Friday, 18 July 2014

YANAYOWAKUTA WATU WA MOMBASA NA WAZANZIBARI PIA WAINGIZWA KAPUNI

Kitendo cha hivi karibuni kwa kuvamiwa watu huko Zanzibar usiku wa manane wakiwa wameitwa ati kuhojiwa na Polisi na baadae kupakiwa kwenye Ndege za Kijeshi na kupelekwa Tanganyika kama vile Zanzibar imekosa mahakama , imewashangaza wengi kuwa kosa liliofanyika Zanzibar vipi lihamishiwe Tanganyika jee vipi Serikali ya Zanzibar imekua ni kijiji kisicho na taasisi zake za kisheria , Wataalamu wetu wanatuambia kuwa ni ukweli Serkali imeshindwa kuwakamata wahusika wa vurugu na sasa harufu ya siasa imeingia kwenye new theater video kama hizi zina siri kali ambazo huko mbeleni huenda ukweli ukapatikana. Yanayotokea huko Palestine kwa serkali ya EGYPT kuimaliza kikundi cha Hamas chenye uhusiano wa kikundi kilicho shinda uchaguzi cha Muslim Brother hood sasa serkali ya CCM imekusidia pia kuwatia misuko suko watu wote waliokuwa washabiki wa kundi la Kidini la Uamsho nawasiokuwawafuasi wa CCM kwa kisingizio cha Kutaka mabadiliko Visiwani Zanzibar sasa Serkali ya CCM inatumia mwanya ya matukio ya uhalifu Visiwani Zanzibar kwa kisingizio cha kuwakamata wafuasi wa wanaiopinga CCM. La kusikitisha pia huko Mji wa Arusha kulitokea matukio kama haya ya ugaidi ila ukamataji wa wtau kiholela umekua tofauti na haya yaliotokea Zanzibar usiku wa manane na watu kujiuliza nani kesho atachukuliwa usiku wa manane kwenye nyumba yake.na kuaicha familia yake ikiwa imechanganyikiwa kwenye mwezi huu wa Ramadhani.Leo Upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka ambaye ni wakili wa serikali mwandamizi Prosper Mwangamila ulidai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam


Na Mwandishi wetu Mohammed Ghasani ,Kauli za Wazanzibari juu ya vita juu ya Waislamu wa Zanzibar kutoka kwenye serkali ya CCM   !Miezi michache iliopita Rafiki yangu mmoja aliniambia kuna habari kwenye gazeti fulani isome uone vita ya kidini unanvyopandikizwa Afrika Mashariki ila sasa niemyaona mambo haya yanaingizwa akilini mwetu.

Najuwa wako wengi humu  ambao wanamjua Rashid Nyange, pengine kuliko ninavyomjuwa mimi. Wako wengi waliofanya naye kazi na waliofaidika na ukarimu wake uliopindukia mipaka na utayarifu wake wa kujitolea. Lakini najua pia hawako wengi wanaothubutu kuinuka wakapinga balaa analozushiwa sasa na taasisi za usalama za dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wana sababu zao. Si lazima nizikubali zote, lakini naziheshimu. Ila mimi sitanyamaza. Nitasema. RASHID SI GAIDI.

Ni makosa ambayo wanadaiwa kutenda kati ya Januari mwaka 2013 na Juni 2014 katika maeneo tofauti Tanzania.Katika kesi zote mbili dhidi ya washtakiwa hao Upande wa mashtaka uliiambia mahakama iliyokuwa chini ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo bi Hellen Riwa kuwa upelelezi bado unaendelea na hivyo kuiomba mahakama kuahirisha kesi hizo hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Julai.
Awali mapema asubuhi msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania Bi Advera John Bulimba aliwealeza waandishi wa habari kuhusu tuhuma dhidi ya washtakiwa hao
Hii ni mara ya kwanza kwa kundi kubwa la watuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa pamoja wakikabiliwa na tuhuma za makosa ya kigaidi huku mtandao wa kijamii wa facebook nao ukitajwa kuhusika katika kutawanya taarifa za kuwezesha kutenda makosa hayo.

No comments: