akamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewapongeza wananchi wa Kisiwa Panza kwa mshikamano waliouonesha wakati yalipotekea maafa ya upepo mkali Jumatano iliyopita.Amesema mshikamano huo unadhihirisha jinsi wananchi wanavyoweza kushirikiana katika masuala ya kijamii na kuweka kando tofauti za kisiasa ambazo mara nyingi huwagawa wananchi.Maalim Seif ameeleza hayo baada ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na upepo huo, na kuelezea kufarajika kwake kwa jinsi wananchi walivyoweza kushirikiana katika kukabiliana na maafa hayo.Amesema umoja na mshikamano ndio msingi imara wa kuleta maendeleo katika jamii, na kuwataka wananchi kuendeleza utamaduni huo wa mashirikiano wakati wowote yanapotokea masuala ya kijamii.Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdallah, amesema jumla ya nyumba ishirini na tano (25) na familia mia moja na kumi na nne (114) zimeathirika kutokana na upepo huo uliovuma usiku wa kuamkia tarehe 22/04/2015.
Friday, 24 April 2015
Maalim Seif awapongeza wananchi wa Kisiwapanza kwa mshikamano waliounesha wakati wa maafa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment