Tuesday 25 August 2015

Lowassa aendelea ukiteka Dar

Lowassa sokoni Tandale, Agosti 25, 2015
Lowassa sokoni Tandale, Agosti 25, 2015 (picha via WhatsApp)
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limepiga marufuku wagombea Urais wa Tanzania 2015 kufanya mikusanyiko isiyokuwa rasmi kutembelea vituo vya daladala, bodaboda au katika masoko na kutakiwa wafuate ratiba iliyotolewa na tume ya uchaguzi ya kufanya mikutano au kampeni ili kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa wananchi.
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda hiyo CP, Suleiman Kova mesema marufuku hiyo inatokana na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao wamedai kuwa mikusanyiko hiyo imekuwa ikisababisha msongamano wa magari hususan katikati ya jiji pamoja na maeneo mengine.

Kova ametolea mfano kitendo cha jana cha mgombea Urais, Mhe. Edward Lowassa cha kufanya ziara ya kushtukiza kwa wananchi na kupanda daladala. Amesema ziara hiyo ya Mhe. Lowassa na mgombea mwenza wake Juma Duni Haji walitembelea Gongo la Mboto, ingeweza kuhatarisha usalama wa wananchi kwa kuwa watu wengi walikusanyika na wengine kuacha kazi zao.

Mgombea wa Urais kupitia UKAWA, Edward Lowassa pamoja na mgombea mwenza Juma Duni Haji hii leo wamewashitukiza wafanyabiashara katika soko la Tandika na mengineyo jijini Dar es Salaam.

Aidha, wagombea hao waliwasili katika soko hilo asubuhi ya leo ambapo shughuli zilisimama kwa muda. Kabla ya kuanza mazungumzo na wafanyabishara hao, Lowassa alikaribishwa chai na mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo.

Ziara hiyo ya kushitukiza iliyoanzia Mbagala siku ya jana ni maalumu kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa "hali ya chini" kuhusiana na matatizo yanayowakumba katika maisha yao ya kila siku.

Jesh la polisi limesema mikusanyiko hiyo isiyo rasmi inaweza kusababisha madhara kwa mgombea Urais kwa kuwa polisi wanakuwa hawana taarifa ili waweze kutoa ulinzi katika eneo husika.

  • Taarifa hii imenukuliwa kutoka blogu kadhaa na ChannelTEN



































Mgombea wa Urais kuoitia Ukawa, Edward Lowassa akiangalia maharage katika soko la Tandale jijini Dar es Salaam, leo wakati wa ziara take ya kuangalia hali ya masoko ya jijini Dar es Salaam.

Askari Polisi wakifanya mahojiano na dereva wa gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya mgombea urais wa UKAWA kupitia Chadema alipotembelea masoko ya jiji la Dar es Salaam.


Askari wa doria wakiwa wamezuia msafara wa Edward Lowassa baada ya kuvamiwa na waendesha bodaboda.


Mgombea wa Urais wa Ukawa akinunua maji ya kandoro katika eneo la soko la Tandika jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea masoko ya chakula jijini Dar es Salaam.

Mgombea mwenza, Duni Haji Duni akiwapungia mkono wakazi wa Tandika.


Lowassa akihojiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala, Lucas Mkondya.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala, Lucas Mkondya.

Lowassa akipita katika soko la mitumba Tandika.

Lowassa akipata maelezo katika soko la samaki la Tandika Dar es Salaam.

No comments: