Tuesday, 28 July 2015

ALIVYOKARIBISHWA LOWASSA NA VIONGOZI WA UKAWA


Edward Lowassa (Kushoto) akiteta jambo na Profesa ibrahim Lipumba (Kulia) katika Mkutano uliofanyika katika hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam Lowassa ametangaza uamuzi huo leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar na kusema amekubali mwaliko wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Amesema kuwa CCM haikumtendea haki katika kupitisha majina ya wagombea urais hivyo hawezi kuendelea kubaki kwenye chama hicho ‘’ Niliwekewa mizengwe kuhakikisha Jina langu halifiki Kamati Kuu na Halmashauri Kuu’’.
Edward Lowassa (Kushoto) akiteta jambo na
Waziri Mkuu huyo wa zamani ameeleza kuwa nia yake ni kuleta mabadiliko hivyo kujiunga na Chadema ni kuendeleza nia yake ya kuwatumikia Watanzania ‘’ CCM Si baba yangu wala Mama yangu, Watanzania kama wameyakosa mabadiliko ndani ya CCM, basi watayapata nje ya CCM’’
Aidha ameongeza kuwa hajakurupuka kufanya uamuzi huo na kuendelea kubaki ndani ya CCM itakuwa ni unafiki ‘’ Sijakurupuka kwa uamuzi huu hivyo basi kuanzia leo natangaza rasmi kuondoka CCM na kujiunga na UKAWA kupitia Chadema’’ alisema Lowassa. Hata hivyo muda mfupi baada ya kutangaza uamuzi huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimkabidhi Lowassa kadi ya uwanachama


No comments: