Tuesday 3 November 2015

CCM Yazidi kutapa tapa Zanzibar

Balozi Seif akutana na viongozi wa Dini na kusema Serikali kuwachukulia hatua waliohusika kuharibu uchaguzi ila la kujiuliza ni nani aliotaka kuvuruga uchaguzi kama sioi CCM au Genge la wahafidhina litachukuliwa hatua ?
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Vongozi wa Dini mbali mbali Nchi mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Balozi Iddi alimua kujibu mapigo baada ya Kumuona Makam owa Kwanza wa RAis alieshinda uchaguzi Maalim Seif amekutana na viongozi wa dini huko Zanzibar 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo katika kusaka amani Zanzibar
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo katika kutafuta ufumbuzi wa mkwamo wa kisiasa Zanzibar
Kufuatia taarifa iliyotolewa na Ikulu Dar es Salaam, na pamoja na jitihada za awali za Makamu wa Kwanza wa Rais na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kujaribu kuwasiliana na Rais Jakaya Kikwete kwa njia ya simu, leo hii Maalim Seif amemuandikia barua rasmi kumuomba wakutane ili kuzungumzia hali ya kisiasa ya Zanzibar kufuatia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

No comments: