Sunday 23 August 2015

UCHAMBUZI, WA UZINDUZI WA MKUTANO WA CCM JANGWANI.


MAMBO 20 NILIYOJIFUNZA KWENYE MKUTANO WA CCM
JANGWANI.
1. Yamoto Band wameshangiliwa zaidi kuliko Magufuli,
2. Wakati Mbowe amewakutanisha Lowasa na Sumaye. Leo
Jakaya amewakutanisha Diamond na Ali Kiba Jangwani,
3. CCM wanajua kuwa mikutano ya UKAWA inapata
mafuriko, kwa hiyo nao walijitahidi wapate "mafuriko"
4. Watu wengi wameenda kuwashangaa wasanii, sio
kumsikiliza Magufuli. Kumuona Diamond bei ghali, leo
wamemuona Live bila kiingilio wataacha kwenda?
5. Magufuli anajua lugha nyingi za makabila kuliko
anavyojua matatizo ya wananchi,
6. Mkapa anahitaji maombi ya kufunga maana anazeeka
vibaya. Amemuita Mpumbavu, Waziri Mkuu aliyemteua
mwenyewe na kufanya nae kazi miaka 10,
7. Mwisho wa mikutano ya siasa ni saa 12 kamili lakini CCM
wamezidisha dakika hadi 12:40. Ikiwa wameshindwa
kutekeleza Sheria waliyoiweka mwenyewe, watawezaje
kutekeleza ahadi zao? CCM hawapaswi kuaminiwa,
8. Kitendo cha Magufuli kukiri serikali inanyanyasa
Machinga na mama Ntilie ni kukiri kuwa serikali yake
imechoka na inahitaji kubadilishwa,
9. Magufuli amemvua nguo Kikwete hadharani. Kusema
anashangaa meno ya tembo yamefikaje uarabuni ni
kusema kuwa JK anashiriki biashara hiyo. Ikiwa Magufuli
amesema atazuia biashara hiyo haramu, nini kimemshinda
JK kuzuia kwa sasa?
10. Magufuli anajua kuwa CCM inakaribia kufa. Wakati
akimalizia hotuba yake ametoa mfano ambao
haukueleweka vizuri, lakini fundisho lake ni kuwa
WATANZANIA MSIIUE CCM. Kumbe anajua kuwa CCM
itakufa,
11. Ccm wamewadharau sn watanzania kwa kuwapandisha
malori ya kubebea vitunguu, nyanya na viazi. Mtanzania
aliyepandishwa lori leo akiipigia kura CCM atadhihirisha
kuwa yeye ni kiazi,
12. Mzee Warioba ameshindwa kabisa kumnadi Magufuli
kwa hoja. Kwa namna alivyojieleza anaweza kuzidiwa na
kijana aliyemaliza form four akapata division zero,
13. Mzee Mkapa ana matusi "makali" kuliko wafanyakazi
wa bar,
14. Bila msaada wa malori na kujazia bodaboda mafuta,
uwanja wa Jangwani leo ungekua mtupu,
15. Warioba anaipenda CCM zaidi ya anavyoipenda
Tanzania,
16. Rais Kikwete amekiri kuwa Magufuli alikua chaguo lake,
it means hakuwa chaguo la wanaCCM. Kwa lugha rahisi
Kikwete amedhihirisha kuwa alienda Dodoma akiwa na
majina yake mfukoni kama ilivyodaiwa,
17. Kwa kuwa Polepole alikiri Warioba ni "Role Model" wake,
leo tumemjua anayemtuma Polepole kutukana UKAWA,
18. Jeshi la Polisi linatumika kisiasa. Wameshindwa kuzuia
maandamano "haramu" ya CCM na kuzuia mkutano ilipofika
saa 12 kamili km sheria inavyotaka,
19. Miongoni mwa watu wanaopaswa kuchunguzwa
UKAWA ikishika dola ni pamoja na Jaji Joseph Warioba na
Mzee Mkapa,
20. CCM haifai kuendelea kuwa madarakani baada ya
October 25.

No comments: