Wednesday 26 November 2014

CCM YAZIDI KUZAMA KWENYE WIZI WA TEGETA ESCROW













ESCROW  NA MCHAKATO WA  KURA ZA MAONI CCM 2015 .IPTIL  Ripoti imekwisha wasilishwa na kubaini mapungufu kadhaa baina ya watendaji na kupelekea upotevu wa bilioni 306. Mapendekezo Kuwajibishwa kwa Mwanasheria mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na naibu wake, Katibu mkuu wa nishati na madini. Kuvunjwa kwa bodi ya shirika la umeme la Tanesco Kufuta umiliki wa PAP iliyoinunua IPTL inayomilikiwa na Harbinder Singh Seth pamoja na kuchukuliwa hatua za sheria Kuundwa kwa chombo kitakacho shughulikia rushwa kubwa ukiachia TAKUKURU na chombo hicho kuwa na mamlaka ya kuchunguza na kupeleka mashtaka mahakamani. Kufilisiwa kwa mali pamoja na kurudishwa fedha kwa wahusika wote waliopokea mgao wa fedha pamoja na wale watumishi wa Serikali kufukuzwa kazi.
Kuangaliwa kwa utaratibu mpya utakaovitazama vyombo vilivyoshiriki utakatishwaji wa fedha na hatua za kisheria kuchukuliwa (STANBIC na Mkombozi Commercial Bank) Kutaifishwa kwa mitambo ya IPTL na kupelekwa TANESCO. Kusimamia mapendekezo ya kamati wa Mwakyembe wakati wa mawasilisho ya kashfa ya Richmond  Maamuzi yatategemea taarifa ya Kamati ya Uongozi ya Bunge itakayotolewa tarehe 27/11/2014 pamoja na mijadala ya Wabunge itakayoendelea tarehe 28/11/2014 TETESI ZA WEREMA, TIBAIJUKA KUNG'ATUKA Hatimaye mwanasheria mkuu wa serikali bwana Fredrik Werema amekubali rasmi kung'atuka katika cheo hicho baada ya ripoti ya PAC kuwekwa rasmi hadharani huku waziri mkuu Mizengo Pinda akisema anasubiri hatma yake katika majadiliano  yatakayofanyika bungeni.  Aidha waziri prof. Anna Tibaijuka naye amekubali kung'atuka baada ya ripoti ya PAC kusomwa bungeni. Hayo yameamuliwa katika kikao cha CCM chini ya Philip Mangula kilichomalizika mjini Dodoma leo alfajiri. Pinda amesema kuwa hatma yake iko mikononi mwa wabunge kama watapitisha kwa kauli moja kuwa ang'atuke yupo tayari kufanya hivyo kutokana na ripoti ya PAC kutokumuwajibisha kwa lolote lile. Ripoti ya PAC imewawajibisha kwa uzembe AG Werema, Saada Mkuya- fedha, Muhongo Sospeter- Nishati na madini na gavana Beno Ndulu.Aidha wengine ni vigogo wote wa juu wa Tanesco. Kwa upande mwingine bunge litaamua  hatma ya waziri mkuu pamoja na mawaziri wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu huku wakikwepa sekeseke la kuwajibishwa na PAC. Kikwete anatarajiwa kurejea kesho usiku ambapo atalazimika kumteua AG mpya na kulisuka upya baraza la mawaziri na kama wabunge wataamua kumsulubu Pinda( kutokana na utashi wao kwani hajabanwa na PAC) basi Kikwete atalazimika kuiunda upya serikali. 

Utafiti wa awali  unaeleza, pamoja na Prof. Tibaijuka, vigogo kadhaa  nao wamelamba asilimia kubwa  ni wagombea Urais wa CCM 2015. (1) Ngeleja amepata dola 400,000 (2) January Makamba dola 800,000 (3) Werema dola 2,000,000 (4) Jack Gotham dola 1,800,000 huyu ni mpambe mkuu wa Bernad Membe na fedha hizi zimetolewa kwa ajili ya uchaguzi. (5) Ndg Nawaab Mullah dola 2,500,000 amepokea kwa Niaba ya Pinda kuchangia Mfuko wa Kampeni za 2015 .  Mullah ndie ambae wanashirikiana na  kampuni tanzu ya Home Shopping Centre kwenye Mradi wa Umeme wa Kinyerezi na Pinda anawasaidia ili serikali itoe Goverment Guarantee Wapewe mikopo. huu mradi escrow ni cha Mtoto Ufisadi uliopo ktk Dili hii.  Tanesco walitangaza Tenda ktk Gazeti la The Citizen mwezi April/May kwa mwaka 2014  na walimpatia tenda za dola milioni 150 Kampuni ya  tanzu  ya  Home shopping Centre kwa ajili ya Kuipatia Tanesco Nguzo za Umeme.   Tend ya Nguzo  Kinyerezi  ina  harufu ya ufisadi wa dola milioni 150. Pinda kwa sasa Anapiga Dili za vibali vya Sukari na Zakaria Hanspope, wanapitisha bila kulipa kodi  inadaiwa amekuwa akimtumia afisa wa serikali anayeitwa Masamaki.
 Mtikisiko! Serikali, CCM wahamia Dodoma. Pinda, Kagasheki watoleana uvivu Hali sasa ni dhahiri si shwari tena mjini Dodoma.Pilikapilika za magari ya vigogo pamoja na ndege ndivyo vinavyotawala kwa sasa katika mabarabara na uwanja wa ndege! Katika hali ambayo si ya kawaida, vigogo wa ngazi za juu wa CCM pamoja na serikali wameingia Dodoma kwa fujo hivi leo huku makamu wa rais dr. Mohamed Gharib Bilal akitarajiwa kutua hapa mchana wa leo tayari kuongoza kikao kutokana maelekezo aliyopewa na rais Jakaya Kikwete. Jana waziri Prof. Mark Mwandosya aliitwa Dar kwa dharura na tayari amerudi Dodoma leo asubuhi na mapema akiongozana na vigogo wakuu wa CCM wakiwemo Kinana na Mangula. Katika tukio jingine mbunge Hamisi Khagasheki amejikuta katika mtifuano mkubwa na wanaomuunga mkono Pinda baada ya kumtuhumu waziwazi waziri mkuu Pinda katika mitandao ya kijamii kuwa ni mwizi ambaye hakupaswa kusubiri hadi leo. Miongoni mwa waliomjia juu Khagasheki ni John Komba huku akimdhihaki kuwa anaona gere baada ya kutoswa uwaziri! CCM hapa Dodoma imepasuka vibaya sana kwani kuna wakati Pinda anazomewa waziwazi na wanaCCM wenzake wakiwamo wabunge hali inayoashiria kuwa sasa uwaziri mkuu wa Pinda umefikia tamati! Bado hali ni ngumu na inaelekea Dr. Bilal anakuja na ujumbe kutoka kwa rais Kikwete.Pia tayari imethibitika kuwa zote hizo ni jitihada za kumnusuru Pinda ingawa Werema, Tibaijuka Muhongo, Masele na Maswi watalazimishwa kwa mara nyingine kujiuzulu leo. Hawa wote wameambiwa iwe isiwe ni lazima wang'oke kabla ripoti haijapelekwa bungeni! Bernard Membe anapofanya juhudi za kuiangusha serikali yake Na Nyangeta Marwa,  Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Barnard Membe anatuhumiwa kufanya kampeni nzito kwa wabunge waishambulie na kuiangusha serikali bungeni kupitia saakata la Escrow. Mpango huu unaendeshwa kwa usiri na umakini wa hali ya juu huku kachero huyo wa zamani akiwatumia wabunge wa upinzani na si wa chama chake CCM.  Taarifa zilizovuja kutoka ndani ya kambi ya Membe zinaeleza kuwa Membe anaitumia nafasi hii ya sakata la ESCROW kama fimbo ya kujiimarisha kuelekea 2015 kwa kumshughulikia mtu anayetajwa kumvurugia upepo wake wa kisiasa waziri mkuu Mizengo Pinda. Katika kufanikisha jambo hili, Membe anatumia ushawishi na hata kuwahonga fedha baadhi ya wabunge wa upinzani akimtumia mpambe wake wa karibu ambae ndiye humtumia katika kusimamia mipango yake ya urais Jack Steven Gotham.  Inasemekana Membe ameamua kuendesha mkakati huu kwa siri kubwa akiwa amejificha nyuma ya kivuli cha waziri mkuu wa zamani EDWARD LOWASSA ambaye ndiye anatajwa kuwa anawatumia wabunge kumshambulia Pinda na serikali ili ajiuzulu kama njia ya kumsafishia njia ya Urais 2015. Hivyo Membe ametumia akili zake za ukachero kucheza na fikra za watu, na kufanya kampeni ya siri kumuondoa Pinda. Aidha, Membe amekataa kuwatumia wabunge wa CCM akihofia kuwa watavujisha siri. Hadi sasa maelfu ya dola na shilingi yameendelea kutumika kufanikisha kazi hii. Taarifa za ndani zinaonesha kuwa Membe amekuwa akivujisha siri na kuwapa wabunge hao juu ya mipango inayofanywa na serikali kukabiliana na sakata hili. Chanzo cha kuvuja kwa habari hii ni baadhi ya wabunge hawa kuzungumza na wenzao wa CCM. Mpambe wa Membe, Jack Gotham amekuwa ndiye muwakilishi wa Membe katika vikao vyake vya kushawishi watu wamuunge mkono Membe. Aidha amekuwa akimuwakilisha Membe katika vikao vya kusaka pesa za kampeni. Kabla ya kutua Dodoma, Jack alikuwa katika ziara ya nchi za kiarabu ambako Membe anasemekana kupata fedha za kampeni ya Urais.  Hongera Membe. Tuungane kuiangusha serikali.Endelea na moyo huo wa kuwasaidia wabunge wetu wa upinzani. Mpambe huyu wa Membe ndiye aliyesaidiwa kupata tenda ya mabilioni ya shilingi ya vitambulisho vya taifa ambavyo hadi leo bado vimekua ndoto. Jack Gotham ambae ametua na kujichimbia Dodoma kwa siri kubwa, amekuwa akifanya vikao na wabunge mbalimbali ili kufanikisha zoezi hilo.  Baadhi ya wabunge ambao tunawahifadhi wanaotoka vyama vya upinzani wameitwa na kupewa maelekezo maalum ya kuhakikisha kuwa wakati wote Pinda ashambuliwe, achafuliwe na kushinikizwa awajibike kisiasa kwa kujiuzulu. Baada ya maelekezo wabunge hao walipewa fedha za kimarekani USD kama posho ya kazi kufanikisha anguko la Mizengo Pinda.  Mgawanyiko wa Wabunge, Mchakato wa Urais 2015 na Mgongano wa kimaslahi baina ya wafanyabiashara na wanasiasa. Wabunge wa Bunge la Tanzania wamegawanyika waziwazi juu ya issue ya Escrow na wengine wakiomba muda uongezwe ili kuwaumbua wale wanaotumika na kambi moja ya urais ili kupotosha umma juu ya fedha za Escrow. Hapa kuna kambi mbili tena wengine huwa ni maadui lakini ktk hili sakata wameungana kwa mda ili wakimaliza lengo kila mmoja aludi kule kwa zamani. Kuna Kambi ya Mhongo,naibu wake,mawaziri wa zamani wa nishati,Maswi,Werema, Tibaijuka, pinda na wenzao kibao.  Kuna kambi ya Mzee mengi, mkono, Zito, kafulila na wenzao wakiwemo wahindi kibao wenye Mgongano wa kimasilahi huko wizara ya Nishati. Hapa wengi si kwamba wana Uchungu na IPTL Bali wana usongo na Waziri Mhongo baada ya kuwanyima Vitalu vya Gesi huku Mkono akinyang'anywa Tenda za kisheria ameungana na Mzee mengi kupambana na Mhongo kwa nia ya kupigania Masilahi Yao Binafsi lakini sasa wanasaka Huruma za watu ili wawasaidie kujinufaisha.  Hilo kundi la Werema wao wanatuhumiwa kujitotea mkwanja wa IPTL peke Yao pasipo kuwamegea akina Mkono ndiyo Maana wahindi wapinzani wa Yule Singasinga mmiliki wa IPTL wamechanga Pesa wakampatia Mengi akawapatia Zito na kafulila ili wapaze Sauti akiamini Kuwa Mhongo atajiuzulu na yeye kujitwalia Vitalu vya Gesi kiulani, Hapa kikubwa ni Mgongano wa Masilahi Kati ya Mengi na Mkono. vs Maswi na Mhongo, Wenye Uchungu na pesa ni Wananchi pekee lakini hao akina Mkono wapo after money tu. 

No comments: