Leo nitawakumbusha siku nilipokutana na RAIS SAMIA mwaka 2023 na mazungumzo yetu juu ya nia yake ya kuleta MAGEUZI Tanzania niliondoka pale nikiamini Tanzania mpya inaletwa na mama Mzanzibari na hata agenda kuu ya Uraia pacha ya watu wa diaspora ipo salama kwa wakati muafaka ukifika baada ya uchaguzi wa 2025 kumalizika. Masuali yangu ya kwa Nini ulimueka FREEMAN MBOWE ndani
na kutokubaliana nae na njia yake ya utawala wake wa kuwaeka wapinzani wake Ndani nilimuambia hapa ulikosa busara za hali ya juu na yeye alinieleza tafrani zake alizokumbana nazo Ndani ya CCM ya upinzani wa watu wanaompinga na wengi waliokuwa wafuasi wa bosi wake RAIS Magufuli na baadae kina Mbowe kumuongezea tafrani za kudai katiba mpya alihitaji kufocus kupanga serikali yake ya watu walio watiifu kwake
Rais Samia alitamani sana kuona Tanzania yenye muelekeo wa serikali ya mseto baada ya uchaguzi wa 2025 kuona hatuoneshani vidole bali wanaionyooshea vidole Taifa la Tanzania na sisi kama Watanzania tunawanyooshea mabeberu vidole kama Watanzania bila kujali tofauti ya vyana vyetu.
Kwa Nini ndoto ya Rais Samia imetekwa NYARA?
Wakati Rais Amani Karume anafanya mazungumzo ya Siri na RAIS wa MOYO WA WAZANZIBARI Maalim SEIF Sheriff HAMAD alipambana na vikwazo vikubwa ndani ya chama chake cha CCM na kuitwa msaliti hadi mitandaoni na mabalozi wetu nje wenye asili ya Zanzibar nikuwa RAIS KARUME anataka kuiuza CCM Zanizbar kwa chama cha CUF Na huko CUF kwa hasira nyingi za makovu ya CCM ya huko nyuma ya Komandooo ya muafaka wa ulioanzishwa na katibu wa jumuia ya madola EMEKA ANYAOKU . Licha ya DR SALMIN AMOUR alieusaliti muafaka no 1.Maalim SEIF na RAIS KARUME walianzisha muafaka no 2 kutengeneza maslahi ya Utulivu wa Zanzibar sio maslahi ya CCM na CUF , lakini Maalim SEIF na yeye alikumbana na mabomu ya wahafidhina wa CUF kuwa anajipendekeza kwa RAIS KARUME hakuwa salama kwa kushambuliwa kuwa anapigania mafao yake kustaafu ya uwaziri kiongozi yaliokatwa na kunyimwa mafao yake toka alipofukuzwa CCM .Maalim na timu yake ya watu watano walipambana kuhakikisha hakuna kidudu mtu anafanikiwa mara hii kuyakoroga mazungumzo yale .
Baadae wote wawili Maalim SEIF na 'Rais Karume walijua wapo vitani kuwa ndani ya vyama vyao kuna camp za wahafidhina zinazopinga mazungumzo yale kutokana na kambi ya CCM kuhofia kundi fulani maslahi yao kuguswa ikiwa CUF wataingia serkalini na ndani ya CUF makovu ya watu kupigwa risasi kuuliwa mwaka 2001 hadi Tanzania kuzalisha wakimbizi Mombasa Kenya kitendo ambacho Rais Mkapa aliandika kwenye kitabu chake ndio doa la utawala wake Tanzania kuzalisha wakimbizi nje ya NCHI
wakati Tanzania ilikuwa ni NCHI ya kupokea wakimbizi wa nje . Maalim na Rais Karume waliafanikiwa mazungumzo yao kwa Kila upande kulegeza kamba na kufikia mauafaka uliiopelekea kuanzishwa Sheria ya kura ya maoni iliowakilishwa kwenye baraza la wawakilishi la Zanzibar
Wazo letu la wengi la wanadiaspora wengine waliotumia mlango wa nyuma wa diplomasia la kutaka KINA LISSU na LEMA na Kampeni aya Mheshimiwa Mbowe kuachwa na wlaiopo nje warudi nyumbani kuondoa doa la kuwa Tanzania ina wakimbizi wa kisiasa nje ya NCHI alilichukua kwa mikono miwili hata haikufika miezi miwili mama wa KIZANZIBARI nilimuona yupo ubelgiji anakutana na TUNDU LISSU hapo niliamini kabisa kwenye moyo wangu kua SAMIA sasa hatanii bali anataka kuleta mshikamano wa taifa letu kwa nadharia ya Maalim SEIF na kuyaponya yale makovu ya walioumizwa na makovu ya CCM ya tawala zilizopita na makovu ya chaguzi zilizoacha misiba na simanzi nyingi hasa kwa ndugu zake kule Zanzibar roho za watu 29 zilipotea na mamia ya Wazanzibari wenzake kuachwa na ulemavu.
Nafikiri Wapinzani wa CHADEMA waliasahau kuwa wahafidhina wanaompinga mageuzi ndani ya CCM bado wapo .Mfano wa Kitendo kile kiliniacha na huzuni kubwa baada ya Kumsikia Makamo wa pili wa RAIS wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed alipendekezwa na Magufuli kuwa Makamo wa RAIS kukanusha kuwa hakuna watu waliouliwa Zanzibar au kupigwa risasi yeye hana taarifa hizo na Kila waliojaribu kumkaribia Rais Mwinyi kuwasaidia mayatima waliouliwa ndugu zao alijieka mbali kwenye kuwakaribia au kuwatembelea kuwafariji kwa misiba waliopata familia hizi 29 waliouliwa ndugu zao na hata majeruhi kama viongozi wa CUF na Waziri wa Afya wa ACT sasa alietekwa na kupigwa na kuumizwa pamoja na mjumbe wa tume ya uchaguzi wa CUF ndugu Ayoub Bakari ambae sasa hiviamerudfi tena kwenye tume ya uchaguzi wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment