Wednesday 31 December 2014

UKAWA WAITEKA MTWARA l

Mji wa Mtwara wazizima kwa ujio wa viongozi wa Ukawa wakiongozwa na Prof Lipumba wa CUF. Maandamano makubwa ambayo hayajawahi kutokea yakiongozwa na waendesha magari, bodaboda, bajaji pamoja na watembea kwa miguu. Pamoja na hali ya mvua na manyunyu yaliyopo, hamasa ya watu iko pale pale. Wakiimba "oooh! oooh! chaama, chama cha wananchi CUF" Ujio wa UKAWA kulingana na baadhi ya wabashiri wa kisiasa unatokana na kasi ya mabadiliko katika mkoa wa Mtwara, hali ya kisiasa hususan kashfa iliyotikisa nchi ya Escrow, wananchi  kupoteza imani na chama tawala, hali ya umaskini , rushwa pamoja na ukosefu wa huduma mbalimbali za kijamii hususan ajira, elimu, huduma za afya , umeme pamoja na maji. Kubwa na ambayo ni kidonda kwa wana Mtwara ni sintofahamu ya ujenzi wa bomba la gesi. Mkutano unatarajiwa kuanza saa tisa alasiri katika viwanja vya mashujaa. Hii ndio itakuwa funga mwaka kwa mkoa wa Mtwara ambapo wananchi wana kiu ya kumsikiliza mheshimiwa Lipumba na viongozi walioambatana naye wa UKAWA. Wananchi wa Mtwara wameghairi na wanataka mabadiliko ya kweli. Sio mabadiliko ya majengo na mabarabara wanataka mabadiliko ambayo yatabadilisha maisha yao miaka mingi ya baadae na msingi wa mabadiliko hayo ni elimu, huduma bora za jamii, kuondoa rushwa na upendeleo serikalini na utoaji wa haki ulio sawa pamoja na mgawanyo stahiki wa rasilimali zilizopo.

No comments: