Wednesday 8 June 2016

Tanzania yarudi,enzi za chama Kimoja?

Masuala Matano Muhimu yaliyoibuka Wakati wa Mahojiano ya Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe na Polisi, Leo Jijini Dar es salaam.

• Maombi ya Chama Cha ACT Wazalendo ya mkutano ilikuwa 'Kujenga Chama' Lakini Chama Kilizindua "Operesheni Linda Demokrasia" (Operesheni ambayo Ni Sehemu ya Ujenzi wa Chama, Maana Kama Demokrasia ikiachwa iteketezwe Na Serikali ya Rais Magufuli, bila Kulindwa, Basi hata Uwepo wa Vyama Vingi Utakuwa Mashakani).

• Kusema "Rais Ameropoka kuhusu Sakata la Sukari Nchini" (Kwa kuelezea Namna alivyoueleza Umma akiwa Babati Kuwa Kuna Sukari imefichwa Na kukamatwa Mbagala, Taarifa ambazo TRA na Takukuru walizikanusha na Kusema Sukari Husika haikuwa imefichwa).

• Kumchonganisha Rais na Wananchi kuhusu suala la kuwaita Vijana wa Kitanzania Kuwa ni "Vilaza" (Kwa Kumnukuu Rais Mwenyewe alipowakashifu Vijana hao Wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam).

•Kumgombanisha Rais na Wananchi kwa Kusema "Yeye anajifanya Rais wa Masikini (Huku akiwakashifu hao Watoto wa Masikini Kwa Kuwaita "Vilaza") na hivyo kumgombanisha na wasio Masikini" (Pamoja Na Kunukuu Kuwa Kauli ya Kuwa Yeye Ni Rais wa Masikini ameitoa Mwenyewe Rais).

• Kumwita Rais Dikteta na Kwamba anaendesha Nchi Kiimla (Pamoja Na Kutoa Mifano ya Udikteta wake Kama Kulipangia Uongozi Bunge, Serikali yake Kuondoa Bunge Live, Kuwafukuza Bungeni Wabunge wanaotimiza Wajibu wao wa Kuihoji Serikali na Kudhoofisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Za Serikali Nchini, CAG Kwa Kuiondolea Kiwango Cha Bajeti iliyopangiwa kinyume Na Sheria).

Maelezo ya Jeshi la Polisi ni Kuwa yote hayo yanaangukia kwenye Kifungu Cha  89(1)(a) cha Penal Code, Yaani "Kutumia Maneno ya Matusi yenye Kuweza Kuvunja Amani" (Abusive Language).

Jeshi la Polisi limemuomba Ndugu Zitto afike Tena Kituoni Hapo Juni 15, 2016 Kwaajili ya Mahojiano zaidi.

Mwanasheria wa Ndugu Zitto ameliomba Jeshi la Polisi kupeleka Mashtaka Mahakamani Juu ya Suala Husika, Na Kwamba Ndugu Zitto atakwenda Kuthibitisha Ukweli Na Undani wa Masuala hayo Mahakamani.

No comments: