Saturday, 7 November 2009
HAMAD MEET PRESIDENT KARUME
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Amani Abeid Karume leo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad huko Ikulu, Mjini Zanzibar.Katika mazungumzo hayo, ambayo hayakutarajiwa na wengi wawili hao yaligusia mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na haja ya kudumisha amani na utulivu nchini na maelewano na mashirikiano kati ya wananchi wote.
Viongozi hao wamezingatia haja ya kuzika tofauti zilizopo ambazo zinachangia kuwatenganisha Wazanzibari na kutoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa jumla kushirikiana katika kujenga nchi bila ya kujali itikadi zao za kisiasa.
Viongozi hao walifafanua kuwa wananchi wakishirikiana na kujenga nchi kwa pamoja, watapiga hatua kubwa zaidi za maendeleo.Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walihusisha umuhimu wa mchakato wa mazungumzo endelevu baina yao na vyama vyao kwa jumla.
habari 2:
Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar amekutana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad na kuzungumzia mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar.
Viongozi hao ni mara ya kwanza kukutana Ikulu kuzungumzia hali ya Kisiasa ya Zanzibar tangu kukwama kwa mazungumzo ya kujadili kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani hapa.
Taarifa iliyopatikana baada ya mazungumzo hayo, imesema kwamba mazungumzo ya viongozi hao yamepata mafanikio makubwa hasa kuhusiana na suala la kuzingatia umoja na mshikamano kwa wananchi wa Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kitengo cha habari cha Ikulu ilieleza jana kwamba mazungumzo hayo yalizingatia suala la kudumisha amani na utulivu pamoja na kujenga ushirikiano miongoni mwa wananchi.
Aidha viongozi hao wamezingatia suala la kuzika tofauti zilizopo zikiwemo za kisiasa ili kuharakisha maendeleo ya Zanzibar na kujenga umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Zanzibar.
Maalim Seif na Karume katika taarifa hiyo wamesema wananchi wa Zanzibar iwapo watachukua hatua za kushirikiana, Zanzibar itapiga hatua kubwa ya maendeleo na kuwataka kuachana na tofauti za kisiasa ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Viongozi hao wamekubaliana kwamba ipo haja ya mazungumzo hayo kuwa endelevu baina ya vyama vya CCM na CUF ili kuhakikisha tofauti za kisiasa zinazikwa na kufungua ukurasa mpya wa kujenga nchi kwa maslahi ya wananchi wake.
Hatua ya viongozi hao kukutana inafungua matarajio mapya ya kumaliza mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar baada ya vyama vya CCM na CUF kushindwa kupata mwafaka.
Majadiliano ya mwafaka baina ya CUF na CCM yaliparaganyika kufuatia vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM kuagiza kwamba mapendekezo ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa lazima yapigiwe kura ya maoni na wananchi kabla ya kufikia utekelezaji wake.
Aidha viongozi hao wamekutana huku wafuasi wa CUF wakiwa katika mgomo wa kujitokeza katika zoezi la uandikishaji wa dafatari la kudumu la wapiga kura kwa madai kwamba kuna idadi kubwa ya watu wamenyimwa vitambulisho vya Uzanzibari Mkaazi.
Kadhalika mazungumzo hayo yamekuja ikiwa ni wiki moja tangu Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amalize ziara ya kutembelea nchi za Ulaya na kurejea kimya kimya kwani hadi sasa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu ziara yake hiyo.
Naye Kiongozi mwandamaizi wa CUF, Ismaili Jusa, alithibitisha viongozi hao kukutana lakini hakuwa tayari kuzungumzia ajenda zilizotawala katika mazungumzo hayo.
“Tumekubaliana Ikulu ndio watoe taarifa. Mimi sina cha kuzungumza zaidi ya kile kilichoelezwa isipokuwa tumeangalia hali ya kisiasa zaidi katika nchi yetu,” alisema Jusa ambae ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CUF.
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, hali ya kisiasa ya Zanzibar imekuwa ikizorota hasa kila baada ya kufanyika uchaguzi kutokana na chama cha CUF kupinga matokeo ya uchaguzi kwa madai ya kutokuwa huru na wa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment