Monday 12 October 2015

Ccm ikubali kubadilika na kukataa mabadiliko ndio mwisho wa chama hichi

Mapinduzi ya mawaziri wakuu na serikali 3

Baada ya mawaziri wakuu kupuuzwa kwa miaka mingi katika nafasi ya urais ,tunaona mawaziri wakuu hawa safari hii wameamua kukamata nchi na bora ingekuwa inaishia hapo,tunaona pia wakijaribu kubadili mfumo wa utawala katika nchi hii kutoka serikali2 mpaka 3.

Kwa nini nasema mawaziri hawa wakuu ndio kichocheo cha mabadiliko kutoka serikali 2 kwenda 3.
Kwanza tunaona nafasi ya uwazir mkuu ni nafasi nyeti kabisa katika nchi hii.

kuna wengine wanasema kiutendaji waziri mkuu ndio rais wa Tanganyika kwani waziri mkuu hujishughulisha na mambo yote yanayohusu bara/Tanganyika na pia ndio kiongozi mkuu wa shughuli za kiserikali katika bunge la Tanzania. Tunaweza kujiuliza kwanini mwaziri wakuu karibu wote wanaunga mkono muundo wa serikali 3?

ili kupata jibu la swali hili lazima tufahamu kwanza kazi za waziri mkuu.
Waziri mkuu Ndiye kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bara na bungeni.

Ndiye msimamiz na kiongozi wa wizara zote na katika shughuli zao wanakutana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha shughuli zao katika uendeshaji na usimamiaji wa serikali.

Mojawapo ya changamoto kuu ni mgawanyo wa madaraka,fedha za bajeti,usimamiaji wa wizara,mawasiliano kati ya bara na zenj pamoja na kero za muungano.

Na kama watu ambao wana uzoefu wa moja kwamoja wameliona tatizo la muundo na ndio waliotoa pendekezo la kuundwa kwa serikali3.

Ndio maana napoangalia marais wanaopinga huu muundo siwashangai,kwan muundo wa serikali 2 humpa madaraka makubwa rais na kumfanya aelemewe na kushindwa kuendesha nchi vizuri na hivyo hivyo kumpa kazi nyingi sana waziri mkuu ambazo mwisho wa siku hushindwa kuzitimiza zote, kutokana na kubanwa na kazi nyingi halaf kutokana na madaraka makubwa kupewa rais,waziri mkuu anakosa uwezo wa kuwabana wanaokosea mpaka ashughulike rais.

Tuangalie mawaziri wakuu hawa na michango yao katika kuiunda serikali 3

1.Joseph Warioba1985-1990 huyu ndio alieandika katiba mpya ambayo ndio chanzo cha ukawa na inasimamiwa na ukawa

2.Salim Ahmed Salim1983-1985 huyu naye alikuwa mwenyekiti msaidizi katika tume ya warioba kwa namna zote alishiriki na kukubaliana muundo wa serikali 3

3.Fredrick Sumaye 1995-2005 mwanzoni watu wengi tulihisi atakuwa haungi mkono harakati za serikali 3 ila kitendo cha kujiunga na ukawa ni ishara tosha kuwa yupo mstari wa mbele kuipigania serikali ya Tanganyika

4.Edward Lowassa2005-2008 huyu ndiye anayegombea kiti cha urais kupitia ukawa na ametangaza akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya 5 ataifufua serikali ya Tanganyika kwa kuunda serikali 3

5.John Malecela1990-1994 Serikali ya Tanganyika.huyu malecela alipata misukosuko iliyosababisha aondolewe katika nafasi ya uwaziri mkuu na nafasi yake kupewa Cleopa Msuya baada ya kubainika kuwaunga mkono G55 kundi la wabunge waliokuwa wakitaka serikali ya Tanganyika mwaka 1993 na mwl nyerere akamwandikia kitabu katika kumkemea na kumpinga.

Waliobaki Cleopa Msuya 1994-95,Mizengo Pinda 2008-2015 na wengine hatupo nao tena kama hayati Rashid Kawawa,Edward Sokoine na Mwalimu Julius Nyerere.

Naomba nihitimishe kwa kusema kwa kuangalia idadi ya mawaziri wakuu wanaounga mkono serikali kuwazidi waliounga mkono serikali 2 na ukiangalia wamekuwa wahanga wa muda mrefu katika kunyimwa nafasi ya kuwa rais, nadiriki kusema haya ni mapinduzi ya mawaziri wakuu

No comments: