Tuesday 30 June 2020

NINA IMANI NA MAALIM SEIF




Mpaka muda huu takriban masaa 30 hivi yamepita tokea Seif Sharif atangaze nia ya kugombea Urais wa Zanzibar kwa chama cha ACT Wazalendo tumeamza kusikia mayowe. Nashindwa kuelewa tatizo ni Maalim Seif, Chama chake au wafuasi wake? Binafsi napenda kuheshimu mawazo ya mtu hata kama yanapingana na mimi. Ikiwa kuna anaemini Maalim Seif amepoteza mvuto basi atumie fursa hiyo Oktoba kwa kumchagua yule ambae yeye ataamini anamvuto zaidi ya Maalim katika kupigania maslahi ya Zanzibar hili la kwanza. La pili vyama pinzani na Maalim Seif waibebe hii kama ndio hoja yao kwenye kampeni naamini kabla siku ya kura watakuwa wameshapata majibu.

Ikiwa suala ni kugombea mara nyingi nadhani ilo pia lipo kwenye mikono ya Wananchi wenyewe, hakuna ushahidi kama Maalim Seif anajiweka mwenyewe isipokuwa hupewa imani ndani ya uongozi wa chama na anapokuja kwa Wananchi nao humkubali kwa imani zao na chama pia. Kama kugombea mara nyingi ingekuwa ni kosa basi Wananchi wangilimkataa tokea kwenye hatua za kwanza,  pili wangekuwa wanamuadabisha kwa kumkataa kwenye sanduku la kura, lakini kwa nini haiwi hivyo? Anakubalika!

Matokeo yake anapewa ushindi kwa imani ya Wananchi wenyewe basi tutafute hoja nyengine hii haina mashiko. Chama cha siasa chochote mtaji wake ni watu, ikiwa chama kina watu na watu hao hao wana imani na kiongozi wao kwa sababu zilizo wazi huyo ndio kiongozi. Ccm wamechua fomu watu 32 hatuokuna mshtuko. Isipokua kituko kilichojitokeza baada ya aliyekuwa mkuu wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, bwana, Jecha kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya chama chake ndio ilikuwa habari lakini kwa wengine hali ilikuwa ya kawaida tu.

Kutangaza nia Maalim Seif Sharif Hamad mayowe yamekuwa mengi kupita kiasi hii hofu inatokea wapi? Inshaallah ifikapo Oktoba mimi nitamchagua Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wengine wa ACT Wazalendo kuanzia Udiwani, Uwakilishi na Ubunge. Matarajio yangu tutakuwa na umoja madhubuti na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema basi kwa nafasi yoyote ya kiongozi wa Chadema nitamuunga mkono.
MKULIMA KUTOKA  TUMBATU ,ZANZIBAR

No comments: