Sunday, 20 December 2015

Wazanzibari: Sisi Ndio Waamuzi Wa Hatma ya Visiwa Vyetu.
Tunachukua Nafasi Hii kuandika Makala hii Kwakutoa ONYO KALI Kwa CHama Au Kundi Lolote Linalo SHAWISHI CUF Kukubali KURUDIWA KWA UCHAGUZI VISIWANI MWETU.. Sababu yakuandika ONYO Hili nikutokana nakuona Kwamba Chama Cha CCM ZANZIBAR Kikisaidiwa na Viongozi Wa TANGANYIKA wametuzalilisha Sisi Wananchi Wa Zanzibar- Tukisema Hivi Tunamaanisha kwamba:
– Siku ile CCM (BARA) Walipoamua Kuleta JESHI Kubwa la Tanganyika katika Miji na Vitongoji Vya Zanzibar.
– Kuiteka TUME Ya Uchaguzi ZEC na Kituo cha Matangazo ya Uchaguzi kuwekwa Under Military Control ya JWT.
– Kumteka Mwenyekiti Wa TUME na KUmlazimisha Kufuta Uchaguzi Mzima wa 25.October 2015; Wakati KURA Zimehesabiwa na Kutangazwa katika Vituo Vya Kupigia kura bila ya Malalamiko yoyote yale.
– Na chakushangaza Zaidi Nikwamba Kura Hizi Hizi Ziliokuwa HARAMU kwa Chama kilichoshinda na Kuwa HALALI Upande Wa Pili Wa (WABARA). Nakutumia Kura Zetu Zinazokataliwa hivi sasa na Kumuongezea Magufuli Ushindi.

Tunataka Kutoa Wito Kwa Viongozi Wa CCM- ZANZIBAR na Wale Wa TANGANYIKA Kwamba:

1. Wazanzibari Ni Binaadamu Kama Watanganyika, licha yakuwa na Tofauti ya MAJINA, DINI NA RANGI. Lakini Sisi tunahaki Za Kiraia na Haki za Kuchagua Viongozi Tunao Wataka Watuongoze -kama Walivokuwa na Haki Hii Wananchi wa Tanganyika na SI VYENGINEVO.

SIKU ya tarehe 28.October 2015, haki yetu hii ( WAZANZIBARI) ambayo tuliisubiri kwa HAMU Sana- na tumeitekeleza Kwa Njia za AMANI Na UTULIVU Kabisa Tumenyanganywa na Viongozi wa CCM TANGANYIKA kwa kushirikiana na CCM WAHAFIDHUNA waliopo hapa Zanzibar. Na hakuna Asiejuwa Kwamba Serikali ya CCM TANGANYIKA Ndio Inayomiliki Vyombo Vyote Vya ULINZI wa JWT na POLISI- na Siku ya Tarehe 28.October Zanzibar, Kulimiminwa JESHI Kubwa Sana Ili KUIKINGIA KIFUA CCM Ikatae Matokeo ya Uchaguzi ambayo Yalikuwa Yanampa Ushindi Maalim Sefu Sharif Hamad. Matokeo yake ni Wazanzibari Ambao ni RAIA wa Kawaida Wameendelea Kuishi Ndani ya Dhulma, Manyanyaso, na Khofu Mpaka Leo hii sasa tunaandika Makala hii. Vile vile, Kinachoendelea Sasa ni Wazanzibari kusikia Propagander za Kisiasa Ambazo Zinashi-ndikizwa na Baadhi ya Viongozi Wa KIBARA Dhidi ya CUF kukubali kurudia Kwa Uchaguzi.

La Ajabu ambalo tumeliona Sisi Wazanzibari Nikwamba miaka 20 Ya Vyama Vingi CUF Imekuwa Ikishinda Chaguzi Zote Lakini CCM Waliwaibia. Na Pale CUF Ilipokuwa Ikilalamika Uchaguzi Urudiwe CCM TANGANYIKA Hawakusema KItu Wala KUINGILIA SUALI HILI.. IWEJE LEO VIONGOZI WA KIBARA Wapate MIDOMO MIREFU YA KUITETEA CCM ZANZIBAR?

2. Hivo Tunataka Kuwaeleza Viongozi Wote Wale Wanaoamini Kwamba Uchaguzi Wa ZANZIBAR Ulikuwa na FUJO Na Unahitaji Marudio. Mtu Huyo Au Kundi Linalosimama na Kauli Hiyo HAWATUTAKII MEMA SISI WANANCHI WA ZANZIBAR.. Wanachokifanya Watu Hawa Nikutaka Kuiweka ZANZIBAR Katika Vita Vya WENYEWE KWA WENYEWE ILI WAO WAENDELEE KUTUTAWALA KIMABAVU. WaZanzibar Tayari Wameshauliwa Ndugu zao 1964, 1995,2010 na mpaka sasa watu wanavamiwa nakupigwa Ovyo Ovyo- lakusikitisha Hatuja Msikia Kiongozi Yoyote Yule Kutoka Bara akikemea Suali Hilo Au Hata kuolitaka Jeshi lililowekwa Zanzibar kurudi Kwao Tanganyika. Kwahivo Sisi Wazanzibari Tunatoa Wito Kwa WAHAFIDHINA, Umwagaji Wa Damu Nunao Utafuta Watakao Athirika sio CUF au Wapinzani Pekeyao ni Wazanzibari Wote na Itakayoteketea ni Mali ya wazanzibari Wote. WATANGANYIKA ambao Sasa Hivi wanapalilia Ugomvi wa zanzibar wanahisi hawato athirika. Lakini TUNASEMA LIKIPIGWA ZANZIBAR BASI BARA LITACHEZWA TUU BIIDHINILLAH..

Jengine Sisi Kama Wananchi Wa Visiwa Hivi, Tunaamini Kwamba Marudio Ya Uchaguzi Sio Maamuzi Ya Chama. Bali Ni Maamuzi ya WANANCHI WENYEWE. Na Sio Hivo Tu Bali Hata Uchaguzi Ukirudiwa X100 Basi CCM Hawatatoa NCHI kwa VIKARATASI Yaani ( Kutumia Kura).. Meneno haya Wameshasema Kinaga Ubaga Katika Bunge La TANGANYIKA Kule DODOMA na Kupata BARAKA ZOTE ZA WATANGANYIKA WANAOICHUKIA ZANZIBAR.

a. Tukisema Hivi Tunamaanisha Kwamba Sisi Wazanzibari Tumeamuwa Ku-Ikataa CCM kuendelea Kukaa Madarakani Kwa Sababu Tayari Chama Hiki Kimeshatawala Zanzibar Zaidi ya Miaka 50 Sasa Chini ya ASP na Baadae Chini Ya CHAMA cha TANU ambacho Kinajiita CCM. Hivo Hata Uchaguzi Urudiwe Sisi Tutaamua Kuikataa Tena CCM na CCM Itaendelea Kukataa Matokeo hayo.. Jee Kuna haja Gani ya Viongozi Wa KIBARA Kuchochea Kwamba Uchaguzi Urudiwe??

b.Kutokana Nakuona Maendeleo Yaliokuwapo Miaka ya 80s sasa yanazidi Kudidimia Chini na Zanzibar au Wazanzibari Kupoteza kuzidi Umasikini, Kupoteza UTU na Silka Zao. Ndio Sisi Wazanzibari Tumeamua Kutokichaguwa Chama cha CCM. Na Sisi Ndio Wenye Maamuzi yakurudia kwa Uchaguzi Au Kutorudiwa.

Kwa kukumbusha CCM Wahafidhuna na WABARA tunawaeleza Katika Uchaguzi 25.October Mshindi alipatikana. CCM WA KIBARA na WAKIHAFIDHINA Wanajuwa kwamba Chama cha CUF ndio Kilichopata RIDHAA Kutoka Kwa Wananchi Wa Zanzibar Ili kuongoza SERIKALI ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Sio Tu Chama cha CCM Kwamba Wanajuwa bali Hata Nchi Za ULAYA, SADIQ na UNDP Zote Zinaelewa Hivo. Kwahivo Uchaguzi Unaopigiwa DEBE na CCM BARA au Wahafidhuna Sio Uchaguzi Bali Wanatafuta Umwagaji Wa DAMU za Wazanzibari Wasio na Hatia Ili CCM Walipe VISHUO Vyao.

Namalizia makala Yetu Nikisema Maamuzi ya Uchaguzi hayako Ndani ya Chama chochote Kile na Sisi Wazanzibari Tumekuwa hatuamini Kwaba Marudio Ya Uchaguzi Yanaweza Kutubadilishia Maisha yetu na Dhiki Zetu.. Tayari Tumemchagua Kiongozi ambae Tulitegemea angetuvusha katika Umasikini na Unyonge lakini Kwa Faida za Viongozi Wachache Wamezuia Mabadiliko na Imani za Wazanzibari.. Hivo Basi Tunawaomba Wale Wanaoamini Kwamba Watatumia NGUVU Kulazimisha Uchaguzi. Na Kusababisha Umwagaji wa DAMU.. Sisi Wazanzibari Tunasema Kwamba DAMU ya WAZANZIBARI Ikimwagika serikali ya Muungano ndio mhusika mkuu.

No comments: