Msafara wa Viongozi wa UKAWA. Kutoka Kushoto Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, Mbunge wa Singida Mashariki Mh Tundu Lissu, Mbunge wa Kigoma Kusini Mh David Kafulila, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Patrobas Katambi na mwanausalama wa CHADEMA. Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA ambaye pia ni mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Tundu Lissu akihutubia umati mkubwa wa wakazi wa Jiji la Arusha katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro katika mkutano uliokuwa katika sura ya UKAWA kwa kuwashirikisha NCCR Mageuzi.
Mkutano huo nusura uathiriwe na mvua kubwa iliyonyesha wakati Mbunge wa Kigoma Kusini Mh David Kafulila akihutubia lakini mapenzi ya wafuasi wa CHADEMA kwa chama na viongozi wao yaliwafanya wavumilie kunyeshewa mpaka mwisho. Viongozi walikataa kukingwa na mvua hiyo na kujikuta wote wakilowa mwili mzima kama wananchi wengine.
Katika hotuba yake, Mh Lissu aliwaeleza wakazi wa Arusha kitendo cha Serikali ya CCM kukorofishana na karibu kila kundi la jamii kwa kutaja wafanyabiashara, walimu, madaktari, madereva, wafanyakazi n.k ni ishara kuwa chama hicho kimechokwa na kinaweza kuondoka madarakani katika Uchaguzi wa mwaka huu ambao alisisitiza ni lazima ufanyike mwaka huu.
Mh Lema akiwatambulisha viongozi wa Kata ya Ngarenaro na kueleza namna walivyoingilia kati hujuma ya kuchimbua uwanja huo mkutano usifanyike. Yupo diwani Doita
Msafara wa viongozi ukuindoka uwanjani hapo mara baada ya mkutano kumalizika. Wananchi waliwazonga kiasi cha kusababisha kazi ya ziada kwa wanausalam
No comments:
Post a Comment