Monday, 24 August 2015

Lowassa apokewa mitaani kwa Kishindo


Info Post
8/24/2015 06:38:00 PM

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika kituo cha mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo. Mh. Lowassa aliianza ziara yake eneo hilo la Gongo la Mboto na baadae alipanda daladala mpaka Pugu Kajiungeni, jijini Dar.


Lowassa akimsikiliza Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es Salaam leo.


Lowassa akizungumza na vijana wanaoendesha Bodaboda waliokuwepo kando ya Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.


Lowassa akiwa katikati ya umati wa watu wakati alipotembelea eneo la Gongo la Mboto mwisho.


Lowassa akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliokuwa kituoni hapo kusubiria usafiri.


Lowassa akiwa ndani ya Daladala alilopanda kutokea Gongo la Mboto Mwisho mpaka Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaam, mapema leo asubuhi. 

Mhe. Lowassa akishuka kwenye daladala.
Wakazi wa mji wa Mbagala wakiushangilia msafara wa mgombea Urais wa Tanzania 2015, Lowassa pamoja na mgombea mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakati walipotembelea kituo cha mabasi cha Mbagala Rangi tatu jijini Dar es Salaam, wakati walipotembelea kituo hicho leo


Lowassa akizungumza na Vijana wanaojihusisha na shughuli mbali mbali katika stendi kuu ya Mabasi yaendayo mikoa ya Lindi na Mtwara, ilipo Mbagala jijini Dar.


Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia wakazi wa Mbagala.


  • Picha, taarifa tumeshirikishwa na Othman Michuzi/Mtaa kwa Mtaa blog.

No comments: