Tuesday 4 March 2014

UCHAGUZI MDOGO CCM NA CHADEMA JINO KWA JINO !


Uchaguzi uliopita na Vipi CCM waliweza kushinda na vipi Chadema watashusha asilimia ya CCM kabla ya 2015

WILAYA YA IRINGA
KALENGA
Candidate
Political Party
Number of Votes
Percentage Votes
MGIMWA WILLIAM AUGUSTAO
CCM
31,42184.39
REHEMA MAKOGA MORINE PAULO
CHADEMA
3,3569.01
KATINDASA JOHN LUMULIKO
TLP
9342.51
MAKUKE ISMAIL MJINJA
JAHAZI ASILIA
3320.89
SPOILT VOTES1,1913.2
TOTALS37,234100

PICHA: CHADEMA KALENGA KAMPENI NYUMBA KWA NYUMBA, YATEMBELEA JAMII YA KIMASAI
Juu na chino Meneja Kampeni wa Chama cha Deokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Alphonse Mawazo, akicheza ngoma ya jamii ya kimasai baada ya kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Grace Tendega Mvanda, jana asubuhi.


Mzee wa Mila wa Kimasai katika Kijiji cha Mfyome, Lioper Ilmuduji, akimpatia baraka mgombea ubunge wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Bi. Grace Tendega Mvanda, wakati chama hicho kilipofanya kampeni ya nyumba kwa nyuma kuomba kura kwa wananchi katika kijiji hicho jana asubuhi. Mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Bi. Grace Tendega Mvanda akishiriki chakula cha kimila pamoja na watu wa jamii ya kimasai katika Kijiji cha Mfyome jana asubuhi baada ya msafara wa mgombea huyo kufika kijijini hapo kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba.

No comments: