Tuesday 10 February 2015

Jimbo la Vunjo ni Jimbo litakaloleta Msisimko tena mwaka wa 2015


WAHENGA walisema ukiyastaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni. Hivi ndivyo unavyoweza kumwelezea Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Lytonga Mrema ambaye ataingia katika vitabu vya rekodi na historia kama mwana siasa “mtata” pengine kuliko wengine waliowahi kutokea hapa nchini.Mrema anaweza kuingia katika kitabu vya kutunza kumbukumbu za matukio muhimu ya dunia cha (Guinness Book of Record), iwapo madai na tuhuma zinazoelekezwa kwake zitathibitishwa na wenye kukusanya na kuhakiki ukweli wa data za kitabu hicho.Katika hali ya kushangaza na nadra kuonekana katika kampeni za uchaguzi, Mrema amekuwa akimpigia kampeni mgombea wa nafasi ya urais kupitia CCM, Jakaya Kikwete katika jimbo la Vunjo ambako yeye Mrema pia anagombea ubunge.Hatua hiyo ya Mwenyekiti huyo wa TLP imekuwa si tu ikiwashangaza wanasiasa wenzake; bali hata wananchi wa Vunjo kwa kumpigia kampeni mgombea urais wa CCM hadharani; huku chama chake kikiwa na mgombea wake wa urais Mutamwega Mugahywa.Hali hiyo imesababisha baadhi ya wananchi watafsiri kwamba CCM ina “wagombea wawili wa nafasi ya ubunge” katika jimbo hilo.


Wiki mbili zilizopita, Mrema pia aliingia matatani na wana CCM mkoani Kilimanjaro baada ya kutuhumiwa kuanzisha ushirikiano wa kisiasa usio rasmi baina yake na aliyekuwa Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro ambaye aliangushwa katika uchaguzi wa kura za maoni uliofanyika Agosti mosi mwaka huu.Imeelezwa kuwa, Mrema amekuwa akipita katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo akiwaeleza wapiga kura na wananchi kuhusu mambo mazuri aliyoyafanya Kimaro katika kipindi chake cha miaka mitano ya ubunge; huku akijinadi pia kuwa atamalizia kazi ambazo Kimaro alikuwa hajazimaliza.Baada ya kuwania urais kwa vipindi vitatu mfululizo mwaka 1995, 2000, 2005; huku katika vipindi vyote akishindwa kufua dafu, Mremasasa anawaniwa ubunge katika jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP naanapambana na wagombea vijana John Mrema (CHADEMA) na Crispin Meela (CCM).

Lakini sasa mwanasiasa huyo anashutumiwa na wagombea wenzake kutoka vyama hivyo viwili na baadhi ya wananchi kwa tabia yake hiyo ya kumpigia kampeni Kikwete katika mikutano yake wakati chama anachokiongoza pia kina mgombea wa wanafasi hiyo ya urais.Taarifa za uhakika kutoka vyanzo mbalimbali na baadaye kuthibitishwana viongozi wa CCM na CHADEMA, zinaeleza kuwa Mrema katika mikutano yake ya kampeni amekuwa akiwaomba wananchi wamchague kuwa mbunge wao lakini pia akimwombea kura mgombea urais wa CCM akidai kuwa ‘chama hicho kina sera nzuri.’Inadaiwa kuwa Mrema amekuwa akimnadi Kikwete hasa katika mikutano yake ya ndani na ile ya nyumba kwa nyumba kuwa wamachague yeye Mrema na kura za urais wampigie Kikwete kwani ni ‘rafiki yake wa karibu’, na pia kwa pamoja wanaweza kuleta manedeleo makubwa Vunjo.Mmoja wa viongozi wa TLP mkoani Kilimanjaro (jina linahifadhiwa) aliithibitishia Raia Mwema kuwa ni kweli Mwenyekiti wake wa chama amekuwa akimkampenia Rais Kikwete kwa muda; hali inayowapa tabu hata viongozi wa ngazi ya wilaya na wafuasi wao kwa ujumla.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, baadhi ya mikutano hiyo ni ileiliyofanyika katika maeneo ya Marangu Mtoni, Kirua Vunjo, Himo, Kilema nabaadhi ya vijiji katika kipindi cha wiki tatu zilizopita.“Ni kweli katika mikutano ya kampeni tuliyofanya katika maeneo tofautiya jimbo la Vunjo, Mwenyekiti amekuwa akiwashawishi wapiga kura wamchague yeye kuwa mbunge na kura za urais wampe mgombea wa CCM Kikwete ili washirikiane naye kuleta mabadiliko katika jimbo hilo….na hii hasa imetokea katika mikutano ya ndani”, alisema kiongozi huyo.Kiongozi huyo wa TLP aliongeza: “Hatua hiyo ya Mwenyekiti imekuwa ikiwachanganya wanachama wetu na hata wale wa CCM, na wengi wanadhani kuwa CCM imewasimamisha wagombea wawili wa nafasi ya ubunge katika jimbo la Vunjo, na hivyo wakati mwingine wananchi kuanza kutuhoji maswali kama viongozi wa ngazi za chini.”.Aliongeza kuwa, kama chama, wameshindwa kuchukua hatua zozote kwa kuwa ni vigumu kumshauri Mrema kutokana na tabia yake ya kutopenda kusikiliza ushauri kutoka kwa watu walio chini yake.Mrema pia amekuwa akiwasuta hadharani wote wanaobeza maendeleo ya Serikali ya Rais Kikwete na aliwahi kuzungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kilichofanyika mapema mwezi Juni alipopewa nafasi ya kutoa salamu za TLP ambapo alikaririwa na vyombo vya habari akiwaomba wana CCM waendelee kumsaidia Kikwete ili afanye vizuri zaidi.

Alisema ya kuwa katika marais wengi waliopita, Kikwete ni madhubuti na Mtekelezaji, na yeye Mrema anaumia roho sana anaposikia kuna watu wanambeza eti hajafanya lolote hivyo wamtose.Lakini pamoja na kumuombea kura Kikwete, Mwenyekiti huyo wa TLP pia anadaiwa kumpiga vijembe na kumshambulia mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk.Wilbroad Slaa kuwa hafai kuwaongoza Watanzania hali ambayo imemjengea uhasama na baadhi ya wananchi hasa wale wanaomshabikia mgombea huyo.Habari zaidi ambazo, hata hivyo, hazikuthibitishwa na vyanzo vya uhakika zilieleza kuwa Mrema ameingia katika harakati za kumsadia Kikwete kisiasa baada ya kufanya makubaliano na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM kuwa awasadie katika kupambana na upepo mkali wa Dk.Slaa ambaye nyota yake inazidi kung’aa ili naye aachiwe nafasi ya ubunge katika jimbo la Vunjo.Kuna uwezekano madai hayo yanaweza kuwa na ukweli kwa kiasi fulani kutokana na kauli za Mrema ambapo kama mwezi moja uliopita alikaririwa na vyombo vya habari, mjini Moshi, akitoa siku saba kwa Dk. Slaa aeleze sababu zilizomfanya akaacha utumishi wa Kanisa Katoliki lakini siku hizo saba zilipita bila Mrema kuuthibitishia umma alichopanga kukifichua.

Akizungumzia madai hayo, Katibu wa CHADEMA, Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema alisema wameyapata malalamiko hayo kutoka kwa wananchi na wanachama wao kuhusu vitendo hivyo vya Mrema, na wanachofanya ni kuwaelimisha wananchi wanaohudhuria mikutano yao ya kampeni katika maeneo mabalimbali ya jimbo hilo.Alisema kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko mengi dhidi ya Mrema kuwa ni kati ya wanasiasa wanaozoretesha kambi ya upinzani nchini na kuongeza kuwa kwa kumkampeni mgombea wa CCM sasa ameonyesha sura yake halisi.“Kitendo hicho sasa kinawapa picha Watanzania na wapenda mabadiliko wote nchini kuwa Mrema ni mwanasiasa mwenye sura gani….ni jambo la kusikitisha sana kwa kambi ya upinzani, lakini CHADEMA tunasema kuwa njama zake hizo hazitamsadia sana .. tumejipanga vizuri kupambana naye”, alisema Lema.Mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia CCM, Crispin Meela naye alieleza kushangazwa na hatua ya Mrema kumwombea kura Kikwete katika kampeni zake na kuongeza kuwa mwanasiasa huyo anaelekea kufilisika kisiasa.

“Sina maneno ya kuelezea hatua ya Mrema kumkampenia mgombea urais wa CCM….lakini kwa upande mwingine namshukuru maana anamwombea kura mgombea wetu”, alisema kwa kifupi Meela.Lakini Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Vicky Nsilo Swai alieleza kuwa mbinu anazotumia mgombea huyo wa TLP hazikubaliki katika kipindi hiki cha demokrasia ya siasa ya vyama vingi, na walikuwa wakijiandaa kuwasilisha malalamiko yao Tume ya Uchaguzi (NEC) ili imchukulie hatua za kisheria.Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alishindwa kufafanua kuwa hatua hiyo ya Mrema kuipigia debe CCM inaweza kuwa kosa kisheria.“Ni jambo la kusikitisha na ni utumiaji mbaya wa demokrasia…..kitendo cha Mrema hakikubaliki, na sisi tutawasiliana kwanza na Meneja waKampeni wa CCM kitaifa, Abdulrahman Kinana kabla ya kulalamika NEC…lakini nasema tena jambo hili halikubaliki, na ni aibu kwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama ambaye pia amesimamisha mgombea wa nafasi ya urais”, alisema Mama Swai.Alisema kuwa CCM haina mkataba wa kusaidiana kisiasa na TLP na wanapinga kwa nguvu zao zote kitendo cha Mrema kutangaza uzuri wa sera zao na kumwombea kura mgombea wao; kwani CCM na viongozi wake ina uwezo wa kuendesha kampeni bila ya kusadiwa na chama kingine chochote.Mwenyekiti huyo alisema anashangazwa na kitendo cha Mrema kuacha kwenda jijini Dar es Salaam kuzindua ilani na kampeni ya chama anachokiongoza kama Mwenyekiti wa Taifa, na badala yake anaendesha “fitina” za kisiasa katika jimbo la Vunjo.

Kwa upande wake, , alipinga madai yanayotolewa dhidi yake na kuita kuwa ni porojo ambazo hazina maana na madai hayo yanatolewa na wapinzani wake ambao wanaelekea kushindwa.“Nimepiga kambi Vunjo ili kuhakikisha kuwa ninashinda kwa kishindo na chama changu kiwe na mbunge katika bunge lijalo..….kwani chama ambacho hakina mbunge ni sawa na chama au kikundi cha kucheza ngoma”, alisema.“Na kwa nini wanakuja kulalamika kwa mwandishi ambaye yuko Arusha kama hayo si majungu?”, alihoji Mrema na kuongeza: “Kama wameshindwa siasa wakafanye kazi nyingine, kazi ya saisa watuachie sisi”.Mrema alisema kuwa katika Mkutano Mkuu wa TLP, uliofanyika mwezi wa saba, wanachama wote walikubaliana kwa kauli moja kuwa aweke kambi Vunjo na kuhakikisha ananyakua jimbo hilo kutoka mikononi mwa CCM na kazi hiyo anaifanya ipasavyo, na ndiyo maana ameshindwa kuhudhuria uzinduzi wa kampeni za chama chake kitaifa.Kutokana na kuzuka kwa madai hayo mapya dhidi ya Mrema, hali ya kisiasa katika jimbo la Vunjo inazidi kuwa tete na kampeni zenye ushindani mkali kutoka kwa wagombea wote watatu zinatarajiwa kushika kasi hasa katika awamu ya ‘lala salama’ mwezi ujao kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31 mwaka huu.

S

No comments: