Na Julius Mtatiro.
Jimbo la Mbarali
Jimbo la Mbarali kama yalivyo mengine lilianza siasa za vyama vingi mwaka 1995 kwa ushawishi wa kipekee kutoka kwa vyama mbalimbali, huku NCCR Mageuzi ikionyesha kila aina ya makeke.CCM haikuwa na hofu na ilimtumia kiongozi mzoefu wa kijeshi, Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa ambaye hakufanya ajizi, aliwashinda wapinzani na kutunza heshima ya CCM hapa Mbarali. Kanali Mjengwa aliongoza kipindi kimoja, 1995 -2000.Mwaka 2000 katika Uchaguzi Mkuu, CCM ilibadilisha ladha na kumleta mwanamama. Huyu ni mtaalamu wa masuala ya uhasibu, Estherina Kilasi.
Jimbo la Mbarali
Jimbo la Mbarali kama yalivyo mengine lilianza siasa za vyama vingi mwaka 1995 kwa ushawishi wa kipekee kutoka kwa vyama mbalimbali, huku NCCR Mageuzi ikionyesha kila aina ya makeke.CCM haikuwa na hofu na ilimtumia kiongozi mzoefu wa kijeshi, Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa ambaye hakufanya ajizi, aliwashinda wapinzani na kutunza heshima ya CCM hapa Mbarali. Kanali Mjengwa aliongoza kipindi kimoja, 1995 -2000.Mwaka 2000 katika Uchaguzi Mkuu, CCM ilibadilisha ladha na kumleta mwanamama. Huyu ni mtaalamu wa masuala ya uhasibu, Estherina Kilasi.
Estherina alivaa viatu vya kanali mstaafu kwenye kampeni na ni kama alijengewa ujasiri wa kijeshi, hakuwaogopa wanaume na akasaidiwa na mtandao wa CCM ambao kipindi cha nyuma ulikuwa na maana ya ushindi.Alitangazwa mshindi na akafanikiwa kuongoza Jimbo la Mbarali kwa kipindi cha kwanza mwaka 2000 – 2005.Mwaka 2005 unakumbukwa kwa kimbunga cha Kikwete pamoja na matokeo yenye utata kwa maana ya upigaji kura uliokuwa umepitiliza, (siku za mbele katika uchambuzi wa masuala ya siasa tutakuja kuongelea masuala ya kushuka na kupanda kwa upigaji kura ambako kunatia shaka).Wapigakura walijitokeza kwelikweli na kazi kubwa ikafanywa na wagombea huku CCM wakimpa nafasi mwanamama Estherina ambaye alikuwa ameongoza kipindi kimoja.
Vyama vya CUF na TLP vilikuwa na nguvu jimboni humu na kufanikiwa kuweka wagombea, ule utitiri wa vyama wa mwaka 1995 ulipotea.Filimbi ya upigaji kura ilipopulizwa na matokeo kutangazwa, mwanamama Estherina aliwabwaga wagombea wa TLP na CUF. Estherina alipata kura 52,713 akifuatiwa na Pwilla Getrudi Jacob wa TLP kura 10,168 na Kharid Shaweji wa CUF kura 6,912.Kwa jumla vyama vya upinzani vilijitahidi lakini viliangushwa na dhana ya ushindi wa kimbunga wa CCM katika kila kona ya nchi. Bi Estherina akawa na ridhaa mkononi na akawa mtumishi wa wananchi hadi mwaka 2010.Mwaka 2010 ulifika huku vyama vikiwa vimejiimarisha na CCM ikiendelea kutumia juhudi za mtandao wake.ananchi wa Mbarali hawakuwa na kumbukumbu nzuri sana na mbunge aliyemaliza muda wake, kwa sababu hakufanya vizuri katika kipindi cha miaka 10 na Chadema iliitumia nafasi hiyo kujipanga.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliporuhusu vyama kujitosa kwenye uchaguzi vilipatikana vyama vitano.Kampeni zilionyesha dalili ya ushindani wa wazi kati ya Chadema na CCM ambapo vyama hivi viwili vilileta wagombea wapya, huku TLP ikimleta mgombea yuleyule aliyesimama mwaka 2005.Mgombea mpya wa CCM Modestus Kilufi alipata kura 34,869 na alifukuzwa bila mafanikio na Jidawaya Kazamoyo wa Chadema kura 16,090.Wagombea wengine watatu akiwemo wa TLP waliambulia asilimia moja ya kura zote.
Kama yalivyokuwa maeneo mengi ya nchi, siasa za Mbarali zilitawaliwa na Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na jambo hilo lilikuwa na maana kubwa wakati nchi inaelekea katika uchaguzi wa mwaka huu.Hata hivyo, safari ya kiushindani jimboni Mbarali haiwezi kupita bila kupimwa kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, japokuwa watu wengi huhoji kigezo hiki kutokuwa na maana pale ambapo tathmini za ubunge zinafanyika.Kigezo hiki kina maana kubwa mahali ambapo vyama vinachomoza na vinaweza kufanya lolote.
Uchaguzi huu unasaidia kujenga mtandao wa ushindi wa chama kwenye uchaguzi mkubwa na wakati mwingine unaweza usisaidie ikiwa chama chenye mtandao huo kitaweka mgombea asiye na sifa.Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwezi Desemba mwaka jana uliipatia Chadema vijiji 18 kati ya 102 na vitongoji 121 kati 713.
Matokeo haya siyo kipimo kizuri kwa Chadema kuelekea uchaguzi wa mwaka huu na kuipatia Ukawa ushindi, lakini ikumbukwe kuwa Chadema iliweza kupata asilimia 30 ya kura za ubunge mwaka 2010 kwenye jimbo hili bila kuwa na hata asilimia 2 ya vijiji na vitongoji.Hali hiyo ina maana kuwa mipango ya Chadema kulitwaa Jimbo la Mbarali ikiwa itaweka mgombea anayekubalika itakuwa kwenye njia sahihi na haitakwazwa na matokeo haya ya serikali za mitaa. Lakini ikiweka mgombea dhaifu, CCM watafanya sherehe
.Jimbo la Mbozi Magharibi
Mwaka 1995 Mbozi Magharibi ilianza safari ya siasa za vyama vingi kwa cheche za hali ya juu. NCCR Mageuzi ilitisha na kujipanga kimtandao lakini haikufua dafu kwa CCM.CCM ikiwakilishwa na Eliachim Simpasa ilifanya vyema na mwakilishi huyo akawa mbunge wa kwanza wa jimbo hili chini ya mfumo mpya wa ushindani wa vyama.Mwaka 2000 wakati NCCR Mageuzi inasambaratika vyama vingine vikianza kuchomoza zaidi, CCM haikusita kumrejesha Simpasa ambaye kitaaluma ni mwalimu mwenye shahada ya elimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Enzi za Simpassa zilikoma baada ya kipindi hiki cha pili cha uongozi na mwaka 2005 kulikuwa na habari mpya zaidi.Habari inayosemwa kuwa mpya mwaka 2005 ni kuletwa kwa Dk Luka Siyame kuchukua nafasi ya Simpasa ndani ya CCM. Siyame alishindana na Daniel Mwangamba na Victor Sichone kutoka vyama vya CUF na TLP ambapo vyama hivi viwili vilipata jumla ya kura 5,016 vikiiacha CCM na Siyame wakifurahi kwa ushindi wa kura 44,781.Dk Siyame ambaye ni msomi mwenye shahada mbili za uzamili zote zikihusuutabibu alifanikiwa kuongoza Jimbo la Mbozi Magharibi hadi mwaka 2010.Ukuaji wa Chadema jimboni Mbozi Magharibi ulikuwa na hatari kwa ustawi wa CCM.Silinde David kijana machachari aliyekuwa katibu wa kitivo cha biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (sasa Shule ya biashara) alifanya jitihada za kufanya harakati za kiasiasa katika jimbo hili huku akiwa mwanafunzi chuoni.Nakumbuka wakati huo nikiwa waziri wa mikopo na baadaye waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Silinde alinijia mara kwa mara akinijulisha kuwa atakuwa mbunge.
Sikuamini haraka maneno hayo na nilijiuliza atakuwaje mbunge wakati uchaguzi umekaribia na bado sisi tuko chuo! Silinde alionyesha kuwa makini na kauli zake na mara nyingi alikuwa jimboni.Juhudi za kijana huyu wa miaka 26 wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, zilizaa matunda.Wagombea wengine wa vyama vitatu waliambulia asilimia 11 ya kura zote. Zambi akaliongoza Jimbo la Mbozi Mashariki kwa miaka mitano ya kwanza.Mwaka 2010 haukuwa mzuri kwa CCM jimboni hapa. Umaarufu wa chama hicho kikongwe ulishuka, huku mgombea wake akipoteza uungwaji mkono wa vijana.CCM ilimsimamisha tena Zambi ili atumie uzoefu wake na kufuta makosa yake kukinusuru chama chake na huu ni wakati ambapo Chadema ilikuwa juu ikiongozwa na kada kijana, Mtela Mwampamba ambaye wakati huo alikuwa anatokea masomoni.
Mwampamba alikuwa na kila sababu za kuongoza Jimbo la Mbozi Mashariki kwa kushinda uchaguzi wa mwaka 2010, lakini wananchi wengi nilioongea nao (hasa vijana) wanasema kuwa kuna wakati iliwalazimu hata kumchangia pesa za mafuta ya pikipiki na gari ya kukodi.Kwa kweli hakuwa na uwezo wa kiuchumi kukabili ukubwa wa maeneo ya vijijini na inaonekana Chadema haikudhani jimbo hili lilikuwa rahisi, kwa hivyo hakuwa amepata msaada wa kutosha katika kampeni.
Udhaifu huo ulimwangusha. Zambi wa CCM aliponea chupuchupu. Matokeo yalipotangazwa CCM ilisherehekea ushindi wa kura 49,095 dhidi ya kura 31,997 za Mwampamba. CUF ilipata asilimia 1.01 ya kura zote na haikuwa tishio.Kama Chadema wangelijua umuhimu wa jimbo hili na kujipanga kulisukuma kimkakati huku wakimpa Mwampamba nguvu, leo tungekuwa tunaongea mambo mengine.
Mara nyingi vyama vya upinzani huwa na maeneo muhimu sana ya ushindi lakini hupiga hesabu kimakosa na kujikuta maeneo hayo yanaangukia kwa chama tawala hata kama yalikuwa “yameiva” kisiasa na yana wagombea wazuri.
Mwampamba baadaye alishajisalimisha CCM na kuwa kada wa chama hicho kinachoongoza dola.Nadhani alikosa umakini na uvumilivu ambao ungempa ushindi mkubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, kwani ni kijana mzuri na ana uwezo wa kiuongozi.Kuondoka kwake Chadema na kuhamia CCM kwa sababu ya kutofautiana mitazamo na viongozi wake na kutazama kama udhaifu kwa kijana huyu ambaye alipaswa kutambua kuwa maisha ya kisiasa yana kupanda na kuteremka, hivyo alipaswa kuwa mtulivu. Sioni kama atafanikiwa kisiasa ndani ya CCM.Nimeongea na wana CCM watatu jimboni Mbozi Mashariki na wanadai kuwa Godfrey Zambi ana nafasi ndogo ya kurudishwa katika uchaguzi wa mwaka huu na chama chake (katika kura ya maoni).Arudi au asirudi, mtandao wa Chadema umeendelea kukua vizuri jimboni humu na panahitajika kumpata mgombea thabiti.
Maeneo ya kata za mijini katika jimbo la Mbozi Mashariki wanamtambua vizuri Mhandisi Msyette kwamba anaweza kulichukua jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, lakini wanasema maeneo ya vijijini hajajiuza kwa kiwango kikubwa.Ni kazi kwa Chadema kujipanga katika jimbo hili ambalo linahitaji kuongeza asilimia 20 tu ya ushindi na kuongeza mbunge mwingine atakayeongeza changamoto za uwajibikaji na demokrasia katika nchi yetu.Jumamosi ya wiki hii tutakamilisha uchambuzi wa Mkoa wa Mbeya kwa kuangazia majimbo ya Kyela, Rungwe Magharibi na Rungwe Mashariki na kisha kesho yake Jumapili tutahamia Mkoa wa Katavi na kudadavua majimbo yake yote.(Julius Mtatiro ni kiongozi mzoefu katika siasa. Ana shahada ya Uzamili ya Utawala na Uongozi (M.A), na ni mwanafunzi wa fani ya sheria (L LB): +255787536759,
No comments:
Post a Comment