Sunday, 13 September 2015

Mgombea wa UKAWA Tanga afariki kwa ajali ya gari.


Nimesoma kwa masikitiko na majonzi kuhusu ajali iliyompata kaka Mohamedi Mtoi aliyekuwa akiwania Ubunge katika jimbo la Lushoto kwa tiketi ya CHADEMA na mwavuli wa UKAWA.

Nimesikitika sana kusikia kuwa ameaga dunia.

Nilimfahamu Mtoi kupitia mawasiliano ya intaneti baada ya yeye kuniandikia kwa utani na baadaye nikagundua kuwa alikuwa mmoja wa wanafunzi wa mama yangu katika Chuo cha Ualimu Korogwe.

Tangu nifahamiane naye kwa miaka mitatu, tumekuwa tukiwasiliana hapa na pale hasa kwa machapisho yake kadha wa kadha aliyokuwa akiyatuma na kwa salamu alizokuwa akinitumia punde anapoonana na kumjulia hali Mama yangu.

No comments: