Wakifurahia jambo nje ya mahakama.MWENYEKITI wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, na wanachama wenzake ambao mwanzo walifunguliwa kesi ya kushiriki maandamano haramu, wamepewa dhamana upya katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Dhamana hiyo imetokana na kesi yao ya awali ambayo ilifutwa na kuanza kupitiwa upya.
MWENYEKITI wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, na wanachama wenzake ambao mwanzo walifunguliwa kesi ya kushiriki maandamano haramu, wamepewa dhamana upya katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Dhamana hiyo imetokana na kesi yao ya awali ambayo ilifutwa na kuanza kupitiwa upya.
Katika kupewa dhamana upya, watuhumiwa hao japokuwa walikuwa nje kwa dhamana, walitakiwa kufika leo na wadhamini wawili kila mmoja na kusaini karatasi ya maandishi yenye kiasi cha thamani ya Shilingi milioni mbili kila mmoja.
Watuhumiwa wote walikidhi vigezo.
Pia, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, alihudhuria mahakamani hapo na kusema amefurahishwa na kitendo cha hakimu kwa kuwapatia dhamana watuhumiwa wote.
‘’Nimefurahishwa na kitendo cha hakimu kufuata sheria na kuhakikisha watuhumiwa wamepata dhamana na hata wadhamini wao kujitokeza,” alisema.
Mwendesha Mashtaka wa kesi hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkeha, alitaja shauri hilo kusikikilizwa tena Mei 6. Watuhumiwa wote wanakabiliwa na kosa la kutaka kufanya mkutano na maandamano pasipokuwa na kibali.
No comments:
Post a Comment