Sunday 2 March 2014

CCM ZANZIBAR YAPASUKA DODOMA


Jana niliwamabia moto utawaka kweli umewaka wazi wazi  imekuaje mapendekezo yaliopelekwa Feb 5th 2013 yawe leo ndio Kitimoto kwa Wahafidhina wa Zanzibar ?
CCM inaanza kupasuka vipande vipande. Wanafik na Wasaliti wa Zanzibar, Salmin Awadh na Asha Bakari wamefanya press conference leo na wamemkanusha na kumtukana Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Ameri Kificho kwa mapendekezo waloyapeleka Tume ya Katiba walioafaikiana vyama hivyo viwili huko Zanzibar.Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wawakilishi walioandaa na kupitisha waraka wa maoni ya Baraza la Wawakilishi yaliyowasilishwa mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo yalipendekeza kuwepo kwa mamlaka huru ya Zanzibar, mamlaka huru ya Tanganyika na mamlaka ya Muungano kwa ajili ya kushughulikia mambo ya Muungano ina wajumbe 13 wa CCM na CUF ni 3 tu.


Wasaliti wa Zanzibar, Salmin Awadh, Shamsi Vuai Nahodh na Asha Bakari wamefanya press conference leo na wamemkanusha na kumtukana sana Kificho kwa mapendekezo waloyapeleka Tume ya Katiba.Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wawakilishi walioandaa na kupitisha waraka wa maoni ya Baraza la Wawakilishi yaliyowasilishwa mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo yalipendekeza kuwepo kwa mamlaka huru ya Zanzibar, mamlaka huru ya Tanganyika na mamlaka ya Muungano kwa ajili ya kushughulikia mambo ya Muungano ina wajumbe 13 wa CCM na CUF ni 3 tu. Leo wale Matapishi yao !Jana asubuhi, zaidi ya wajumbe 10 wa Baraza la Wawakilishi akiwamo Shamhuna, Nahodha na Ali waliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma na kumtupia lawama Kificho wakisema; “Amewasaliti katika mchakato huo wa Katiba.”Akizungumza katika mkutano huo, Mnadhimu wa BWZ ambaye pia ni Katibu wa Wawakilishi wa CCM, Salmin Awadh Salmin alisema katika uwasilishaji wa maoni ya taasisi hiyo katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Baraza la Wawakilishi halikutumia fursa hiyo ipasavyo.“Ni viongozi wachache tu waliobeba jukumu hili kubwa na zito bila kuwashirikisha wajumbe walio wengi. Sisi wawakilishi tunashukuru kwa taasisi yetu hii kupatiwa heshima kubwa ya kutoa maoni yetu ingawa utekelezaji wake haukuendana na malengo tuliyokusudia.Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho amekiri kuwasilisha waraka kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba na kupendekeza Zanzibar na Tanganyika kuwa na mamlaka huru, hatua ambayo imezua malalamiko miongoni mwa makada wa chama hicho ambao wamesema huo ni usaliti.Akizungumza kwa simu kutoka Dodoma, Kificho ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), alisema kimsingi waraka huo ulilenga kuipa nguvu Zanzibar kushughulikia mambo yasiyo ya Muungano ili kujiimarisha kiuchumi.Kauli ya Kificho inakuja wakati baadhi ya wajumbe wa CCM kutoka Zanzibar wakiitisha mkutano na kutoa tamko la kumshutumu kwa kutoa mapendekezo hayo, wakisema ni kinyume na msimamo wa chama hicho.Kificho alionyesha kushangazwa na madai kuwa mapendekezo hayo yaliyoandaliwa na watu wanne ambayo ameyasaini si msimamo wa BLW.“Tatizo lililopo ni tafsiri ya kila mmoja anapousoma waraka huo, hakuna sehemu tuliyoandika tunataka Serikali tatu, mamlaka huru maana yake kila upande uwe na uwezo wa kushughulikia mambo yake yasiyo ya Muungano na kujijenga kiuchumi, ikiwa ni pamoja Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu ya Kimataifa (OIC) na siyo kuunda dola,” alifafanua Spika Kificho.Alisisitiza kuwa angependa mambo ambayo hayamo katika orodha ya Muungano yaendeshwe na Zanzibar bila ya kuwekewa vikwazo mahali popote.Madai hayo ni dalili za wazi za mgawanyiko baina ya wajumbe wa CCM ambao wameanza kuonyesha makundi mawili yenye misimamo tofauti.

Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wawakilishi ni:- 1. Pandu Ameir Kificho - Spika - CCM. 2. Ali Abdalla Ali - Naibu Spika - CCM. 3. Balozi Seif Ali Iddi - CCM. 4. Mohamed Aboud Mohamed - CCM. 5. Omar Yussuf Mzee - CCM. 6. Abubakar Khamis Bakary - CUF. 7. Salmin Awadh Salmin - CCM. 8. Abdalla Juma Abdalla - CUF. 9. Mahmoud Mohamed Mussa - CCM. 10. Mgeni Hassan Juma - CCM. 11. Hamza Hassan Juma - CCM. 12. Asha Bakari Makame - CCM. 13. Makame Mshimba Mbarouk - CCM. 14. Amina Iddi Mbarouk - CCM. 15. Omar Ali Shehe - CUF

BARAZA LA WAWAKILISI LA ZANZIBAR : MAONI YA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR JUU YA KATIBA MPYA 1.0 Utangulizi Kwa niaba ya Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar naomba kuchukua nafasi ya kuipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania kwa umakini mkubwa inayochukua katika kupata maoni thabiti ya wananchi kuhusiana na Katiba wanayoitaka. Pia naishukuru sana Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutupa nafasi Baraza la Wawakilishi, kama taasis, kutoa maoni yake kuhusiana na Katiba inayofaa itumike kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Badala ya Katiba iliopo sasa. Baraza la Wakilishi limekuwa linafatilia kwa makini utoaji wa maoni ya wananchi mmoja mmoja na vikundi kuhusiana na Katiba inayohitajika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya kutafakari, katika kikao cha Wajumbe wote na katika vikao mbali mbali vya Kamati yake ya Uongozi, na kuona hali halisi ya maoni inavyoendelea na ufanisi mkubwa unaopatikana, Baraza la Wawakilishi linaamini kuwa maoni yaliyotolewa tayari yameweka wazi yale mambo muhimu ambayo wanachi wanapenda yazingatiwe katika kupata Katiba mpya. Na kwa kuzingatia pia kuwa, katika hatua iliyopo sasa ya maoni ya wananchi ambapo hayajalolewa mwelekeo wake rasmi ni vigumu sana kwa Wajumbe wa Baraza kufikia makubaliano ya maoni ya Baraza kikamilifu (detailed opinion) hata kwa yale mambo ambayo kwa ujumla wake Wajumbe wa Baraza wanakubaliana kwa pamoja. Kutokana na ukweli huo, Wajumbe wa Baraza wameeonyesha mwelekeo wao wa kijumla juu ya mambo wanayoamini kuwa yanahitajika kuingia kwenye Katiba mpya ya Jamhuri nya Muungano wa Tanzania. Mambo ya msingi ambayo Wajumbe wa Baraza kwa ujumla wameyaona na kuitaka Kamati yao ya Uongozi kuyawasilisha kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni kama yanavyoelezwa hapa chini. 2.0 Maoni Yenyewe Baraza la Wawakilishi la Zanzibar linaamini kuwa suala la namna ambavyo Katiba mpya ya Tanzania inapaswa iwe litajitokeza wazi wazi zaidi katika maoni ya wananchi. Kwa upande wake Baraza la Wawakilishi, kama Taasisi ya kuwawakilisha wananchi, linajitayarisha kusimamia zaidi juu ya mambo ya msingi ambayo Wanzibari na Watanzania walio wengi wameonyesha umuhimu wa kuingizwa kwenye Katiba ijayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, Baraza la Wawakilishi lenyewe limeangalia baadhi ya mambo ambayo linahisi ni muhimu ambayo kama Wanazibari wangependa yawe ni misngi muhimu ya kikatiba katika Katiba ijayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mambo yenyewe ni haya yafuatayo: 2.1 Misingi ya Muungano na Utaifa Kwa sababu Wazanzibari ni waumini wa Muungano haukuondoa na hautoondoa uwepo wa Zanzibar kama nchi, ni vyema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ijayo iweke wazi kuwa Tanzania ni Jamhuri ya Muungano inayotokana na Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Hali hii itahakikisha kuwepo na maeneo maalum ya mamlaka ambayo Zanzibar ina uwezo nayo kama nchi (yaani, Mamlaka ya Dola ya Zanzibar). 2.2 Mgawanyo wa Mamlaka za Muungano Kwa sababu inapendekezwa kuwepo na Mamlaka ya Zanzbar huru na Mamlaka ya Tanganyika huru ndani ya Jamhuri ya Muungano, Mamlaka ya Muungano iwekwe wazi – maeneo yake, uwezo au nguvu zake, na utendaji wake. Mambo yote hayo yawekewe wazi na mipaka yake. 2.3 Usawa wa Ushirikishwaji katika Mamlaka ya Muungano Uwepo wa Muungano uonekane katika hali zote – uundwaji wa Mamlaka za Muungano, ufanyaji kazi katika Mamlaka za Muungano, ufanyaji wa maamuzi katika Mamlaka za Muungano, na uingizwaji na upunguzwaji katika orodha wa mambo ya Muungano. Kwa mfano, maamrisho kama yale yaliyopo sasa kwenye Ibara ya 64(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, ambayo yanawezesha jambo kufanywa la Muungano bila ya kuishirikisha katika maamuzi Mamlaka ya Zanzibar, yasiwe na nafasi tena ya kutokea kwa mujibu wa Katiba ijayo ya Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika ushirikishwaji, Katiba itamke wazi kuwa uwepo uwiyano ulio wazi wa viongozi na watendaji katika utumishi wa Mamlaka za Muungano. Yaani, kwa mfano, endapo Rais wa Muungano anatoka upande mmoja wa Muungano, Makamo wa Rais atoke upande mwengine. Mamlaka ya viongozi wakuu wa Muungano yawekwe bayana ndani ya Katiba; na uwepo utaratibu wa kubadilishaji nafasi hizo kwa pande mbili za Muungano. Yaani, upande unaotoa Rais kwa kipindi fulani, uje kutoa Makamo wa Rais kwa kipindi kingine, na kadhalika. 2.4 Mfumo wa Kutunga Sera na Sheria za Muungano Utungaji wa sera na sheria za Muungano isiwe ni jambo la kuzingatiwa na kutekelezwa na Mamlaka za Muungano pekee. Kama tulivyoelezea hapo awali kuwa uwepo ushirikishwaji wa sehemu (Dola) mbili huru katika kufanya maamuzi na uendeshaji wa Mamlaka ya Muungano. Ushirikishwaji huo ni lazima udhihirike katika maamuzi yatakayopelekea kuundwa kwa sera na sheria zote za mambo ya Muungano. 2.5 Umiliki wa Rasilimali za Muungano Rasilimali za Muungano iwe ni milki ya pande mbili za Muungano; na rasilimali hizo ndio zitumike katika uendeshaji wa Mamlaka za Muungano. Ugawaji wa rasilimali ufanye kwa u

No comments: