Thursday 27 February 2014

MTIKILA AWA KIVUTIO BUNGE LA KATIBA

WENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amekuwa burudani ya aina yake katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kutokana na misimamo na misemo yake wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Mtikila hukusanya idadi kubwa ya waandishi kila anapozungumza huku baadhi ya wanasiasa na wajumbe wengine wa Bunge la Katiba wakimshangaa.
Jumatatu iliyopita, Mtikila alishangaza alipodai kwamba Baba wa Taifa, hayati  Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, hayati mzee Abeid Amani Karume hawakuziunganisha Zanzibar na Tanganyika, bali kitendo hicho kilifanywa na majasusi wa CIA wa Marekani, kwa ajili ya kuhofia hali ya usalama wakati ule wa vita baridi kati ya Mataifa ya Magharibi na iliyokuwa dola ya Urusi, USSR.
“CIA hawakutaka…

No comments: