Monday 27 July 2015

Wabunge wa zamani warusha kata zao kwenye vyama vyengine


Katibu wa Mipango na Mikakati wa Chama cha ACT-Wazalendo, Habibu Mchange (kushoto), akimkabidhi kadi ya chama hicho, aliyekuwa mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Iringa mjini, Chiku Abwao baada ya kuhamia rasmi ACT-Wazalendo Dar es Salaam leo mchana.


Mbunge Chiku Abwao (kulia), akionesha kadi ya chama cha ACT-Wazalendo baada ya kukabidhiwa.


Mbunge Chiku Abwao (kulia), akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhiwa kadi ya chama cha ACT-Wazalendo.

.

Info Post
7/27/2015 04:33:00 PM
Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Leticia Nyerere akifafanua jambo kwa waandishi habari juu ya kuondoka katika chama hicho.

MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere amengatuka rasmi leo katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam, Leticia amesema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.

Amesema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.
“Moyo wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa CHADEMA na kuacha kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa nasema narudi nyumbani kutumikia”
amesema Leticia.

Leticia amesema kwenda CHADEMA alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge.

Amesema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa shahihi. 


Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Leticia Nyerere akinyanyua mikono ikiwa ni sehemu ya ishara ya kuondoka katika chama hicho na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati alipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es 

Aliyekuwa Mbunge CUF na kuhamia ADC achukua fomu ya Urais  Info Post

7/27/2015 04:54:00 PM


Na Abdi Suleiman na Abdi Shamnnah,PEMBA.

Aliyekuwa mwanachama wa chama cha siasa cha CUF na Mbunge wa jimbo la Wawi kisiwani Pemba, ambaye kwa sasa amehamia chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed, Leo amechukuwa fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia chama chake hicho kipya.

Fomu hiyo alikabidhiwa leo na kamishna wa ADC Kanda ya Pemba, Said Seif huko katika ofisi za chama hicho Wawi kibegi Wilaya ya Chake Chake Pemba.

Akitoa nasaha zake mara baada ya kuchukuwa fomu hiyo, mgombea huyo Hamad Rashid, alisema hatua ya kuchukuwa kwake fomu inalenga kuleta mabadiliko makubwa ya kisiasa Zanzibar.
Alisema kuwepo kwa chama hicho ni kuondosha dhana iliyojengeka miongoni mwa wananchi wa Zanzibar, pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani, kwamba vyama vya CCM na CUF ndio vyama vyenye uhalali wa kuongoza nchi.

Alisema hatua ya wananchi wa Pemba kujitokeza na kumpokea kwa wingi ni thibitisho tosha kwa wananchi kuwa wamejenga imani nayeye na wamekubali mabadiliko ili kuelekeza nchi hiyo katika maendeleo ya kweli.

"Leo ni siku ya historia katika chama cha ADC tokea miaka tatu kuwepo kwao, kimeweza kutoa mabadiliko makubwa kufikia kupatikana mgombe wa urais wa Zanzibar" alisema Hamad Rashid.
Aidha aliwapongeza wananchi na viongozi wa ADC kwa ujasiri wao mkubwa wa kuanzisha chama hicho, huku baadhi ya watu na viongozi wa upinzani wakiona hatua hiyo kwamba ni dhambi.

Aliwataka wananchi kisiwani Pemba kuendeleza imani na chama hicho na kuondokana na dhana kwamba CUF ndio chama pekee chenye uwezo wa kuwapelekea maendeleo, huku akibeza kisiwa hicho kubaki nyuma kimaendeleo.

Mgombea huyo wa ADC anatarajiwa kurudisha fomu hiyo Julai 28 mwaka huu, Kwa katibu mkuu wa chama hicho Unguja, kabla ya kuchukuwa fomu ya Serikali ya kugombea urais wa Zanzibar.
Mapema kamishna wa ADC kanda ya Pemba Said Seif alimshukuru mgombea huyo kwa ujasiri na uamuzi wake wa kujitokeza kuchukuwa fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia ADC.

"Hiki ni kitendo cha kihistoria kwa mlezi wetu kujitokeza kuchukuwa fomu, sisi wananchi na wananchama wa ADC tuko pamoja na yeye"alisema.

Alisema mgombe huyo ni kiongozi shupavu na aliyekomaa kisiasa, huku wananchi wakiwa na matumaini makubwa kutoka kwake katika kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye nafasi ya urais wa Zanzibar.
via ZanziNews blog

No comments: