Thursday, 6 March 2014

MKATABA WA MUUNAGNO UKO WAPI ?

Inafurahisha Bunge la katiba linataka kumtoa paka aliefichwa kwenye gunia , Kuna Mzanzibari mmoja alikwenda Mahakamani kudai kuona Mkataba wa Muungano na tuhuma zilizoeena ZNZ ni kuwa Mkataba huo haupo.Pale alipohojiwa Rais Karume na kusema yeye alipokua Ikulu ya Zanzibar hakuwahi kuuona na alipohojiwa DR Shein alikuja na Ukali na kusema kuwa yeye anao Waraka huu huko Ikulu Zanzibar . Sese Siri hii huenda Bunge la Katiba likamtoa Paka kwneye Gunia sikiliza Video hii .

Dodoma. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imekataa pendekezo la Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM) aliyetaka Hati ya Muungano iendelee kuwa siri na kuweka bayana kuwa nyaraka hiyo iko wazi kwa mtu yoyote.Msimamo huo ulitolewa juzi katika Bunge Maalumu la Katiba na Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Othman Masoud Othman wakati akitoa ufafanuzi kuhusu hoja hiyo ya Ole Sendeka, ambayo ilisababisha minong’ono miongoni mwa wajumbe.Othman alisema Hati ya Muungano iliridhiwa na kupitishwa katika sheria ya kuridhia Muungano wa nchi za Tanganyika na Zanzibar hivyo nyaraka hiyo ni ya umma. “Katika sheria tunasema kwamba hati za namna hiyo ni `judiciary notice’ (hati ya kimahakama). Yaani ni vitu ambavyo ni ‘public document’ (nyaraka ya wazi kwa umma),” alisema Othman huku wajumbe wakilipuka kwa vicheko na makofi.Othman alisema Ole Sendeka anaweza kuwa na hoja kama atakuwa anazungumzia hati nyingine ya Muungano.“Wajumbe wa bunge hili hawahitaji kusubiri waletewe nyaraka hiyo, wanaweza kufanya juhudi zao kuipata,” aliongeza Othman.Mapema Ole Sendeka alitoa tahadhari ya Hati ya Muungano kuwa ni siri wakati akichangia marekebisho ya kanuni ya nne inayohusu haki na kinga ya Bunge Maalumu la Katiba baada ya mjumbe mwingine, John Mnyika kuwasilisha marekebisho binafsi akitaka wajumbe wawe na haki ya kupatiwa nyaraka muhimu. endelea hapa kujikumbusha moto wa Muungano. http://www.raiamwema.co.tz/vurugu-za-uamsho-zanzibar%C2%A0je-tutangaze-kuchafuka-hewa-kisiasa

No comments: