Saturday, 24 October 2015

CCM WANATAPATA HAPA SEGEREA


Kuanzia wiki ilopita wanazunguka wakitangaza kuwa Mtatiro amejitoa. Jana nusura dereva wa gari yao moja auawe kwa sababu ya kutoa Tangazo hilo. Usiku wa kuamkia leo wamebandika picha walizotengeneza, ni picha za dada yetu Anatropia Theonest ambaye alikwishajitoa kisheria kwenye uchaguzi huu ili kulinda makubaliano ya UKAWA kuwa mbunge wa Segerea atatoka CUF.
Hizi ni dalili mbaya sana kwa CCM na wagombea wao. Ati wanadhani wananchi wataamini kuwa aliyebandika ni Anna. Akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa.

Jana usiku mitaa ya Karakata wananchi wamegawiwa almost milioni 10 fedha za Tanzania. Tuliweka mtego tukaita TAKUKURU hawakuja. Nchi yetu imeharibika sana, CCM imeshaharibu nchi hii kwa fedha za hongo, rushwa na kutowajibika. Ikiwa CCM inahonga fedha kiasi hiki ili kumpa ushindi Dk. Magufuli, wabunge na madiwani wao. Ni nani atapambana na wala rushwa baada ya CCM kuendelea kuongoza nchi? Unawezaje kupambana na rushwa ikiwa wewe mwenyewe umehonga wananchi matrilioni ya pesa ili kuingia madarakani??
Mungu yuko upande wetu na Segerea ni yetu sote. Inshalla tutaijenga kwa pamoja baada ya kupata ridhaa ya wananchi kesho.
Mtatiro J,
Segerea.

No comments: