Sunday, 11 October 2015

Uchaguzi huu ni nani mwenye number au mikoa yenye wapiga kura wengi.2013 nchini Kenya alitokea mwanazuoni moja aliyepata umaarufu sana katika vyombo vya habari na hata kwa wananchi.

Mutahi Ngunyi aliibuka na " Tryanny of Numbers Kenya" falsafa kubwa katika hii hypothesis ilikuwa ni kuonyesha uwiano wa kura watakazopata muungano wa Jubilee (Uhuruto) na ule wa CORD (Raila na Kalonzo)..

Mutahi Ngunyi kwa mahesabu yake na kwa kuangalia uandikishaji wa kadi za mpiga kura kwa jamii ya GEMA, Kalenjin, Luo, na Kamba alisema wazi kuwa Uhuruto na muungano wao wa Jubilee watashinda urais, tena kwenye firts round. Na kwa hakika hicho ndicho kilichotokea...

Mutahi Ngunyi alieleza mapema kabisa kuwa uchaguzi ni mahesabu. Na kama hauna numbers usijaribu kuingia kwenye uchaguzi... Kuna ambao watasema siasa za Kenya ni tofauti na za Tanzania, hawako sahihi..

Uchaguzi wa sasa lazima tukubali mgombea atapata kura kadri anavyokubalika katika eneo husika (we call it block). Uchaguzi wa sasa utaangalia nani aliinvest mapema kwa wananchi. Uchaguzi wa sasa utaangalia zaidi jina na umaarufu wa mgombea husika. Uchaguzi wa sasa utaangalia mtandao waliojiwekea kwa miaka 20 au zaidi iliyopita.

Uchaguzi wa sasa utaangalia nguvu waliyonayo kwa kundi la vijana. Uchaguzi wa sasa utaangania ni jinsi gani unaungwa mkono na makundi maalum kama machinga, bodaboda, mamantilie ambao ndio wako wengi zaidi.

Lowassa ambaye ni mgombea wa Chadema na anayeungwa mkono na umoja wa Ukawa ana kila dalili za kushinda huu uchaguzi. Lowassa alijipanga sana kwa muda mrefu, zaidi ya miaka 20. Lowassa alijipanga kwa wananchi (na kumbuka hii ni kampeni yake ya pili anafanya, baada ya ile ndani ya CCM aliyozunguka nchi nzima, na karibia wilaya zote).

Lowassa aliwekeza kwenye vyombo vya usalama. Lowasaa aliwekeza kwenye chombo cha mahakama. Lowassa aliwekeza ndani ya usalama. Na kubwa zaidi Lowassa aliwekeza kwenye jumuiya za kijamii....

Ukitumia methodology ya Mwanazuoni Mutahi Ngunyi lazima utaona kwamba Lowassa atakuwa na uwakika wa kushinda katika mikoa mingi. Tena mikoa ambayo ina idadi kubwa ya wapiga kura... Lowassa ana100% confidence level kushinda, mikoa ifuatayo....

1. Dar es Salaam
2. Mbeya
3. Mwanza
4. Arusha
5. Tanga
6. Kilimanjaro
7. Mara
8. Geita
9. Kagera
10. Shinyanga
11. Singida
13. Pemba
14. Mtwara
15. Ruvuma (*upepo unaweza kubadilika)
16. Njombe
17. Iringa
18. Manyara
19. Katavi

Ukipiga mahesabu kwa hiyo mikoa, ni wazi Lowassa atashinda. Haya sio maajabu wala miujiza. Ukitumia fomula ya Muhayi Ngunyi huwezi kuwa na wasiwasi kwenye hili (kwa kujua fomula husika, goolge Mutayi Ngunyi "Election hypothesis")...

Huu uchaguzi sio miujiza. Tofauti kubwa ni kwamba Lowasaa kaingia kwenye huu uchaguzi akiwa tayari ana numbers kama ilivyokuwa kwa Uhuruto. CCM hasa "mgombea wa CCM" kaingia kwenye huu uchaguzi kwa mara ya kwanza wakiwa hawajui idadi yao kamili ya kura watakazopata kwenye mikoa husika na hata wilaya husika...

Lowassa alihamasisha sana wananchi hasa vijana kujiandikisha kwa wingi. Lowassa alikuwa na makundi zaidi ya 6 yanayomuunga mkono, na hayo makundi yalifanya kazi kubwa sana ya kuhamasisha vijana kujiandikisha kwa wingi sana. Na ndio mana leo hii tunaona kwamba vijana zaidi ya asilimia 68.58% ndio waliojiandikisha (NEC, record)....

NB: Naomba niwambie wazi kabisa, CCM kushinda huu uchaguzi ni ndoto. Ukawa/Lowassa watashinda tena kwa asilimia nyingi sana...

Baada ya siku 15 nitarudi tena hapa. Na kwa hakika mtasema Ocampo four kawa Mutahi Ngunyi wa Tanzania....

No comments: