#Sarafu
Turudi kutazama historia na jinsi gani haya masuala ya exchange rate yalipoanzia duniani. Baada ya vita ya pili ya dunia, Madeni yalitawala soko la dunia. Muingereza alidaiwa na Marekani, nayo ikiwadai Ufaransa na nchi nyengine zilizowasaidia katika vita ile; nao halkadhalika wakalielekeza deni kwa Ujarumani. Inasemekana haya madeni yalianzia tokea vita ya kwanza ya dunia ila sasa hali ikawa mbaya zaidi katika uchumi wa dunia. Katika kulipana ndio likazuka hili suala la sarafu ya kulipana na kila mmoja akashashua thamani ya sarafu yake kama njia za kukabiliana na hali mbaya ya uchumi na madeni yaliowazunguka.
#BrettonWoodFixed
Hapa ndipo lilipoanza hili suala la fixed exchange rate ambapo lilijulikana kama Brent Wood System ambayo sarafu ikawekewa kigezo cha dhahabu katika kubadilishana na kwa vile Marekani ndio iliokuwa na shehena kubwa ya dhahabu katika milki yake ndio nayo dola ya Marekani ikawa ndio sarafu ya kutumika zaidi duniani huku yenyewe ikiweka kiwango cha $35 kwa ounce moja ya dhahabu kipindi hicho.
#FixedExhangeRate
Mfumo huu wa Brent wood ukaweka sharti za sarafu kubadilishwa kwa kigezo maalum na haikufuata soko lilivyo. Kwa kipindi kile ilikuwa ni jambo sahihi kwa sababu ya hali ya uchumi ulivyokuwa duniani baada ya vita ya pili ya dunia. Miongoni mwa masharti yake ni kuwa serikali itaweka kiwango maalum cha ubadilisho wa sarafu ya kigeni na kuhakikisha sarafu ya nje inauzwa na wale tu waliopewa kibali hususan mabenki chini ya uangalizi wa benki kuu ya nchi. Ni sawa na tunavyoona sasa ambapo wimbi la maduka ya kubadilisha pesa za kigeni kufungwa na amri zinatolewa zinazoonyesha kabisa hatufuati tena mfumo wa soko linavyotazama mahitaji na usambazaji (demand and supply).
#FlexibleExchangeRate
Mfumo huu ambao ndio unaoshika nafasi kubwa katika dunia ya leo kwa vile hutazama soko lilivyo na uhuru wake. Mfumo huu unahitaji sera madhubuti za uchumi hasa zingatio katika madeni, pamoja na ile deficit ya soko katika mahitaji ya bidhaa za kuingia na zile zinazotoka. Miaka ya 70 nchi nyingi zilijiondoka katika mfumo wa fixed exchange rate na kuweka hii “fluidity” ya sarafu kutokana na ukweli wa hali ya uchumi ulivyo. Ukiziona nchi zimerejea katika mfumo wa fixed exchange rate basi itazame hali yake ya uchumi utaikuta itaaban na ndio njia pekee ya kung’ang’ania sera dhaifu za kiuchumi zisiokidhi matakwa ya uendeshaji wa uchumi mzuri. Kwa sasa nafikiri listi ya nchi zinazoendelea na mfumo huu ni chache ikiwamo Zimbabwe, Iran, North Korea na za mfano wa hali zao.
#Uingereza
Miaka ya 30 sera hizi ziliwahi kutangazwa na serikali ya chama cha Labour kwa sababu ya vita ya kwanza ya dunia. Hali ya uchumi ilianguka na madeni yakaongezeka na njia pekee ya kukabiliana na mashaka yalioletwa na vita ya kwanza ya dunia yalisababisha kufuatwa kwa mfumo huu mpaka pale ulipobadilishwa katika miaka ya 70. Wachumi wengi huutazama muda huu kuwa ndio sababu ya mashaka makubwa yalioharibu zaidi uchumi wao na ongezeko la wasio na ajira. Ilisaidia kwa kipindi cha vita lakini ulidumishwa mpaka alipokuja Thatcher akauondoa.
#AfrikaKusini
Halkadhalika katika kipindi cha Zuma sera hizi zilirejea Afrika Kusini na kusababisha anguko la uchumi wao kutokana na makatazo mengi yanayoendana na uwepo wa fixed exchange rate. Kwa makampuni makubwa yaliokuwa na makao makuu Afrika Kusini lakini yakiendesha shughuli zake kwengine ilikuwa ngumu kuendelea na malipo kiurahisi wakati makao makuu yakiwa katika himaya ya fixed exchange rate. Hata wale walioamua kuhama nchi walipoteza kiasi kikubwa cha pesa zao kutokana na hizi “restrictions” za fixed exchange rate.
#Dual Fixed/Flexible Exchange Rate
Kuna tafiti iliofanywa India walipoamua kuweka mfumo wa flexible kwa asilimia 60 na 40 kwa fixed. Kwao waliona watanufaika na urahisi wa kupeleka bidhaa za nje kwa anguko la sarafu yao dhidi ya dola kwa kutumia asilimia 60 walioweka kwa “flexible flow” na hapo hapo kwa mfumo wao wa fixed exchange kwa Capital na hivyo kufaidika na ile import kwa bei inayotazamwa na mfumo huo. Kiundani ni vigumu kuuelewa lakini hata hivyo nao haukuonekana wa manufaa na wakaamua kujijengea mazingira mazuri ya kuhakikisha wanakwenda moja kwa moja katika mfumo wa sarafu kubadilishwa ikitegemea soko badala ya serikali na maficho ya sera dhaifu.
#Hasara
Katika hasara kubwa ya mfumo huu wa Fixed exchange rate ni serikali kuweka mbinu zinazopunguza imani ya uwekezaji kutokana na kukosekana umahiri katika kutambua hali halisi ya sarafu ilivyo dhidi ya nyengine (transparency). Mfano mzuri mwengine ni Venezuela ambapo haya yalifanyika kimkakati dhidi ya matajiri na matokeo mabilioni ya fedha za watu zikayeyuka ghafla huku nayo Venezuela ikingia katika umasikini mkubwa na kudorora zaidi kwa uchumi wake.
#Magendo
Jengine ni kuwa mfumo huu wa fixed exchange rate hupelekea ongezeko la magendo ya fedha za kigeni na huchochewa zaidi na nchi jirani ambazo kwao ni fursa ya kujijenga zaidi kiuchumi kwa kufungua zaidi soko lake na kwa urahisi mkubwa. Haya yalikuwepo Tanzania kipindi cha Mwalim na kulitokea ongezeko la ubabe wa watu kutaifishiwa mali zao wengine ni kwa kukomolewa au tu dhana ya kuwa ni mhujumu wa uchumi. Yatarudi kwa sababu hali halisi ya sarafu yetu ni dhaifu, magendo yanaweza kuwa tegemeo la utajiri wa haraka hasa pale mahitajio ya sarafu husika kuzidi. Ni sawa na hivi sasa ambapo utasikia uchumi umekuwa (Vitabuni), lakini kiuhalisia walio masikini wanaongezeka hasa wale wasiomudu dola moja kwa siku. Exchange rate haitaki hivyo, tusome kwengine na athari zao.
#Watabiri
Halkadhalika wako wanaofaidika na mfumo huu moja kwa moja. Mfano mzuri ni wale “Speculators” ambao kazi yao ni kutazama jee serikali inazo fedha za kigeni za kutosha kukasimu mfumo huu wa fixed exchange rate ambao huhitaji serikali kuwa na akiba kubwa ya fedha za kigeni na vile vile za ndani ili kuweza kumudu ile “artificial demand and supply” ya sarafu yake. Inapotokea “speculators” wakahisi serikali haikidhi vigezo basi huzinunua fedha kwa wingi na kuzibadili kwengine huku wakizirejesha zinazohitajika kwa faida kubwa zaidi. Uingereza iliwahi kukumbwa na kadhia hii kipindi cha mwanzo cha Euro ambapo speculators walinunua sarafu yao wakaibadili Ujarumani na baadae wakairejesha ikiwa na thamani kubwa zaidi kwa vile sokoni haikuwapo wakafaidika na ongezeko la thamani.
#UsawaKibiashara
Katika misingi bora ya kiuchumi, usawa kibiashara (trade balance) hupatikana katika flexible exchange rate kwa maana ya kuwa ikiwa kuna “trade deficit” basi fedha ya kigeni huzidi thamani na hivyo kuzifanya bidhaa za nje kuwa ghali na kutovutiwa katika soko la ndani na hivyo moja kwa moja ile trade deficit kufidiwa. Katika Fixed exchange rate hili hukosekana na ndio chanzo cha anguko zaidi la uchumi.
#SeraFiscal
Hata sera za kiuchumi (fiscal policies) huwa haziendani vyema na mfumo huu wa fixed exchange rate kwa sababu utawezaje kupunguza kodi au kuongeza fedha zaidi za ndani katika mzunguko bila ya khofu kubwa ya kutokea trade deficit? Hizi fiscal policies hufanya kazi vizuri katika mfumo wa flexible exchange rate. Ukweli ni kuwa katika mfumo huu wa fixed exchange rate kuna nafasi kubwa ya kupanda kwa kodi na kupunguza ongezeko la pesa katika soko hasa panapotokea trade deficit na hili ndilo chocheo kubwa la kuporomoka kwa ajira.
#kujilindaHedging
Masoko ya dunia hasa ya leo yamejidhatiti katika kutafuta njia za kuongeza faida. Hivyo hizi Fixed exchange rate huwa chocheo kwa vile uwepo wa mifumo mengine katika taasisi mbali mbali zinazojilinda na anguko la thamani ya sarafu (Hedging). Mara nyingi taasisi huwa na makubaliano ya kibiashara ambayo hutoa uhakika wa kutoathirika na anguko la thamani mapema katika makubaliano yao ya kibiashara, matokeo yake ndio yale yale athari hasa katika trade deficit na upandaji wa kodi huku pesa zikipungua katika mzunguko. Ni vigumu kukuta taasisi ikiingia makubaliano bila ya uhakika huu, anaebeba mashaka ni serikali katika hii Fixed exchange rate huku tayari taasisi zikiwa na mfumo wa malipo usioathirika.
#FaidaFixedExchangeRate
Faida zake zaidi katika kujenga nidhamu ya soko na uchumi pale ambapo anguko la sarafu ya ndani linapozidi kuongezeka. Lakini athari zake ni kubwa zaidi maana ni “artificial strategy” ya kuizuia sarafu ya ndani kuanguka. Inawezekana ikawa na faida kwa utulivu wa kiuchumi au hata kuzipa mamlaka husika heshima ya udharura katika soko, lakini bado huwa ni kiini macho maana uhalisia ulivyo hauendani na masharti yanayoipa nguvu sarafu ya ndani isiobebeka.
#Mbadala
Halkadhalika huweka njia mbadala za kuhakikisha uwekezaji kuendelea na biashara za kimataifa kutosita na hata kupunguza athari za mara kwa mara za speculators lakini mara nyingi speculators huziganda nchi zenye mfumo huu wa fixed exchange kutokana na ugumu wake wa kuhakikisha wingi wa fedha ya kigeni na ya ndani katika akiba.
#Tujiulize
Tumefikaje hapa tulipo hata ukaja udharura huu wa kujitakia mpaka leo tunatumia nguvu katika kujenga “artificial demand” ya sarafu ya ndani na sera hizi zitazozuia ukuaji wa uchumi mpana na wenye fanaka? Kulikoni wakati uchumi unakuwa?
#Zanzibar
Hapa ndipo tunaposema tunahitaji uwezo wa kuwa na fiscal policies zetu wenyewe ili kuwa na ile “tailored strategy” inayoendana na uhalisia wa uchumi wetu ulivyo hasa mazingira ya wingi wa watu na udogo wa ardhi yetu. Tufikiri athari za mazuwio haya yaliopoteza mapato ZRB kwa kufungwa hizi “Bureau De change” na halkadhalika athari katika ajira. Itazame kibiashara athari za ukosefu wa fedha za kigeni moja kwa moja na jee tutajikinga vipi na magendo. Kubwa zaidi ni namna gani tunafaidika na “remittances” ambazo zinaweza kuathirika na sera holela za fedha zinazolenga zaidi sehemu kubwa moja zaidi huku hii ndogo yenye hitajio la fedha za nje zaidi kujiendesha kuwa katika msukumo usio rafiki na uchumi wetu ulivyo.
No comments:
Post a Comment