Wednesday, 22 January 2014

KIEMBE SAMAKI KUMEKUCHAKura ya Maoni Visiwani Zanzibar itaanzia Jimbo la Kiembe samaki baina ya wanaotaka serkali mbili au tatu Mukumbuke tu asilimia 66% ya Wazanzibari wameukataa muundoa wanoupigania CCM wa serkali Mbili Matoeko ya Kiembesamaki hayawezi kui represent Zanzibar ila tutapata kuona mwanga wa Kura ya maoni itakayofuatia kujua vipi Zanzibar madai yake na muafaka wa mazungumzo ya siri Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ndio alieshika mpini wa maamuzi ya Muundo wa muungano ,Mkutano wa  Maalim Seif na Rais Kikwete bado  ni siri bado iliofichwa kapuni  imegeuka sirikali juu ya muundo wa Muungano siri hii inaonekana inawakera wahafidhina wa CCM Zanzibar.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM na Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtambulisha Mgombea wa CCM katika uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Nd Mahmoud Thabit Kombo katika viwanja vya kiembesamaki michungwani Zanzibar.  
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia Wanachama wa CCM wa Jimbo la Kiembesamaki katika Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo, unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao uzinduzi huo umefanyika katika uwanja wa mpira kiembesamaki michungwani.
 Mgombea Uwakilishi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Bwa, Mahmoud Thabit Kombo, akiwaonesha Vitabu vya Ilani ya Uchaguzi wa CCM baada ya kukabidhiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo zilizozinduliwa katika viwanja vya mpira kiembesamaki.  
Mgombea wa CCM  Bwa. Mahmoud Thabit Kombo akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM katika viwanja vya mpira kiembesamaki.

 Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea wao wakati akimwaga Sera za Chama chake katika mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar.
 Mgombea wa CCM Bwa. Mahmoud Thabit Kombo akiwahutubia Wapiga kura wake katika mkutano wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira kiembesamaki Zanzibar.
Mwakilishi Kijana wa Jimbo la Bububu Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) akiwa jukwaani kumnadi Mgombea wa CCM jimbo la Kiembesamaki Bwa. Mahmoud Thabt Kombo.
 Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Waride Bakari Jabu, akimnadi Mgombea wa Nafasi ya Uwakilishi katika viwanja vya Mpira kiembesamaki katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vaia Ali Vuai, akihutubia katika mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki baada ya Mwakilishi wake kupitia CCM kuvuliwa Unanachama na nafasi hiyo kuwa wazi bila ya mwakilishi .
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Yussuf Mohammed akihutubia katika mkutano huo wa kampeni ya  Uchanguzi mdogo wa jimbo la kiembesamaki. 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mohammed Seif Khatib, akiwahutubia Wanachama wa CCM na kuwahamashisha kumpigia kura mgombea wa CCM, Bwa. Mahmoud Thabit Kombo.
Viongozi wa Meza Kuu wakiwa katika viwanja vya Uzinduzi wa Kampeni ya Chama cha Mapinduzi katika viwanja vya mpira kiembesamaki.
Wanachama wa CCM wakimshaniria Mgombea wao wakati akitambulisha katika mkutano wa Uzinduzi wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira kiembesamaki Zanzibar.
Viongozi wa CCM na Wabunge wakiwa katika viwanja vya Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni wa Jimbola Kiembesamaki.
Wanachama wa CCM wakichukua picha kupitia simu zao kwa ajili ya kumbukumbu ya Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki kupitia Chama cha  CCM. No comments: