Tuesday, 11 July 2017

UAMSHO WAMESUTWA NA WAZANZIBARI ?

angu kutajwa kwa mchakato wa kukusanya maoni juu ya katiba mpya, wananchi na tasisi mbalimbali za kiraia nchini Zanzibar wamekuwa wakifuatilia kwa ukaribu hatua hiyo kwa kufuatilia mijadala mbalimbali na hatimae kufikia kuwasilisha maoni yao kwa tume husika. Wengi watakubali kwamba jumuiya ya Uamsho imefanya kazi kubwa katika kuyachambua masuala mbalimbali ambayo Zanzibar ingeyahitaji kuzingatiwa katika katiba mpya.
Katika kufanya hilo, serikali za Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Muungano wa Tanzania hazikuweza kuvumilia mwenendo huo kwa kile walichokiita “uchochezi, fujo, uharibifu wa mali na matusi”. Hatma ya viongozi wa Uamsho imeishia kuwekwa kizuizini kwa takriban miezi miwili sasa.
Tukio la kuwekwa ndani kwa viongozi wa Uamsho limewatia khofu wengi ya wafuasi wake, na wale wanaoamini sera zake, hivyo kuwafanya wawe kimya si tu katika kuendeleza harakati za madai yao, lakini hata katika kuwatetea viongozi hao. 

No comments: