Saturday, 26 December 2015

Jipu la Zanzibar linahitaji mtu mwenye meno ya kweli sio mnafiki.

Matokeo ya kukosa uthubutu kwa Mkapa na Kikwete sio tu kwamba yameendelea kuwa muendelezo wa uhuni wa kila baada ya miaka mitano visiwani Zanzibar, bali pia wote wawili wameondoka na kuiwachia hali kuwa mbaya zaidi kuliko walivyoikuta. Wote waliyawachia makundi ya kihalifu yaundwe na yatekeleze hujuma dhidi ya maisha na mali za wananchi wa Zanzibar – majanjawidi yaliundwa wakati wa utawala wa Mkapa na Kikwete ameondoka akiyaacha mazombi na masoksi – huku wao wakiyaangalia hayo kuwa ni “matatizo ya Wazanzibari wenyewe.” Lakini jumuia ya kimataifa inaingalia Tanzania kwa ujumla ndio yennye mamlaka ya vyombo vya ulinzi kulinda raia na mali zao na usalama wao.http://mwanahalisionline.com/mazombi-wahangaika-kuvamia-cuf/
Lakini Rais Magufuli amejipatia mwenyewe jina la “mpasua majipu”, ambalo linamaanisha kuwa “mtu mwenye kuthubutu.” Ikiwa kweli upasuaji wake majipu utaakisika kwenye suala la Zanzibar, hapana shaka atafanikiwa. Na wala hapaswi kuchimba mbali sana. Kwa mfano, akiwa rais na amiri jeshi mkuu wa nchi, ana nyenzo na taasisi za kumpa taarifa zote za ukweli wa nini kilifanyika Zanzibar ndani ya miaka 10 iliyopita na nini kinaendelea sasa. Ndani ya ripoti hizo, muna mikasi ya kutosha ya kulipasua jipu la Zanzibar, sindano za kushonea, dawa za kulipaka na bendeji za kulifungia. Baada ya miaka mitano tu, kitakachobakia kitakuwa ni kovu na sio tena kidonda.
Naamini Wapo wana CCM wanaooona chama chao kinaharibiwa na kundi hili dogo linalotumia violence kwa upande wa Zanzibar ndio njia ya kubaki madarakani lakini chama chote kinaingia doa kwa sababu ya kundi hili dogo lililokosa maadili .CCM kamna kweli inataka kujisafisha kwa Wazanzibari kionekana tena kuwa ni chama cha kiistarabu kinahitaji kuwatema wahafidhina waliokichafua chama hichi na kukikosesha ushindi na kuonekana ni genge la kihuni machon imwa wazanzibari.
Ikiwa MAgufuli na jeshi lake wana meno ya kweli kukisafisha chama chao tutayaona meno ya Magufuli kwa upande huu wa pil iwa muungano unamsubiri kwa hamu .Njia pekee kwa Magufuli kuisafisha njia CCM na jina la Tanzania huku nje ni kukubali demokrasia ifuate mkondo wake .Atakua ni Kipenzi  cha majority ya Wazanzibari au atabaki na siasa zilizooifelisha CCM zanzibar na kuifanya CCM ionekane ni chama kisichoheshimu haki za binadamu kila baada ya uchaguzi kisa kulilinda kundi hili la wahafidhina.
Hatari kubwa inayoikabili serkali ya MAgufuli ni kupoteza credibilty kwenye mezani ya kimataifa mfano wa hivi karibuni kunyiwa msaada wa Millenium Challenge ni onyo la kutosha kuwaamsha wanaomtaka MAgufuli angare kwenye medani za Kimataifa.


No comments: