Ujecha bado unaendelea, CCM bila ya ujecha isingekuepo:
TAARIFA KWA UMMA
CUF Chama cha Wananchi kinalaani kitendo kilichofanywa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Bw Daudi Mayeji kutangaza Matokeo tofauti na Kura zilivyopigwa na Madiwani wa Tanga. Uchaguzi huo wa Kumtafuta Maya na Naibu wa Jiji la Tanga umefanyika leo kwa kuhudhuriwa na Wajumbe 20 toka Cuf na Wajumbe 17 toka CCM hivyo kufanya Jumla ya Wajumbe kua ni 37. Kwa Uchaguzi wa Naibu Meya ambapo Cuf ilimsimamisha Mohammed Aniu na CCM ili msimamisha Mohammed Mambea, Msimamizi wa Uchaguzi Bw Selemani Zumo alitangaza Matokeo ya Kura kama zilivyopigwa na Kuhesabiwa, ambapo Mgombea wa Cuf Mohammed Aniu alimshinda Mgombea kwa kupata Kura 21 na kwa Kura 18. Utata ulizuka pale Mkurugenzi wa Jiji la Tanga alipoanza kutangaza Kura alizopata kila Mgombea wa nafasi ya Umeya ambapo alimtangaza Rashid Jumbe wa Cuf kupata Kura 18 na Selemani Bosi wa CCM kupata Kura 19 jambo lililopingwa na Wajumbe toka Cuf, ambapo waliotoa hoja ya Kuhakiki Kura hizo ambazo zilikua kwenye sanduku mbele yao. Cuf na Vyama vya upinzani bado vina kumbukumbu ya Mkurugenzi huyu alipokua Wilaya ya Kilindi pale alipowaengua Wagombea wote wa Upinzani na hivyo kufanya CCM kupita Bila kupingwa. Mkurugenzi huyu alishindwa kumtangaza Mgombea wa CCM kama alivyokusudia kufuatia vurugu kubwa na kulazimika kuokolewa na Polisi kutokana na hamaki za Wajumbe toka Upande wa Cuf.
Mpaka Muda huu nina Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mussa Mbarouk, Rashid Jumbe, Mohammed Aniu na Madiwani wengine watatu wapo Kituo cha Polisi wakitoa Maelezo kwa kile kilichotokea.
Cuf sio tu tunalaani Lakini pia tuna mashaka makubwa na tukio hili kwani limefanyika Huku kukiwa na Mmoja Kati ya Mawaziri wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Ummy Mwalimu. Kama waziri anashuhudia uhuni huu Kisha hapati taabu kwenye nafsi yake, basi ni dhahiri Nchi hii ina mapungufu makubwa kwenye eneo la Demokrasia na Mambo ya Utawala Bora.
Misimamo wa Cuf, tunamtaka Mkurugenzi wa Jiji la Tanga kumtangaza Mshindi halali wa Nafasi ya Meya kama Kura zilivyopigwa na Wajumbe wa Kikao hicho. Kama Hilo halitafanyika, Cuf itatangaza Hatua zitazofuata.
Abdul Kambaya
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma
CUF TAIFA
No comments:
Post a Comment