Tuesday, 6 January 2015

Tume ya Uchaguzi kutumia 293bn/- uchaguzi mkuu wa mwaka huu

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetenga kiasi cha shilingi bilioni 293 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa, uandikishwaji  wapiga kura pamoja na upigaji kura nchi nzima.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji  mstaafu, Damian Lubuva,  wakati akitoa tathmini ya utekelezaji wa zoezi la majaribio la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa mpya wa Biometric Voters Registration (BVR).

Alisema zoezi  hilo la majaribio limekamika katika kata za Bunju na Mbweni katika jimbo la Kawe, manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kata za Ifakara,Kakingiuka,Ipangala na viwanja  sitini katika jimbo la Kilombero,mkoani Morogoro,pamoja na kata za Ikuba,Usevya na Kibaoni jimbo la Katavi halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Alisema jumla ya BVR kits 250 zilitumika katika uboreshaji huo kwa mgao wa halmashauri ya Kilombero BVR kits 80,halmashauri ya wilaya ya Mlele BVR kits 80,pamoja na halmashauri ya Kinondoni BVR kits 90,ambapo vituo vyote vilifunguliwa kuanzia saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa 12.00 jioni.

Alisema koa wa Dar es Salaam, kata za Bunju wapiga kura 15,123 waliandikishwa kati ya 27,148 kata ya Mbweni wapiga kura 6,200 waliandikishwa kati ya 8,278 ambapo takwimu hizo zilikisiwa mapema kutokana na matokeo ya sensa mwaka 2012.
Aidha alisema mkoa wa Morogoro kata za Ifakara,Kakingiuka,Ipangala ,Mlabani na Viwanja sitini  wapiga kura walioandikishwa ni 19,188 ambapo ilikadiriwa kuandikishwa wapiga kura 17,790  na mkoa wa Katavi halmashauri ya Mlele kata za Ikuba,Usevyana Kibaoni wapiga kura 11,210 waliandikishwa wakati makadirio yalikuwa watu 11,394.

Pia alisema matokeo hayo yanaridhisha kuwa vifaa vya uandikishaji vilifanya kazi vizuri na hivyo vinaweza kutumika katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa nchi nzima. Hata hivyo, alisema licha ya  mafanikio kuna baadhi ya changamoto zilijitokeza katika zozezi hilo,ambapo zilitumika camera za  laptop badala ya kutumia camera iliyowekwa kwa ajili ya kupiga picha pamoja na uchukuaji wa alama za vidole ilisababisha mfumo  kusimama. 
Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni uandikishwaji na matatizo ya watendaji wa zoezi hilo, BVR kits kuchelewa kufikishwa katika vituo pamoja na vurugu wakati wa uandikishwaji.

No comments: