Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent Mashinji, akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuchaguliwa, kwenye Mkutano Mkuu uliokuwa ukifanyika Jijini Mwanza. Dkt. Mashinji anaziba nafasi iliyoachwa wazi na Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Willbload Slaa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, Makamu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Mh. Said Issa Mohamed pamoja na Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Mh. Edward Lowassa wakifatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu mpya wa Chama hicho, Dkt. Vicent Mashinji
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA wakishangilia baada ya kupatikana bila kwa Katibu Mkuu mpya, Dkt. Vicent Mashinji.
WASIFU WA DK. VECENT MASHINJI
Dk. Mashinji aliyezaliwa katika Wilaya ya Sengerema, alianza elimu ya msingi katika Shule ya Iligamba Januari 1981 hadi Oktoba 1987 na kisha kuendelea na masomo katika Shule ya Sekondari ya Makoko Seminari kuanzia Januari 1988 mpaka Oktoba 1991 alipohitimu na kufaulu kujiunga na Shule ya Sekondari Mzumbe kuanzia Julai 1992 hadi Juni 1994 alipohitimu kidato cha sita.
Alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere Uganda mwaka 1995 hadi alipohitimu mwaka 2001 na kutunukiwa shahada ya udaktari. Mwaka 2003 hadi 2005 alisomea Shahada ya Uzamili ya Anaesthesiology katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya Muhimbili (MUHAS) na mwaka 2007-2010 alijiunga na Taasisi ya Teknolojia ya Blekinge ya Sweden ambako alisomea Shahada nyingine ya Uzamili, safari hii katika Utawala na Biashara (MBA).
Hivi sasa ni mwanafunzi wa Shahada nyingine ya Uzamili katika Afya ya Jamii anayosomea Chuo Kikuu cha Roehampton, Uingereza na pia Shahada ya Uzamivu ya Uongozi katika Chuo Kikuu Huria.
No comments:
Post a Comment