Tuesday, 12 January 2016
Miaka 52 ya Mpasuko wa Zanzibar na Mpasuko wa CCM Zanzibar
Ikiwa sasa imetimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar uhakika Zanzibar imepita kwenye dharuba za mawimbi mazito kuanzia kuundwa kwa vyama vya mwanzo Zanzibar mwaka 1957 Vyama vya Zanzibar Nationalist Party (ZNP )au Hizbu na ASP au Afro Shirazi party.Zanzibar ilipata uchaguzi wake wa kwanza Mwaka 1961 na Uchaguzi ukarudiwa tena Mwaka 1963 na kusababisha mapigano na kuuliwa watu 68.
Lengo la Mkoloni Muingereza likua serikali itakayochaguliwa na Wazanzibari ikabidhiwe uhuru wake .Mfumo wa uchaguzi uliokuapo Zanzibar ulikua ni kama mfumo wa Muingereza chama kinachopata viti Vingi ndio kinachounda serikali uchaguzi wa 1963 ulileta Mpasuko pia kwenye Chama cha ASP kilichokua na Mvutano wa watu weusi wa Zanzibar na weusi wenye asili ya Bara au wahamiaji kutoka Tanganyika.
Balozi Othman Sheriff na wenzake kina Abrahman Babu pia alijitoa ZNP na na kujiunga na Mohammed Shamte Mbunge wa Chambani chama chao kilichoitwa ZPPP( Zanzibar and Pemba Peoples Party..au maarufu Umma Party wakiwamo vijana waliokua wakiamini mfumo wa Ukomred au ujamaa kina Dr Salim Ahmed salim .
Uchaguzi wa 1963 ASP na ZNP kila kimoja kilipata VIti Tisa na ZPPP walipata viti vitatu . ASP waliwataka ZPPP waunde serkali ya Mseto pia ZNP waliwataka ZPPP pia waunde serkali ya Mseto .
Wabunge watatu wa ZPPP waligawanyika wawili waliunga mkono ZNP na mmoja liunga mseto wa ASP lakini umoja wa ZNP na ZNPP uliweza kuunganisha viti vyao na kuunda serikali ya umoja na sharti la Chama hichi kidogo ni kuwa wao wataunganisha viti vyao lakini wapewe nafasi ya Waziri Mkuu Kilichowaponza ASP walikataa kuitoa nafasi ya Waziri Mkuu na ZNP walikubali kauachia nafasi kuu ya Uwaziri Mkuu kuenda kwa chama kidogo kabisa kuhakikisha mahasimu wao ASP hawaingii mdarakani.
Siasa na Kampeni za uchaguzi za mwaka 1961 na mwaka 1963 zilikua ni uhuru wa Mweusi dhidi ya asiekwua Mweusi siasa hizi bado zinawatafuna Wazanzibari baada ya miaka 52 baadya MApinduzi ya Mwaka 1964.
ZNP na ZPPP waliunda serikali chini ya Waziri Mkuu Mohammed Shamte Mpemba wa Chambani. baada ya serikali hii kuundwa mwezi mmoja baadae ilipinduliwa na watu waliotaka Zanzibar iwe na siasa za ukoministi ni vijana waliotoka Cuba kupata mafunzo ya Kijeshi chini ya Kamanda wao Abdul Rahman Babu.Vijana hawa walipelekwa siri na ABdulrahman Babu huko Cuba , China na Urusi ya Wakati huo USSR.Baadya Mapinduzi ya Zanzibar pia kulitokea jaribio la Kijeshi kumpindua Nyerere huko Tanganyika.
March 1964 baada ya Mapinduzi vyama vya upinzani vilifutwa Zanzibar na kubaki chama cha ASP peke yake .
Kesho nitaeleza Miaka 52 ya Serikali ya ASP /CCM ZANZIBAR, Mauaji na Mpasuko wa CCM ZANZIBAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment