Friday, 18 September 2015

Vipi Mchezo mchafu unaandaliwa, kuvuruga amani.

Assaalmu alaikhum ndugu Watanzania Bara ( Tanganyika), Zanzibar na Viongozi wa UKAWA. Bila yakupoteza muda mwingi naanza kuingia kwenye Mada niliokusudia. Kama tunavojuwa kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafaida kubwa ndani yake ikiwa tu Muungano huu Utakuwa wa Serikali 3.. Kwasababu Mapato ya Muungano Yanatosha kuzisaidia Serikali hizi 2 ambazo zitakuwa na Mamlaka kamili kama Ukawa na CUF itashinda Uchaguzi wa October 2015. Jengine ni Makubaliano ya Ukawa kwamba Wazanzibari ( Mashekhe Wa Uwamsho) Walioshitakiwa Bara kwa Kosa la Ugaidi watolewe na kama wana makosa kweli yaendeshwe Zanzibar.

Sitaki kurudia kuchambua Muungano kwasababu sio Kusudio la mada hii, bali nina Habari nyeti nilizozipata kutoka kwenye Familia yangu ambamo tuna watu 2 ni Wanajeshi Wastaafu ambao Wanatumiliwa na CCM hivi sasa. Wametueleza kwamba CCM Wana Plan 3 kubwa ambazo watazitumia ili kushinda Uchaguzi wa 2015.

1. Plani ya kwanza, Nafikiri tunaijuwa sote ni ile yakutumia kura za Wizi ambazo zitapigwa na baadhi ya Mawakala waliokwisha lishwa Fedha.
b Kutumia watu wale ambao wamefanikiwa kupata Number na majina ya wananchi ambao walikuwa wakidangaywa Mitaani na watu Wasiojulikana ili wajiandikishe kwenye Organisation zakusaidia masikini.
c. Nikutumia TUMe za Uchaguzi kubadilisha matokeo ya Bandua Bandika.. Hili Liliwahi kufanywa kule Zanzibar Wakati wa Salmini Amour katika uchaguzi wa kwanza wa Vyama vingi 1995.

2. Plani ya pili, ni kuchelewesha kutoa Matokeo ya Uchaguzi kule ZAnzibar na Bara hasa matokeo ya Uraisi wa Muungano na uraisi wa Zanzibar. Kwasababu Wanajuwa kwamba wakizipata Nafasi hizi Raisi wa Tanzania akiwa wa CCM Atafinyangwa na Chama chao Aendelee na Sera zao za 1800. Na nafasi ya Uraisi wa Zanzibar kama tunavojuwa Dr Sheni Hana Say yoyote yeye Huburuzwa na Seif Ali Iddi kwakupitia Mkono wa CCM Bara. Hivo uchelewashaji wakutoa Matokeo ya Uchaguzi wa Maraisi utawafanya Watanzania wakusanyike au Waandae Maandamano. CCM walivopanga kutumia Vyombo vya Ulinzi kama vile JWTZ kupita mitaani na Silaha kali za Moto ili Watu Waliokusanyika Waogope na wakimbie.

b. Nikuzima Umeme, katika Mitaa yote ili kuwatia Wananchi Gizani katika kipindi hicho. Katika Sakato la kuzima Umeme Kutatolewa Vijana Wa CCM ambao Watavishwa Uniform za Vyama vilivounda UKAWA hasa Chadema na CUF ili baadhi yao Wavamie ofisi za Balozi hasa ( American na British, Norigean na Denish). Na baadhi ya Vijana hawa wa CCM waingie Mitaani kuchoma choma maduka na kuvunja vunja Vitu, kuiba na uharamia mwengine.. Hili ndilo tokeo wanalolitaka litokee ili Wapate kuwapaka matope UKAWA na Vyama vya Upinzani . Vile vile watakuwa na Ushahidi wa kupinga vyama vingi kushika hatamu ya Serikali na kuipa uzito Plan yao ya 3 ambayo wanaipanga kuifanya kama hizi plan 2 hazitafanikiwa. …. Kwa upande wa Zanzibar CCM watakaovishwa Nguo za Cuf wataanza kuchoma Makanisa kama walivofanya Wakati ule wa 2011.

(C) Nikutumia Vyombo vya Habari kutoa matokeo ya Wizi juu ya jamii au Majambazi ili wananchi wawe na hofu zakuto kutoka nje na badala yake wajifungia majumbani mwao ili CCM itangaze matokeo na ionekane Wananchi Wameridhika Nayo..Katika.

3. Plan ya tatu, Ni ile ilioandaliwa kuwalisha Sumu Watu Mabalozi juu ya Ugaidi ambao Kisiwa Kinachotuhumiwa kwa Ugaidi ni Zanzibar na Viongozi Wanao support Magaidi ni Viongozi wa Ukawa yaani ( Edward Lowassa na Maalim Seif Sharif). Kutokana na Maelezo ya Familia yangu hii ambayo ni Wakereketwa (bandia) wa CCM- Wametueleza kwamba Hii yakuwalisha maelezo juu ya Ugaidi Ndio linaandaliwa na Balozi Seif Ali Iddi Na kwasababu Wamewasikia Wapinzani wa CUF wakisema kama matokeo hayata tangazwa Wataandamana. Wanajuwa Wazanzibari Watakapo andamana wengi wao Watakuwa na hasira za Mashekhe Wao ambao Wametiwa ndani. Hivo mambango yatakuwa yanagusia Magaidi ( Mashekhe Wasio na hatia). Na pili wanajuwa Wazanzibari wakiandamana watavaa kanzu nyeupe hapo Ndipo wataoata Ushahidi kamili kwamba Wandamanaji hao ni Watu Wenye Msimamo mkali wa Kidini..

b Sumu nyengine itapikwa kwenye jamii zenye Madhehebu ya Ki-Kristo na Kiislamu kuanza kuonana Wabaya wenyewe kwa wenyewe. HGii ni njama inayotaka kufanywa kule Zanzibar yaani Unguja na Pemba.. Jamaa wanatueleza kwamba kuna Vijana wa CCM kutoka Bara Wameshaletwa Visiwani na Wanakaa katika Makambi za Majeshi na wengine watu Wenye asili ya Tanga kule Wawi wamelipwa Fedha nyingi Kufanya Uharamia wakuchoma Makanisa.. Watu hawa Watavishwa Uniform za CUF ili Ionekane CUF inapinga Ukristo na UKAWA iparaganyike.Tukumbuke Tutakapokubali kugaiwa Kidini au Kimadhebu ndio Tutatawaliwa.. Haya Yamewatokea Wazanzibari kugaiwa wenyewe kwa Wenyewe na mfumo huu huu wa CCM na Wamejiona wapi walipofika hivi sasa.

Nimemshukuru Kaka yangu huyu Mwanajeshi Mstaafu ambae amenambia niandike makala hii hara ili Watu wa Mitandao ya Kijamii Wawe na hadhari nini Mipango ya CCM kuhujumu Democrasi ya Watanzania Wenye Ustahamilivu na Heshima.. Na Ametueleza kwamba Kuna Document yakufanya hivo na Atatuletea atakapo ipata. Hivo Doccument hiyo tukiipata tutaiweka tena hapa Mtandaoni ili tupate Ushahidi wa Doccument ili tupate kuijadili kwa kina kirefu..

Ningewamba Wana Mzalendo Wachukue Ujumbe huu waupeleke mitandaoni ili na Wenzetu wa Bara wajuwe njama za CCM.. Pia ningeomba Ujumbe huu uwekwe kwenye makala za Mkono wa Kulia ili Tupate kuchangia na kusaidiana mawazo nini Tufanye ili Kuingoa CCM October 2015 ikiwa Kura zetu Zitaporwa?

No comments: