957 to 1960 he was at Euan Smith Secondary School (now Haile Selassie Secondary School) where he attained an Ordinary Level School Certificate. In 1960 he joined the Moscow State University and was awarded with an Advanced Level Certificate in 1962 and seven years later, at the same college, he attained a Bachelor's degree in Veterinary Medicine and Surgery. For a year from 1969 he was at Cairo University for a post graduate certificate in Animal Production and Health. In 1976 he attended a one year course for a Post Graduate Diploma in Tropical Veterinary Medicine at Edinburgh University. In 1982 he joined the University of Florida in the USA for a short course in Veterinary Science and two years later he was at Reading University, UK, for a Livestock Economics course from which he joined the Kivukoni Ideological College (Tanzania).

1995 – 
Mgimwa
Profesa Kighoma Malima
Gilman Rutihinda

Ndugu zangu,
Watanzania wanamkumbuka aliyekuwa Waziri wa Fedha (Mweka Hazina Mkuu wa Serikali) marehemu William Mgimwa, maziko ambayo yalifanyika kijijini kwao Magunga, mkoani Iringa.Kumekuwepo na tetesi nyingi kupitia vyombo vya habari kwamba huenda waziri huyo mkimya amelishwa sumu. Hakuna aliyethibitisha madai haya tangu kutokea kifo hicho Januari Mosi 2014.Kifo cha Mgimwa kimeingia kwenye mlolongo wa vifo kadhaa vyenye utata vilivyowahi kutokea nchini katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Mawaziri wawili waliopata kuongoza Wizara ya Fedha nao wanadaiwa kufa katika mazingira ya kutatanisha, miongoni mwao akiwa Profesa Kighoma Ally Malima aliyekufa Julai 16, 1995.Alipojiengua CCM na kuhamia NAREA (NRA), Prof Kighoma alikwenda Makka katika hijja ya UMRA. Kabla ya kwenda kwake huko aliahidi pindi atakaporudi Tanzania atakuja kutoa yaliyopo moyoni mwake. Baada ya kumaliza hijja alielekea Uingereza na mauti yakamkuta huko. Ilienea katika kila kona ya Tanzania kuwa inawezekana kuna FITNA iliyosababisha kifo chake japokuwa wengine wanasema hakuna FITNA yoyote. 

Steven Kibona, aliyepata kuwa Waziri wa Fedha enzi za Alhaj Ali Hassan Mwinyi, pamoja na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Gilman Rutihinda, nao walikufa vifo vya utata.
Kuna taarifa zilizodai kwamba, wazalendo hao walikataa kuchapisha fedha na kuziingiza kwenye mfumo kwa kutambua kwamba kufanya hivyo kungeongeza mfumuko wa bei na ugumu wa maisha ungeongezeka.Kibona alipelekwa na aliporejea huko akaanza kuumwa. Ikaelezwa kwamba amekula vyakula vya Kihindi ndiyo maana alikumbwa na tumbo la kuhara kwa sababu ya ugeni wa chakula. Hakukaa muda mrefu akafariki dunia.
Rutihinda naye alipata ajali asubuhi tu akiwa anatoka nyumbani kwake. Taarifa zilizokuwepo ni kwamba ilikuwa ajali ya kawaida! Mwingine ambaye kifo chake kina utata ni Horace Kolimba. Huyu anajulikana kwa kauli yake aliyoitoa kwamba CCM haikuwa na dira wala mwelekeo. Akaitwa Dodoma 'kuhojiwa'. Lakini Machi 15, 1997 majira ya saa 11 jioni wakati akijiandaa kutoa maelezo yake, akadondoka ghafla. Walipompeleka hospitali ya Mkoa wa Dodoma tayari alikuwa 'wa jana'. Hivi, hakuna anayeweza kutoa taarifa rasmi kuhusiana na vifo hivi vyenye utata au kifo cha kiongozi yeyote kinapotokea mpaka tusubiri 'redio mbao'?
Nawasilisha.

No comments: