Friday 9 January 2015

majibu ya Dk Kigwangalla kwa Salim KHATRI kuhusu 'offshore companies' na IPTL

majibu ya Dk Kigwangalla kwa Salim KHATRI  kuhusu 'offshore companies' na IPTL


Ndugu Salim,

You present yourself, to me, as a well learned person, I salute you; japokuwa unachokosa ni impartiality kwenye suala hili. Hebu jivue baibui la upendeleo wa dhahiri kwa watu walio-scheme, bila shaka kabisa, kuendesha mchakato wenye kutia 'mashaka', kwa mtu yeyote yule huru, bila kujiwekea hata wingu dogo tu la mashaka na kujiridhisha beyond reasonable doubt! Ukiweza kufanya hivyo utauona ukweli.

kwa kuwa wewe ni mwanazuoni, nitakukumbusha principle hii, kwamba wanazuoni hupenda ku-present ukweli bila upendeleo wala uonevu. Soma 'phenomenological reduction'.

Ripoti ya PAC, siyo Qur'an, kwamba ni kazi ya manani isiyo na makosa, la hasha; lakini kwa hakika imefanywa kwa ustadi, umakini na uzalendo wa hali ya juu. Mimi sikukubali kuingia kwenye kamati ya PAC ili kumshughulikia mtu. Niliingia na nilitoka nikiwa na dhamira safi. Na sikutumwa na mtu, na kwa hakika sikumtetea ama kumuonea mtu, niko safi kwa hapa duniani na kesho kwa ALLAH. Na kama ningebaini kuna mbinu chafu za kumkandamiza mtu kwa sababu za binafsi ama mambo yasiyohusika na uchunguzi, nakuhakikishia ninge-object, na kama nisingeeleweka, ningejitoa, na dunia nzima ingejua. I am that principled, kama hukuwahi kunifahamu. Huwa sishiriki mambo ya hovyo hovyo.

Kukujibu maswali yako sasa, baada ya bashraf hiyo:

1. Kaka, najua sana haya mambo ya offshore companies, I have friends wanaocheza mchezo huo kwenye nchi zao na nchi mbalimbali za Africa, I know why they do that. Wanafanya hivyo kwa sana ili kukwepa kodi...mfano kwa Tanzania, toka tufanye mabadiliko ya Sheria ya Income tax ule mwaka 2012, kuna kodi kubwa ya Capital gains tax (wageni ni 20%, wazawa ni 10%) huwa wanaikwepa kwa kusajili makampuni na kufanya mauzo kwenye nchi zisizo na kodi hiyo, mfano kule BVI, Seychelles na jurisdictions nyingine zisizo na kodi hiyo. Huo ni mfano mmoja tu.

Sababu ya pili wafanyabiashara wanafungua offshore companies ni hii iliyojificha, ambayo ndiyo inayoweza kuwa yenye kuhusika kwenye deal ya Mechmar-PLI-PAP, nayo ni kuficha 'true identity' ya 'wamiliki halisi' wa hisa za kampuni husika. Wanafichaje? Kwa kutumia 'power of attorneys' na firms za attorneys/finance & investments kuwawakilisha. Sababu ya tatu, ambayo nayo imejificha, na huwa haiandikwi wala kufundishwa kwenye business schools...ni kufanyia uhalifu wa kibiashara, kifedha ama wa kitapeli kisha kutakatisha! Kwa mfano: PLI inasajiliwa kimazabe mazabe huko offshore - inanunua hisa ambazo hazipo, wamiliki wake wanakuwa hawajulikani, inapata mkataba, haina share certificates, inakuja Tz inaziuza hisa hizo kwa mikataba tu bila hata kuwa na share certificates, ina-declare bei ya chini sana (ambayo haipo) inalipa kodi kama za kiosk, inakamilisha mchakato wote mchafu na wa kihuni, kisha inaiuzia PAP ambayo inakuwa ni kampuni mpya, genuine, local na inaweka rekodi zote sawa - inakuwa compliant and clean kabisa!

2. Usiponunua tu hisa za kampuni kihalali, basi mchakato mzima wa mauzo na miamala utakayofanya vinakufa kifo cha kawaida... mchakato wa manunuzi ya hisa za Mechmar na za VIP haukuwa halali kwa mujibu wa sheria za nchi na hivyo transaction yote inakuwa void.

3. Pamoja na barua na taarifa mbalimbali za Ndg. Ngwilimi, kuna namna ya ku-collate taarifa tulitumia katika uchunguzi, hivyo usidhani unajua kila kitu. Kuna mengine mengi tu hatukuyatumia kuandika tarifa, kuna mengine hayakuwa na uzito wa kuyaleta kwenye public domain, tumeyatunza. Kuna mengine yangeudhi watu, yangechafua uwanja wa siasa na jamii yetu, tumeyafukia. Siwezi kusema zaidi ya hapa. I am sorry.

4. Kila kazi ina utaratibu wake. Sijui wewe unafanya kazi gani. Hata mimi nilipoingia kwenye siasa na utaalamu wa sayansi na biashara, nilizidisha kiwango cha kuwa muwazi na mkweli, kama ilivyo culture ya taaluma niliyojifunza na kufanyia kazi kwa muda kidogo, nikapata shida sana mwanzoni, kama alivyopata Mzee Prof. Muhongo, nikaamua kunyamaza mwaka mzima, nikajifunza kuchagua maneno na kuweka akiba ya maneno. Sasa ninaishi vizuri na wenzangu kwenye siasa na uongozi.

5. Wakati Jaji Utamwa anafanya uamuzi wake pengine hakukuwa na hizi taarifa zilizopo leo, na ndiyo maana hukumu huwa zinapitiwa upya, zinakatiwa rufaa, zinapingwa mahakamani. Na hivi tunavyoongea, sina shaka una taarifa ya uwepo wa kesi kadhaa mahakamani zinazopinga ama kudai mambo mbalimbali yanayohusiana na jambo hili. Unajua ni zaidi ya 10? Hivi jambo clean na straightforward, lililomfanya PS-MEM na wenzake kwenye mlolongo huo walikimbize na hata kufikia ku-release pesa nyingi kiasi hicho ndani ya siku saba (efficiency?) tu lingeweza kuzua utata wote huu? Na je, waziri mwenye dhamana ya EM naye hakujulishwa kweli? Kuna mawili tu hapo, kwamba aidha ni conspiracy theory yao, ama ni wazembe na ma-bogus kupindukia, la mwanzo lina uwezekano mkubwa zaidi, maana la pili waliishaturidhisha watanzania, kwa kazi yao nzuri, beyond doubt, kwamba wao ni watu makini, wachapakazi na wenye weledi mkubwa tu.

6. Si ajabu kwa HSS kama 'anayedaiwa kununua IPTL' na sasa kuwa mwenyekiti wa IPTL na mwenyekiti wa PAP kuamua malipo ya fedha nyingi kama zile kulipwa kwenye kampuni mpya namna ile, kwenye macho ya mtu mwenye uelekeo na mtazamo wa aina yako. Lakini kwa wengine, ambao hatujalalia popote, tunashangaa sana. Kwa sababu, IPTL ina liabilities zake, ina kodi za kulipa...inadaiwa na serikali, inadaiwa na TANESCO, sasa tuache hayo mengine yote lakini tubaki na jambo moja tu kubwa na la msingi, kwamba kwenye serikali huwa kuna ka-principle kamoja very simple kwamba, kodi ni first charge...kwamba, kwenye kila malipo yanayofanywa na serikali basi afisa wetu tunamtarajia atutazamie kama kuna kodi yetu hapo...sasa sisi tulifanyaje? Lingine ni kwamba, mkataba wa escrow unatoa maelekezo mahsusi ya namna ya ku-deliver funds zilizomo kwenye escrow a/c, je, mkataba huo unasema pesa hizo alipwe nani? Huoni kwa nini Governor wa BOT alikataa mara kadhaa kukubali malipo hayo yafanyike?

Unaongelea eti kulikuwa na mkataba wa ku-deliver hizo pesa, unajua kikao cha makatibu wakuu na wataalamu walipokaa walisema nini kuhusu kuzi-deliver hizi funds? Walikubali? Wao walitia mashaka. Je, ni nini kilitokea baada ya wao kusema wanadhani suala hili bado sana kwa sasa, lakini cha kushangaza kamati hii ya wataalamu ilirukwa, ni kwa nini?

Sintoweza kukubadilisha mtazamo wako, lakini ukweli unaujua.

Wassalaam,
HK.

No comments: