Saturday 29 August 2015

UKAWA WAZUNDUA KAMPENI ZAO JANGWANI JIJINI DAR

Agust 29, 2015
Kabla ya hapo, jukwaa lililotengenezwa kisasa likisheheni maspika makubwa yakiwemo yaliyowekwa nje ya eneo la mkutano, kwa ajili ya watu wengi zaidi walioshindwa kufika katikati ya viwanja, kulikuwa na burudani zilizooneshwa na wasanii mbalimbali.
Lowassa ambaye pia anapeperusha bendera ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) aliambatana na viongozi wote wakuu wa vyama vinavyounda umoja huo katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wasanii maarufu walioporomosha burudani ni Wanawake Band, Juma Kassimu maarufu Juma Nature na Msaga sumu.
Mbali na burudani za muziki, pia kulikuwa na watu wengi waliokuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa ujumbe mzito kwenda kwa Lowassa huku wakizunguka nayo kila kona.
Yapo yaliyoandikwa “Mzee ukifika Ikulu tuletee Balali ana pesa zetu nyingi” na “Malofa katika ubora wetu.” Mingine ni “Tutawaonyesha ulofa wetu Oktoba 25.”
Mwandishi wa Mwanahalisi liyefika mapema eneo la viwanja ambavyo awali serikali kupitia Manispaa ya Ilala walikataa visitumiwe na UKAWA, alikuta watu wengi wakiwa wamefika, huku simulizi zikisema baadhi ya watu walilala kutoka jana usiku sambamba na kikosi kilichokuwa kikifunga mitambo ya mawasiliano jukwaani.
Barabara zilianza kufurika maeneo ya Magomeni Mapipa hadi Fire njia panda ya Muhimbili, watu wakionekana kukikimbia huku na kule na wakiimba nyimbo za kuhamasishana na zile zilizolenga kukishutumu Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ufisadi na kushindwa kutimiza ahadi ya “maisha bora kwa kila Mtanzania.”
Wimbo uliotia fora katika nyingi zilizoimbwa na wana-UKAWA, ni “Kama sio juhudi zako Kikwete, Lowassa tungempata wapi?” “Sisisi si mnaona? Muziki wa Lowassa kuucheza hamuwezi.”
Katika kufunga mkutano wa uzinduzi wa kampeni, muongozaji wa mkutano, Mkurugenzi wa Bunge wa Chadema, John Mrema, amesema UKAWA wamemaliza mkutano saa 11.55 jioni ili watu wapate kuondoka salama viwanjani, lakini akataka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iwahoji kwa barua CCM waliomaliza mkutano wao wa uzinduzi saa 1 usiku.  Mheshimiwa Mbowe akiwatambulisha wagomeba ubunge wa UKAWA wa Dar

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji wakiwasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Umati wa wakazi wa Jijini Dar es salaam, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye viwanja vya Jangwani kuwalaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama

Sehemu ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali nchini wakiendelea kuchukua habari za Mkutano huo, uliofanyika jioni ya leo kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam na kuhudhulia na maelfu ya Wakazi wa jiji hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akimkabidhi, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, Kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa mwaka 2015/2020 mara baada ya kuizindua, leo Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakionyesha vitabu cha Ilani ya Uchaguzi mara baada ya kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe.
Viongozi wa Vyama mbali mbali vinavyounda UKAWA wakionyesha Ilani hiyo mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam, leo Agosti 29, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kulia) akiwatambulisha baadhi ya Wagombea Ubunge katika Majimbo mbali mbali ya jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akizungumza kwenye Mkutano huo.
Watu wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamembeba mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar aliepoteza fahamu kwa kukosa hewa kutokana na uwingi wa watu uliofurika kwenye viwanja vya Jangwani, Jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akitoa salamu zake kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa akiteta jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji, wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika leo Agosti 29, 2015. 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa akihutubia katika Mkutano huo wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika leo Agosti 29, 2015.

Mmoja wa wanasiasa wakongwe waliotoka CCM, Tambwe Hiza akisalimia.











No comments: