Sunday, 27 April 2014

POLITICS OF THE BELLY AU MCHUMIA TUMBO

Leo nitwakumbushia vijana wetu wengi wanaoingia kwenye siasa  kuwa Siasa sio Lele mama , kwani ukiiingia kwenye siasa na ukiwa na njaa utageuka kuwa ni historia ya Mchumia tumbo na unakua ndio Mwisho wako mifano hii hapa chini.
Leo nitaanza na List ya Wachumia tumbo , Nianze mwaka 1995 na Mwanasheria  Mchachari Masumbuko Lamwai. Mkoa wa Dar es Salaam hautamsahau aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakili Dk. Masumbuko Lamwai. Aliisumbua sana CCM na wala haikushangaza aliposhinda ubunge katika Jimbo la Ubungo kupitia NCCR.Lakini naye alirudi CCM ambako alipewa ubunge wa kuteuliwa; akawa miongoni mwa wanasiasa wapiga debe wa mwanzo kupendekeza katiba irekebishwe ili Rais Benjamin Mkapa aongezewe kipindi. Tuiteje huo? amekua ni mchumia Tumbo alijimaliza kisiasa.Ni Mwanasiasa alieitia hofu CCM na Kufikiriwa Lamwai atakua na Uwezo wa kuiondoa CCM madarakani lakini CCM walimuondoa yeye kwenye ulingo wa siasa.

'Uchaguzi uliopita kwa mara ya Kwanza kwa upande wa Zanzibar tuliona Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mwaka 2010 Fatma Magimbi na yeye kugeuzwa Mchumia tumbo.
Dr Aman Kaborou kutoka Kigoma amekua pia Mchumia tumbo pia na kusahaulika kisiasa.Ningependa kujuzwa alipo huyu bwana mkubwa aliyekuwa mwiba wa CCM akiwa CHADEMA na hatimaye kuhamia CCM.


'
Mwaka wa 2014 kuna wengine wanaingizwa kwenye kundi hili bila kujijua Hamad Rashid Wapemba wanasema ni KUSHNE. Baada ya kusoma article ya leo kwenye Gazeti la Nipashe juu Msiamao wa Hamad Rashid juu ya msiamao wake juu ya Muungano nimemaini na yeye system ishamuingiza kwenye kapu la Wachumia tumbo.
KUNA watu walifanyiwa mizengwe, fitina, hila ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kuna watu ambao mchango wao wa uongozi ndani ya chama hicho haukuthaminiwa.Walibinywa wasisikike na walipoonyesha msimamo waliondolewa na wengine walijiondoa kwa hiari yao na kujenga nguvu ya mageuzi. Wengine walijiondoa katika kipindi kama  cha kura za maoni ndani ya CCM kama Dk Willibrod Slaa.
Walijiondoa CCM wakiwa na msimamo wa kupinga mizengwe, rushwa, upendeleo na zaidi ufisadi ndani na nje ya chama, walidharauliwa na walionekana watu wasioitakia mema nchi.
Lakini baada ya miaka mingi ya kuhangaika walipojitoa CCM, sasa kina Maalim Seif Shariff Hamad, Prof. Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe, Dk. Slaa, Mabere Marando wamejenga upinzani na wanaheshimika katika jamii.
Huko ndiko alikoelekea Fred Mpendazoe aliyejiengua CCM na kujiunga na CCJ kabla ya kuhamia CHADEMA—kuungana na wana mageuzi na aliweza kufuatwa na wanachama safi wa CCM waliokatishwa tamaa na hali ya sasa.Huo ndio msimu wa watu makini kukitosa chama hicho ambacho wenye nacho ndio pekee wanathaminiwa na kupitisha maamuzi nani awe mbunge au diwani na nani asiwe.Huo ndio msimu wa wabunge wote maarufu ndani ya CCM waliotemwa kwa mizengwe, kutafuta sehemu ya kupumulia ili wafanikishe malengo yao.Ieleweke kwamba mradi wa mwanasiasa ni ubunge au udiwani au nafasi yoyote ya uongozi ili atimize ndoto zake. Akikosa katika chama kimoja hasa kutokana na mizengwe, fitina, hila nk atahamia kingine.
Tahadhari
Uzoefu unaonyesha kuwa si wote wanaohamia kambi ya upinzani huwa na lengo la kuimarisha siasa za upande huu. Baadhi hugeuka kuwa wasaliti au baadhi hutuma kudhoofisha upinzani—huu ni wakati wa kuwa macho na wasio na malengo, wasio na tija na wasaliti.Baadhi watajiunga na upinzani kutokana na hasira tu. Hawa ni wengi na mifano ipo.Mwanasiasa machachari katika miaka ya mwanzoni mwa 1990, Njelu Kasaka, alitibuana na wenzake katika kipindi kama hiki mwaka 2005, alipotaka kutetea kiti cha ubunge wa Jimbo la Lupa mwaka 2005, kwa hasira alihamia Chama cha Wananchi (CUF).Kasaka akafanya kazi kubwa ya kuomba wananchi wainyime kura CCM lakini wakampuuza, wakampa ulaji Victor Mwambalaswa. Kwa kuwa hakuwa na nia ya dhati ya kuimarisha mageuzi akasaliti kambi akarudi CCM.
Mwenyekiti wa taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM, John Guninita, alivurugwa kwenye umoja huo na kwa vile CHADEMA walikuwa kwenye chati, akahamia, lakini hakuwa na malengo hivyo hakuwa na tija akarudi na kupewa uenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es alaam.Upinzani ulifurahia kumnasa Richard ‘Tambwe’ Hiza, ambaye alivuma zaidi alipokuwa NCCR-Mageuzi. Mradi wake ulikuwa kuwa kiongozi na alipokosa nafasi alichanja mbuga.Tambwe alikuwa maarufu wilayani Temeke. Umaarufu huo ulimpandisha mabega, na alipoteuliwa kugombea ubunge mwaka 1995 alifikiri kuwa angeshinda kwa kishindo.
Tambwe aliangukia pua. Aliyeibuka mshindi alikuwa Ramadhani Kihiyo wa CCM. NCCR wakaenda kortini kupinga uchaguzi huo na katikati ya kesi hiyo, Kihiyo ‘akabwaga manyanga’ mwaka 1996 kwa madai afya yake haimruhusu kuendelea na ubunge (hata hivyo kesi iliendelea hukumu ya mahakama ikatolewa kwamba hastahili).
Mazingira ya kesi yalikuwa magumu, alibanwa vilivyo mahakamani kiasi kwamba majibu aliyokuwa anatoa yalitia shaka na ili ‘kukubali yaishe’ akajiuzulu. Kesi hiyo ndiyo chimbuko la msamiati ‘kihiyo’ – yaani asiyejua, mbumbumbu katika Kiswahili..
Baada ya Kihiyo kuondolewa, uliandaliwa uchaguzi mdogo kujaza nafasi hiyo. Uchaguzi huo ulimpa Tambwe tiketi ya kurudi CUF.
Kisa? Alichukizwa na hatua ya aliyekuwa mwenyekiti wake, Augutine Lyatonga Mrema kuwania kiti hicho badala yake. Tambwe alimwona Mrema kuwa “ana uchu” wa madaraka.
Viongozi wa CUF nao waliingia mkenge kuamini kwamba Tambwe alikuwa maarufu katika eneo hilo na angeweza kushinda uchaguzi mdogo kuchukua nafasi ya Kihiyo. Haikuwa hivyo. Mrema akashinda.
CUF hawakujifunza kwa matokeo ya 1996; wakampa tena nafasi mwaka 2000. Hapo alirusha ‘mawe ya kisiasa’ akaumiza wapinzani wake hasa mgombea wa CCM, Khadija Kusaga.Hata hivyo, mawe hayo ya kisiasa hayakumzuia Khadija kuibuka mshindi. Baada ya kushindwa tena mwaka 2005, akaondolewa kwenye cheo chake cha Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Sera wa CUF na kubaki kuwa mwanachama tu.Kwa kuwa hakuwa anaamini katika mageuzi kama Kuchilingulo Maole, hiyo ikawa tiketi ya kupanda mkweche wa CCM akitaka umvushe salama kuelekea bungeni. Huko akapewa kazi ya kupiga debe kando ya katibu mkuu Yussuf Makamba.
Kazi ya kwanza aliyofanya Tambwe ni kwenda Kata ya 14 Temeke, kama mwana mpotevu, kuomba radhi kwa kile alichokiita kosa la kuwarushia mawe mazito ya kisiasa ambayo yaliwajeruhi ‘wenye hatimiliki’ ya chama.Kazi ya pili, kwa hasira za kisiasa, alianza kuvinanga vyama vya upinzani, na kueleza uzuri wa chama alichokiponda kwa miaka 10, CCM.
Hapo Tambwe alidhani amejisafisha akatakata vizuri hivyo akataka wamuamini. Wewe! Alipoomba nafasi ya halmashauri kuu ya CCM mwaka 2007, kura zake hazikutosha tena, na safari hii alipoomba kuteuliwa kugombea ubunge, ameangukia pua.
Kwa hiyo, wachambuzi wanapotazama safari Mpendazoe, wajue anatafuta mahali ambapo kura zitatosha kukamilisha mradi wake wa kurudi kuungana na mitume 12 iliyojitoa kwa nguvu zao zote kupinga ufisadi bungeni.
Upinzani lazima uwe makini kwani unaweza kutamba umevuna lakini wanaweza kuwa watu kama Guninita, Kasaka, Stephen Wassira, Prince Bagenda, Daniel Nsanzugwanko, Festus Limbu, Nzugile Jidulamambasi (hayati), Thomas Ngawaiya na wengineo.
Prince Bagenda ameyumba kimsimamo kuanzia enzi za vuguvugu la kudai mageuzi (NCCR), katibu wa NCCR-Mageuzi, mwenyekiti wa Mageuzi Asilia (chama chake kipya kilichoshindwa kupata usajili wa awali), akarudi NCCR-Mageuzi, akaenda TLP halafu CUF na sasa amerudi kwenye chama alimochomoka, CCM. Anatafuta nini?
Tumtazame Thomas Ngawaiya. Alikuwa muumini mzuri wa mageuzi akiwa NCCR-Mageuzi na baadaye TLP akimfuata Mrema ambako alikuja kufanikiwa kuwa mbunge jimbo la Moshi Vijijini.Baada ya kushindwa kutetea kiti chake ndani ya TLP na kwamba hawezi kurudi bungeni Dodoma ‘alitibuana’ na Mrema.Ukweli Ngawaiya alikuwa anatafuta ‘atoke vipi’ kwani siku chache baadaye ‘akaonekana barabarani’ anaringia fulana za kijani na njano huku akimponda mwenyekiti wake wa zamani kuwa ni mroho wa madaraka.
Kioja ni kwamba Ngawaiya huyohuyo, akaanza pilika za kuomba ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kupitia Mkoa wa Kilimanjaro. Alikosa lakini walimpoza kwa kumpa uenyekiti wa WAZAZI, mkoa wa Kilimanjaro.
Tangu Januari mwaka huu amekuwa akitangaza nia ya kumvua ubunge Phillemon Ndesamburo wa CHADEMA. Je, huo si uroho wa madaraka?
Mashushushu wako kazini, wasio na kumbukumbu nzuri watatumiwa kuandika habari iaminike kwamba Mpendazoe ni mroho wa madaraka.
Watatutumia ionekane mtu akirudi CCM akawania madaraka si mroho ila yule anayewania kupitia upinzani akitokea CCM. Huo ni mtazamo finyu.
Mageuzi hawatamsahau Dk. Amani Walid Kabourou. Alikuwa mwiba mkali kwa CCM alipokuwa katibu wa CHADEMA. Alipambana na kumvua ubunge Azim Premji wa CCM katika Jimbo la Kigoma Mjini na akawa alama ya upinzani.
Alipolegea katika utendaji aliondolewa, na baadaye akarudi CCM ambako sasa ni mbunge wa Afrika Mashariki. Wanaomjua Dk. Kabourou wanajiuliza hadi leo: Ilikuwaje?

No comments: