Saturday 14 May 2016

Hukumu kesi ya Kafulila Mei 17

ERDINAND Wambali Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora anatarajiwa kutoa hukumu ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Kusini tarehe 17 Mei mwaka huu, 
Kesi hiyo ya kupinga matokeo ilifunguliwa na David Kafulila aliyekukuwa mgombea wa ubunge katika jimbo hilo kupitia chama cha NCCR-Mageuzi dhidi ya mpinzani wake Husna Mwilima wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayedaiwa kupoka ushindi wa Kafulila.
David Kafulila aliyekuwa Mgombea Ubunge  jimbo la Kigoma KusiniWambali anayesimamia kesi hiyo katika taarifa yake iliyotolewa jana mjini Tabora amesema kuwa, amepanga kutoa hukumu tarehe hiyo baada ya pande zote mbili kuwasilisha ushahidi na maelezo yao
Awali, Jaji Wambali aliamuru Mwilima kuwasilisha ushahidi uliompa ushindi lakini pia msimamizi wa uchaguzi huo naye apeleke ushahidi uliomfanya ampe ushindi Mwilima.
Baada ya kukamilika kwa ushahidi huo, Wambali aliomba kupatiwa muda wa kutosha ili kupitia ushahidi huo na vielelezo vilivyowasilishwa ili aweze kutoa hukumu ya haki.
Huku akisema, Ruben Mfaume aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, ambaye alikuwa msimamizi wa wa uchaguzi jimbo hilo ni mshitakiwa wa tatu katika kesi hiyo.
Katika kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015, Kafulila anaishawishi mahakama itengue matokeo yaliyompa ushindi mpinzani wake   Mwilima badala yake imtangaze yeye kama mshindi halali wa jimbo hilo kwa mujibu wa kura zake.
Walalamikiwa katika kesi hiyo ni pamoja na, Mbunge wa jimbo hilo, Mwilima , Mfaume, na Mwanasheria wa serikali anayewakilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Ktika kesi hiyo wakili Kenedy Fungamtama anamtetea Mwilima huku Kafulila akitetewa na mawakili watatu Prof. Abdallah Safari,Tundu LissU na Daniel Rumenyela.

No comments: