Wednesday 7 October 2015

Mchungaji Mtikila aagwa Rasmi Diamond Jubilee


Rais Kikwete aongoza mamia kuaga mwili wa marehemu Mchungaji Christopher Mtikila Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumatatu Oktoba 7, 2015

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wake, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Hamad wamejitokeza leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kutoa heshima zao mwisho kwenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Democratic Party, Mchungaji Christopher Mtikila.

Rais Kikwete (katikati) akiwa kwenye msiba huo kabla ya kuuaga mwili wa Mch.Christopher Mtikila sambamba na viongozi wengine.

Rai wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akisaini katika kitabu cha maombolezo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisaini kwenye kitabu cha maombolezo.
Marehemu Mtikila alikuwa mwanasiasa mkongwe aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Oktoba 4 mwaka huu katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze Mkoa wa Pwani, wakati akirejea Dar es Salaam kutokea Njombe alikokuwa amekwenda kufanya mkutano wa kampeni.
Viongozi wa vyama vya siasa, taasisi na mashirika mbalimbali yalipata fursa ya kutoa shukurani zao za pekee kuzungumzia historia ya marehemu enzi za uhai wake ambapo kila mmoja alimzungumzia Mchungaji Mtikila alivyokuwa kiongozi shujaa, mwenye maamuzi na kusimamia kile alichokuwa akikiamini.
Akitoa salamu za rambirambi Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Jaji, Francis Mutungi amesema kuwa marehemu ameacha pengo kubwa kwa chama cha DP, kwani alikuwa kiongozi aliyekuwa akisimamia haki na kile alichokuwa akiamini na alikuwa hapindishwi na mtu yeyote na alikuwa ni mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu.
Alisema kuwa Mtikila alikuwa mwanaharakati asiyependa maandamano mwenye kuchukua maamuzi ya kwenda mahakamani kwa ajili ya kupata haki anayoitaka na ndiye alikuiwa mwanzilishi wa kudai mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Mwili wa marehemu umesafilishwa kwenda Ludewa, Njombe ambapo wakazi wa mkoa huo watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuzikwa. Anatarajiwa kuzikwa kesh

No comments: