Saturday, 7 November 2009
CCM Publicity Secretary in Zanzibar Vuai Ali Vuai said that by accepting to meet President Karume, Hamad had recognised Karume Presidency?
Salma Said, Zanzibar.
MKUTANO mkubwa ulioandaliwa na Chama Cha Wananchi (CUF) jana umevunjika ghafla baada ya wananchi kukataa kumtambua Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume.
Tafrani hiyo imetokea muda mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad kupanda jukwaani na kuelezea mazungumzo ya juzi yaliofanyika Ikulu Mjini Unguja baina yake na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume.
Katibu Mkuu huyo alilazimika kuteremka jukwaani ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za Zanzibar Maalim Seif alipigwa hadharani na wanachama wake ambao walikuwa na jazba kubwa.
Maalim Seif amesema kutokana na hali ya kisiasa ilivyo tete hivi sasa hakuna haja ya kuendelea na msimamo wa kutomtambua Rais Karume hivyo uongozi wa baraza kuu umeamua kumtambua ili kuondosha matatizo yanayoweza kujitokeza siku za mbele katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao mwakani.
“Leo asubuhi tulikuwa na baraza kuu la uongozi wa CUF na tumeona kuwa kutomtambua Mheshimiwa Karume ni zaidi nadharia kuliko hali halisi kwa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kwa maana hiyo kwa maslahi ya wazanzibari baraza kuu limeamua kumtambua Mheshimiwa Karume” alisema Maalim Seif. Huku akipigiwa kelele na wananchi hatutaki.
Hata hivyo hali hiyo iliandelea huku wananchi hao wakipiga mayowe ya wakiiema “hatutaki kumtambua karume..hatutaki kumtambua karume yeye na chama chake ni waongo na wanafiki ambapo awali Maalim Seif alikuwa akiigiza maneno hayo lakini hali hiyo ilimshinda na kuwataka wanachama hao wasikilize kinachozungumzwa lakini maneno yake hayakuzaa matunda wanachama hao waliendelea na msimamo wake wa kumtaka Maalim Seif asema kuwa hatumtambui.
Kutokana na fujo na mayowe hayo ya wanachama hao Maalim Seif alifadhaika akiwa ametulia hukua kionesha kushindwa kuunyamazisha umma mkubwa uliokuja kumsikiliza lakini alilazimika kushuka jukwaani ambapo Mwenyekiti wa chama hicho, Professa Ibrahim Lipumba alipanda na kuanza kuwatulia licha ya ya hivyo naye alishindwa kwa kuwa wananchi walikataa kusikia Karume ametambuliwa.
“Maalim Seif ninamfahamu sana tokea yupo chuo kikuu na tokea ameingia katika siasa hajawahi hata siku moja kukisaliti chama nakuombeni nakuombeni tusikilizane huo sio uamuzi wa Maalim Seif huu ni uamuzi wa baraza kuu yeye hawezi kutoa maamuzi yake peke yake hana kawaida hiyo” alisema Lipumba.
Professa Lipumba alijaribu sana kuwatuliza wananchi lakini baadhi yao walitawanyika huku umati mkubwa ukiwa unamsikiliza huku wakitaka utokea kauli nyengine ya chama kwamba Karume hatambuliwi kwa madai kwamba CCM na serikali zote mbili za Muungano na Zanzibar zimekuwa zikisema uongo kwa kutaka kutimiza maslahi yao.
“Sisi tunamheshimu sana Maalim Seif na anachosema chochote tunamuamini lakini kwa hili hatutaki kumtambua Karume kwa sababu CCM na serikali zote mbili zimeshaona zitashindwa uchaguzi hapa ndio wanataka mazungumzo sisi hatutaki kumtambua Karume” alisikika wananchi hao wakisema kwa kelele.
Awali kabla ya kuvunjika kwa mkutano huo Maalim Seif alisema mkutano huo sio wa CUF bali ni wa wazanzibari na kwenda kwake Ikulu juzi ulitokana na uamuzi wa mkutano mkuu wa CUF baada ya kuona hali ya kisiasa inazidi kuwa mbaya lakini walikuwa wakijaribu kusubiri mazingira mazuri ya kisiasa ndipo yafanyike mazungumzo.
“Tulikuwa na mazungumzo na Mheshimiwa Karume naomba mnisikilize vizuri sana hii ni nchi yetu ya Zanzibar kwa zaidi ya karne imekuwa katika misukosuko na huku nyuma wazee wetu wanatwambia walikuwa walikuwa wakiishi vizuri lakini sasa tumekuwa tunaishi roho juu hasa kukikaribia chaguzi” alisema Maalim Seif huku wananchi wakiwa kimya sana.
Alisema baada ya kurejeshwa mfumo wa vyama vingi huko nyuma kulikuwa na mivutano hadi watu kuuawa na kila kukikaribia uchaguzi watu wanakufa, watu wanaumia na enzi zile za siasa za 1961 watu 68 waliuawa na kutokea ghasia na kukafanyika uchaguzi ambao haukuleta matokeo mazuri na jambo ambalo lilisababisha watu kadhaa kupoteza maisha na vitu kuharibiwa.
Alisema kwamba licha ya juhudi za hapa na pale na mataifa ya nje kuingilia hali hiyo haijatengemaa hasa kwa kuwa mazungumzo hayo yote huwa yanafanywa na watu wan je lakini watu wa ndani huwa hawashirikishi bali huambiwa tu lakini sasa watu wenywe wameamua kukaa pamoja na kujadiliana kuweka hali ya usalama nchini.
“Baada ya kuona haya yaliotokea yameshatokea na juzi tulipokutana ikulu tumeulizana hali hii itaendelea hadi lini kuuawa wenyewe kwa wenyewe kudhuriana kwani tumeshapigana vya kutosha tumeshagombana vya kutosha lakini sasa tumesema basi tunataka kuijenga nchi yetu kwa pamoja” alisema Maalim Seif.
Akizungumzia suala hilo Maalim Seif alisema kwa kuogopa dhima mbele ya Mwenyeenzi Mungu wameamua kukaa pamoja na kuleta suluhu ya kudumu hapa Zanzibar kwa kuwa wananchi wamekuwa wakiumia kila ifikapo uchaguzi wamekuwa wakipigwa na kuonewa bila ya kiasi.
“Sisi viongozi wenu mimi na mheshimiwa karume tumekaa na kukubaliana kwamba hali hii itaendelea mpaka lini jamani? tumeona tunadhani njia tunayopita siyo tumeona kwamba tunadhima kubwa mbele ya Mwenyeenzi Mungu na tutakuja kuulizwa kwa kuwaadhibu wazanzibari” alisema Maalim Seif huku akipigiwa makofi kabla kauli iliyowaparaganya wananchi hao haijatolewa.
Hata hivyo alisema hakuna kitu kisichowezekana hasa kwa kuwa kauli za viongozi wa CCM bara walikwishasema suala hilo linaweza kumalizwa na wenyewe wananzibari hivyo hakuna haja ya kuendelea na malumbano yasiokuwa na tija kwa jamii na kuwataka watu wote kukubaliana kukaa pamoja na kuijenga nchi yao.
Juzi Maalim Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume walikutana Ikulu Mjini Zanzibar kwa lengo la kusahau tofauti zao za kisiasa na kujenga mahusiano mema kwa maslahi ya wananchi wote wa Visiwa vya Unguja na Pemba.
Katika mazungumzo hayo ambayo yalichukua takribani sasa mbili wawili hao yaligusia mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na haja ya kudumisha amani na utulivu nchini na maelewano na mashirikiano kati ya wananchi wote.
Viongozi hao wamezingatia haja ya kuzika tofauti zilizopo ambazo zinachangia kuwatenganisha Wazanzibari na kutoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa jumla kushirikiana katika kujenga nchi bila ya kujali itikadi zao za kisiasa.
Viongozi hao walifafanua kuwa wananchi wakishirikiana na kujenga nchi kwa pamoja, watapiga hatua kubwa zaidi za maendeleo.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walihusisha umuhimu wa mchakato wa mazungumzo endelevu baina yao na vyama vyao kwa jumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment