Sunday 25 July 2021

MZIMU WA MAGUFULI UNAMTESA RAIS SAMIA?

 



Ukimsikiliza Ndugai wa leo sio yule wa miezi miwli nyuma kipindi Mama Samia anashika madaraka, huyu wa sasa amerejea kwenye jeuri na kejeri zilezile za utawala wa Magufuli, Anauhakika na anakokwenda. Ukimsikiliza Mwigulu wa sasa, sio yule wa mwanzo wa utawala wa Mama Samia, Mwigulu wa sasa ana jeuri, kibri na dharau iliyovuka mipaka ya siasa za Dar es Salaamu. 


Sasa mwangalie na msikilize mpiga filimbi mdini na mkabila aliyekubuhu wa utawala uliopita bwana Josephat Gwajima, huyu si kwamba anampinga tu Rais Mama Samia, Bali amevuka mipaka na kumtuhumu Rais wa nchi kwamba kahongwa pesa na Marekani ili Marekani iuze chanjo nchini. Genge la utawala uliopita wanaamini Samia ni rais wa Mpito sio rais wa "Awamu". Wanaamini rais wa mpito anakoma 2025 na kwamba mipango yao ya kuwania urais haitaharibiwa na urais wa mpito wa Samia.


Awali kabisa tulionya tukitaka Rais mpya Mama  Samia aunde serikali yake badala ya kuendeleza serikali ya mtangulizi wake ambayo ilijengwa mfumo hatari na wa kiharamia kwa miaka zaidi ya mitano  hakusikiliza ushauri wa Sukuma gang sasa chanjo ya Mzungu ndio tutakayomnyongea  sikiliza hapa chini hamana chanjo hapa.  Mfumo huo huwezi kuubomboa kwa kubadili mtu mmoja ambae ni rais tu, bali kuivunja serikali nzima na kuunda serikali mpya.


Kwakuwa siasa ya Dar es Salaam ambako kuibuka kwa nguvu na mtu na kuanguka ni jambo lisiloshangaza, Mfumo uliounda serikali iliyopita bado unanguvu kubwa sana ya kimaamuzi, Pengine lilikuwa kosa kubwa sana la karne kwa Mama Samia kuamua kuendesha nchi kwakutumia mfumo wa serikali iliyopita, Huenda ilikuwa kwa nia njema ama kosa la kimahesabu, kwasasa ni vigumu kujinasua, kinyume chake unajikuta umezungwa na ma spinning doctors  hata kama una mamlaka kikatiba lakini wenzio wanakukamata kisiasa, michezo kama blackmails ndio inayouteka utawala mpya. Kundi la wahafidhina limefanikiwa kubaki kwenye mfumo, 


Juhudi za Rais wa nchi kupambana na corona kwakufuata masharti ya Shirika la Afya dunia, sasa zinapingwa waziwazi na kundi la utawala uliopita ambalo msimamo wao juu ya janga la corona ulikuwa ni wa kijadi zaidi hali iliyopelekea watu wengi kupoteza maisha katika nchi. Kuhusu Chanjo kwa Tanzania inatakiwa serikali isimame wima itoe elimu ya haraka na ya lazima umuhimu na usalama wa chanjo husika.Kitendo cha Mchungaji Gwajima kuwaambia watu hawana haja ya kujikinga wakati shemegi yake ambae ni Waziri wa Afya anawahimiza watu kujikinga lakini Mchungaji Gwajima amethibitisha wazi wazi Kumpinga Rais na Serikali yake juu ya Chanjo ya kupambana na Corona .


Jamii iliharibiwa vibaya sana na Rais Magufuli alipotangaza hadharani kuwa chanjo ya corona haifai, Wazungu hawawapendi Watanzania na tuhuma nyingi lukuki, Leo jamii inamwamini Magufuli kuhusu chanjo, sifiriki kwamba Watz wengi watajitokeza kuchanjwa. Badala ya serikali kutangaza tu kuleteta chanjo, iingie mtaani kutoa elimu na kuhamasisha watu wakachanjwa haraka iwezekanavyo. 


Mama Samia, vita vya ndani yako ni vikubwa kuliko hivi vya nje ulivyovianzisha, Wenzio wanakusakizia upigane na wapinzani nje huku wanakumaliza ndani, Ya Joyce Banda yanakugonja. Patana na wapinzani ili ushinde vita vyako vya ndani kirahisi. Vita vya nje hutapigana na Chadema tu, utapigana na dunia nzima hata wanaofadhili bajeti yako watakupiga pia na HAUTASHINDA, wewe ni shahidi wa namna Magufuli alivyopitishwa katika magumu alipoamua kutaka kuua upinzani nchini, hakupigana na Chadema tu, alipigana na dunia nzima akaliumiza taifa na akashindwa yeye. Chadema ipo na itaendele


Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi, inakuwaje mtu kama GWAJIMA anamtuhumu RAIS @SuluhuSamia kuhongwa PESA na Marekani ili kupigia CHAPUO Chanjo ya COVIDE19? Mko busy kuhujumu vyama vya upinzani na kumbambikia kesi ya Ugaidi  @freemanmbowetz na kuacha huyu anayehatarisha usalama wa nchi?


Tatizo kubwa katika nchi hii ni kwamba sayansi inageuzwa kuwa siasa. Hakuna jamii iliyowahi kuendelea kwa kubeza sayansi na maarifa. Hakuna sababu ya kugomea chanjo huku ukiendelea kufa, lakini ieleweke kwamba chanjo zote duniani hata za watoto chini ya miaka 5 zina madhara. Kuna wengine hupata hadi vilema lakini tunaendelea kupeleka watoto clinic kwani tunaamini kwamba madhara kama yako chini ya asilimia 0.01 sio shida sana. Pili hawa vurusi  wa Covid kwamjibu wa wataalamu wamagonjwa na tiba wanasema vinabadilika- mutate. Hivyo chanjo zinaendelea kuboreshwa kadri wanavyobadilika. 


Tuheshimu sayansi na tusikilize wataalamu wanachosema na tuheshimu taalama za wenzetu, tusisikilize wanasiasa na matapeli wa kiroho aina ya Gwajima.

No comments: