Sunday, 11 October 2015

Mgombea Mwenza wa Chadema JUMA DUNI anguruma Dodoma

I HAJI AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI DODOMA

Mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji akihutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe mkoani Dodoma. 

Mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji akimnadi mgombea wa Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Benson Kigaila kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe mkoani Dodoma.
Mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji akimnadi kwa wananchi wa Bahi mgombea wa Ubunge Jimbo la Bahi, Mathias Lyamundu kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Kongogo mkoani Dodoma.
Wakazi wa Dodoma wakimsikiliza mgombea mwenza wa urais Chadema anayeungwa mkono na Ukawa akizungumza katika mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe.
Waendesha Bodaboda wakimsindikiza mgombea mwenza wa urais, Juma Duni Haji wakati alipomaliza kuhutubia wakazi wa Dodoma katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe.
Kikundi cha ngoma cha Moto Kali kutoka Ibiwa wakicheza ngoma ya kumkaribisha mgombea mwenza wa urais wa Chadma Juma Duni Haji kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Kongogo mkoani Dodoma.
Aliyekuwa mbunge wa Mkanyageni Zanzibar, Habibu Mohamed Mnyaa akihutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe mkoani Dodoma.
Wakazi wa mjini Dodoma wakifuatilia mkutano huo.

Wazee katika mkutano.

Chanzo - Vijimambo Blog

No comments: